Ajifanyia upasuaji kwa kutumia kisu hii kali jamani ............. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajifanyia upasuaji kwa kutumia kisu hii kali jamani .............

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by MziziMkavu, Nov 8, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  MWANAMUME raia wa Marekani aliyekuwa na matatizo ya ugonjwa wa ngiri aliamua kujifanyia upasuaji kwa kujichana kwenye tumbo ili kutatua tatizo na kisha aliwasha sigara na kuchoma sehemu ya kidonda.Polisi walimkuta mtu huyo akiwa amevua nguo kwenye nyumba yake Los Angeles nje ya mji wa

  Glendale katika jimbo la California, Jumapili baada ya mke wake kuwapigia simu kuwafahamisha kuhusu jaribio la mume wake kujifanyia upasuaji
  , msemaji wa Polisi Glendale, Sajenti Tom Lorenz alisema.

  "Alijichana mwenyewe kwa kutumia kisu cha mkate," Lorenz alisema. "Alimwambia mke wake kuwa alikuwa akichanganywa na maumivu ya ngiri, na hakutaka kusubiri zaidi kwa ajili ya kutibiwa kwa dawa."

  Maafisa wa polisi walimwona mtu huyo, baada ya kutoa kisu kwenye tumbo lake, kuweka sigara katika kidonda, alisema Lorenz.

  "Sijui kama alikuwa akitaka kujiunguza au kitu chochote," alisema.

  Polisi hawakumtaja mtu huyo, lakini Lorenz alisema hakufanya kosa na kwamba inawezekana alishawishiwa na dawa za kulevya au kulewa.

  Alipelekwa katika hospitali ya Los Angeles ijulikanayo kama USC Medical Center ambapo aliwekwa kwa saa 72 kuchunguzwa akili.

  Spoti Starehe | www.spoti.co.tz
   
 2. THK DJAYZZ

  THK DJAYZZ JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Khaaa na hofu na brain yake.
   
 3. ngulinho

  ngulinho JF-Expert Member

  #3
  Nov 8, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 336
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hili si jukwaa la madaktari wala wagonjwa! na log off!!!!!
   
 4. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #4
  Nov 8, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Ganzi jeee aka anaesthesia
   
 5. driller

  driller JF-Expert Member

  #5
  Nov 8, 2011
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 1,119
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  we inabidi upelekwe na huyo jamaa mkaangaliwe huenda mnaumwa ungonjwa mmoja..!
   
Loading...