Ajificha kwenye tairi la ndege kutoka Afrika Kusini mpaka Uholanzi

Polisi wa kijeshi nchini Uholanzi leo wameshangazwa kumkuta mtu aliyekuwa amejificha chini ya ndege kwenye eneo la tairi la mbele kuwa yuko salama.

Ndege hiyo ilisafiri kwa saa 11 kutokea Afrika mpaka Ulaya.

Ndege hiyo ya mizigo ilitokea Afrika Kusini na kutua Kenya kwa muda mfupi kabla ya kuelekea Amsterdam, Uholanzi.

Mtu huyo ambaye uraia wake, jinsia na umri bado havijatajwa sasa yuko hospitali na hali yake inaendelea vizuri.

Uchunguzi kuhusu tukio hilo bado unaendelea lakini Polisi hao wamesisitiza kuwa "hii ni ngumu kuielewa, ukizingatia baridi ya sehemu alipokuwa amejificha na urefu kutoka usawa wa bahari ndege hiyo aina ya Boeing 747 ilipokuwa".

===
Polisi wa Uholanzi wanasema wamempata mtu akiwa hai katika sehemu ya gurudumu la ndege iliyotua katika uwanja wa ndege wa Amsterdam wa Schiphol kutoka Afrika Kusini.

Safari za ndege kutoka Johannesburg hadi Amsterdam huchukua takriban saa 11, huku ndege ya mizigo ikiaminika kusimama mara moja, jijini Nairobi, Kenya.

Si jambo la kawaida sana kwa wanaopanda ndege kimagendo kuishi, kutokana na baridi na oksijeni kidogo kwenye miinuko ya juu.
Umri na utaifa wa mwanaume huyo bado haujabainishwa, polisi wanasema.

"Mwanaume huyo alipatikana akiwa hai katika sehemu ya gurudumu upande wa pua ya ndege na alipelekwa hospitalini akiwa katika hali nzuri," msemaji wa Polisi wa Kijeshi wa Uholanzi Joanna Helmonds aliambia shirika la habari la AFP.

"Inashangaza kwamba mtu huyo bado yuko hai," alisema. Kwa mujibu wa mtangazaji wa Uholanzi NOS, joto la mwili wa mtu huyo liliongezeka katika eneo la tukio na wakati gari la wagonjwa lilifika, aliweza kujibu maswali ya msingi.

Msemaji wa idara ya shehena ya mizigo Cargolux alithibitisha katika barua pepe kwa Reuters kwamba mtu huyo alikuwa kwenye ndege inayoendeshwa na Cargolux Italia.

Kulingana na data ya ndege, ndege pekee ya Cargolux ya mizigo kutoka Johannesburg hadi Schiphol Jumapili pia ilisimama Nairobi.
Haijulikani iwapo mwanaume huyo alipanda ndege hiyo nchini Afrika Kusini au Kenya.
WaAfrika tuna roho ngumu sana sababu ya shida zilizokumba watu. Mungu amfanyie wepesi na apewe uraia na nchi nzuri ughaibuni itakayomjali
 
Back
Top Bottom