TANZIA Ajinyonga kwa wivu wa mapenzi akiwa na ujauzito wa miezi tisa

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,193
4,661
Ni habari mbaya ya kusikitisha mno kutokea Seregeti.

Mwili wa mwendazake akiwa na ujauzito wa miezi tisa ulikutwa juu ya mti wa mwembe ukiwa umening'inia na hii ni baada ya kugunduliwa na Watoto.

Inaelezwa kuwa sababu ya Mama huyo kuamua kuchukua uamuzi huo wa kujinyonga ni changamoto ya wivu wa mapenzi.

Polisi waendelea na uchunguzi na watatoa taarifa kwa umma.

------
MWANAMKE mmoja amejinyonga kwa kutumia kanga kwenye mti wa mwembe katika kijiji cha Itununu wilayani Serengeti, kwa madai ya wivu wa mapenzi, huku akiwa na mimba ya miezi tisa.

Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu, alithibitisha kwamba Mkami Nyamhanga (21) alijinyonga Januari 17. 2021, kwenye mti wa mwembe uliopo shambani.

Alisema mwili wake ulionwa na watoto waliokuwa wanakwenda kuangua matunda kwenye mwembe huo na ndiyo waliotoa taarifa ya kifo hicho. Kwa mujibu wa babu wa marehemu amedai alikuwa anamtuhumu mume wake kuwa na mpenzi mwingine.

Asubuhi alitoka bila kuaga mpaka alipogundulika amejinyonga kwa kutumia kitanzi cha nguo ambayo alifunga kwenye tawi la mwembe na kuning’inia,”alisema na kuongeza:

“Mganga aliyefanya uchunguzi alibaini kuwa kifo chake kimetokana na kitanzi shingoni kilichosababisha mzunguko wa damu na hewa kukosekana. Ndugu walikabidhiwa mwili kwa ajili ya kuuzika na hakuna mtu aliyekamatwa lakini uchunguzi unaendelea.’’

Mganga mfawidhi wa zahanati ya Itununu, Melick Salapioni, alilieleza Mwananchi kuwa mwanamke huyo alikuwa na mimba inayokaribia miezi tisa.

Alisema kutokana na mama kujiua, alikata mawasiliano ya hewa ya oksijeni kati yake na mtoto na hivyo kusababisha kichanga hicho kufa.
 
Ni habari mbaya ya kusikitisha mno kutokea Seregeti.

Mwili wa mwendazake akiwa na ujauzito wa miezi tisa ulikutwa juu ya mti wa mwembe ukiwa umening'inia na hii ni baada ya kugunduliwa na Watoto.

Inaelezwa kuwa sababu ya Mama huyo kuamua kuchukua uamuzi huo wa kujinyonga ni changamoto ya wivu wa mapenzi.

Polisi waendelea na uchunguzi na watatoa taarifa kwa umma.

MCL

Mmh!
Huyu
Mwendazake ?
Mwendawazi kabisa
😢
Sasa kisa cha kuua na kujiua
Kisa wivuuu!! Wa ub#o

Na akafanywe Kuni huko jehamu...
 
Duuh!! Hakutaka hata kukiwaza alichonacho tumboni kwamba ndo kinamuhitaji zaidi. Lol.

Apumzikage kwa amani tu mana huyo aliyemuonea wivu saa hii anaendelea na mambo zake.
 
Back
Top Bottom