Ajinyonga kwa kutumia Mtandio Baada ya Kugombana na Mumewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajinyonga kwa kutumia Mtandio Baada ya Kugombana na Mumewe

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Jul 21, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,204
  Likes Received: 3,995
  Trophy Points: 280
  MWANAMKE mmoja aliyetambulika kwa jina la Pendo Kimaro [21] amejinyonga kwa kutumia kitambaa cha kujitanda kichwani [mtandio] baada ya hasira ya kugombana na mumewe. Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari jijini Dar es SaLaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema kuwa, tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 4 asubuhi huko Kurasini jijini Dar es SaLaam.

  Kova amesema kuwa, polisi wamepata taarifa kutokana na mume wa dada huyo aliyetambulika kwa jina la Shija Kabaho [25] kuja kutoa taarifa katika kituo cha polisi.

  Amesema kuwa mume huyo aliieleza polisi kuwa kulitokea mfarakano kati ya wana ndoa hao na kusema kuwa wakati alipotoka kwenda kwenye shughuli zake aliporudi alimkuta mke wake huyo ameshafariki.

  Amesema kuwa aliporudi nyumbani alimkuta mkewe huyo amekufa na kugundua kuwa alijitundika kwa kutumia mtandio wake ambao ulikuwa umefungwa kwenye dali ya nyumba hiyo.

  Amesema mwili huo umechukuliwa na kwenda kuhifadhiwa hospitali ya Temeke na uchunguzi wa kina unaendelea kubaini chanzo halisi cha kifo hicho.
  http://nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=2578702&&Cat=1
   
Loading...