Ajeruhiwa baada ya kukataa kulipa shilingi 50 kwenye daladala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajeruhiwa baada ya kukataa kulipa shilingi 50 kwenye daladala

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Gudboy, Dec 24, 2009.

 1. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  KIJANA mmoja jina halikuweza kupatikana mara moja, mwenye umri kati ya 28 na30 amejeruhiwa na konda wa daladala baada ya kugoma kulipa shilingi 50 kwenye daladala hali iliyomfanya konda wa gari hilo kupandisha hasira na kuanza kupigana


  Hali hiyo ilitokea leo majira ya saa 3 za asubuhi, kwenye basi la abiria lililokuwa likifanya safari zake Mbezi Posta.


  Kijana huyo alipanda kwenye daladala hiyo katika kituo cha Kimara StopOver na kumpatia konda huyo shuilingi 300 kwa ajili ya nauli na kumwambia kuwa anashuka Manzese Tiptop ndipo ndipo konda alipomuamuru aongezee shilingi 50 kwa kuwa nauli yakutokea hapo alipopanda hadi anaposhuka ni shilingi 350.


  Kijana huyo alimwambia konna kuwa anashojua yeye nauli ya hapo ni shilingi mia 300 na kumwambia konda kwua hana 50 na atashuka pindi gari hilo litakapofika kituo chake husika.


  Kutokana na kauli hiyo konda alipanda na jazba na kuanza kujibizana na kijana huyo hali iliyofanya kuwe na mvurugano katika gari hilo kati ya konda na abiria.


  Hivyo gari hilo lilipofika maeneo ya Mahakama ya Ndizi kijana huyo alimuamuru amshushe kituo kinachofuaata ndipo konda aliponmwambia hatashuka hadi atoe 50.


  Kijna huyo aliamua atoe uvivu na kuanza kumkunja kodna na kuanza kupigana hali iliyofanya abiria wamuamuru dereva wa gari aweke pembeni gari hilo.


  Katika pulukushani hiyo kijana huyo aliweza kujerruhiwa maeno yake yausoni na abiria kuamuru dereva wa gari hilo apelike polisi gari hilo kwa ajili ya usalama.


  Hivyo konda, dereva na kijana huyo walitakiwa wabaki kituoni hapo wka ajili ya maelezo huku badhi ya abiria kumtetea kijana huyo.


  Hadi nifahamishe inaondoka eneo hilo limeacha abiria waliokuwemo kwenye basi hilo kutafuta usafiri mwingine na habari juu ya tukio hilo litafuatiliwa na kuwajia zaidi.

  Nifahamishe.com
  Na Pilly Kigome, Dar
   
Loading...