WanaJF,
Ningeomba wana CHADEMA msaidie Watanzania kuelewa kuhusu ajenda ya kupinga ufisadi ndani ya chama chenu kupitia uzi huu.
Kwa maana Watanzania wote wamekifahamu chama chenu (CHADEMA) kwa ajenda hii ya kupinga ufisadi na sio kwa jambo lingine lolote lile. Ni ajenda ya ufisadi ndio iliipa CHADEMA nguvu na nikiri tu, ajenda hiyo ndio ilikuwa ikiitoa CCM jasho kwa wakati ule kabla Lowassa na genge lake hawajatoka rasmi CCM.
Na kumbukumbu zinaonyesha kuwa ajenda ya ufisadi ilikuwa ikisimamiwa kikamilifu na Dkt Slaa kipindi akiwa katibu mkuu wa CHADEMA. Ni mara chache sana kuona viongozi wengine waandamizi wakikemea ufisadi kama ambavyo alikuwa akikemea Dkt Slaa.
Sasa tangu Dkt Slaa atoke rasmi ndani ya CHADEMA, mimi na Watanzania wengi hatujasikia kabisa CHADEMA ikikemea ufisadi au hata kumpongeza rais aliyepo madarakani ambae tangu ameingia amekuwa akiwasaka mafisadi kwa nguvu zake zote.
Je, ajenda ya ufisadi imepotelea wapi huko CHADEMA? Je, ajenda ya ufisadi ilikuwa ni ya chama ama ya Dkt Slaa pekee!? Kama ni ya chama, iweje tangu Dkt Slaa atoke CHADEMA, chama kimekuwa bubu kuhusu ufisadi!? Je, CHADEMA itabaki hai pasipo kukemea ufisadi kama ilivyokuwa huko zamani?