Ajeruhiwa na Mumewe kwa Wivu wa Kimapenzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajeruhiwa na Mumewe kwa Wivu wa Kimapenzi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, Jul 21, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  MWANAMKE mmoja aliyetambulika kwa jina la Mariam Hassan[23]mkazi wa Sinza jijini Dar es SAlaam, amejeruhiwa na mumewe kutokana na sababu za wivu wa kimapenzi kwa kuwa aliongea na simu kwa muda mrefu na rafiki yake kitendo ambacho mumewe kilimuudhi Mwanamke huyo alijeruhiwa usoni kwa kupigwa magumi na muwewe huyo kwa kile kilichosemekana mumewe alipatwa na jazba kwa kuwa aliongea na simu kwa muda mrefu na mtu ambaye hakumfahamu.

  Dada huyo akiongea na Nifahamishe alisema kuwa juzi alipigiwa simu na rafiki yake ambaye kwa muda mrefu walikuwa wamepotezana.

  Alisema kuwa mtu aliyempigia simu alikuwa ni kijana aliyemtaja kwa jina moja la Hamisi ambaye walisoma wote shule ya msingi Mapambano iliyopo Sinza jijini Dar.

  Alisema kuwa aliongea na kijana huyo zaidi ya masaa matatu na baada ya kumaliza kuongea na simu hiyo aliulizwa na muwewe alikuwa anaongea na nani na kumjibu ni rafiki yangu anaitwa Hamisi nilisoma nae ndio amenipigia.

  Kumbe mumewe huyo wakati anajibiwa hivyo na mkewe huyo hakuridhika majibu hayo na kumwambia kuwa alikuwa akiongea na mpenzi wake na kuanza kumpa kichapo ambacho hakukitegemea kwa wakati huo.

  Alisema alijitahidi kujitetea kadri alivyoweza lakini muwewe huyo hakuridhika na kumshambua na kumwambia anadiriki kuongea na mabwana zake mbele yake.

  Dada huyo alijeruhiwa sehemu zake za usoni na kupelekea hadi kupata uvimbe na kuvilia damu kwa ngumi ambazo alitandikwa na muwewe huyo. http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2533394&&Cat=1
   
Loading...