Nigrastratatract nerve
JF-Expert Member
- Sep 4, 2019
- 1,390
- 3,896
WAZEE WATATULIWE CHANGAMOTO ZAO, WASITUMIKE KUHALALISHA MATAKWA YA WATAWALA
Jana Rais Samia Suluhu Hassan alikutana na wanaoitwa "wazee wa Dar es Salaam" katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City.
Kama kawaida, wazee walipigwa "sound", wakapiga makofi, wakapiga picha, wakala FUTARI wakarejea nyumbani kama walivyokuja.
Matarajio ya kuondoka na majawabu ya changamoto zao yaliyeyuka, badala ya majibu waliambulia ahadi za miaka yote. Kwa ufupi hakuna jipya na kutumainia katika mkutano wao na mzee mwenzao, Mama Samia (Miaka 61).
Wazee walitegemea bima zilizoimarishwa, kiinua mgongo, mikopo ya riba nafuu, kuwajibishwa kwa wanaochelewesha mafao yao na mengine mengi lakini hakuna lililotatuliwa bali walichagizwa kuwa wavumilivu.
Unahubirije subira na uvumilivu kwa mzee mwenye miaka 70 au 80, umri wa kufa kwa mujibu wa Biblia Takatifu? Mzee anakuelewa kweli?
Mahitaji wa kundi la wazee yalipaswa kushughulikiwa kwa uharaka wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa sababu wengi wao wamefikia umri wa kuondoka duniani muda wowote na pia wazee ni kundi dogo sana nchini lisilofikia milioni 4.
NYUMA YA PAZIA
Rais alitumia muda mwingi kuwaomba wazee waiunge mkono serikali yake badala ya kutumia muda huo kuondosha changamoto zao. Kumbe nia ya wanasiasa kukutana na wazee ni kutafuta uungwaji mkono na baraka katika mambo yao na katu lengo siyo kushughulikia masuala ya wazee kama wanavyolaghaiwa.
Jana Rais ametumia fursa kuwaomba wazee waunge mkono masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na
👉Kurejesha ziara katika nchi mbalimbali kwa kivuli cha kusalimia majirani
👉Kuitumbukiza Tanzania katika biashara ya Corona
👉Kufanya uteuzi wa viongozi anavyojisikia
👉Kutoshughulikia kero za wananchi wakiwemo wazee kwa kisingizio cha kishuka kwa uchumi. Yaani uchumi ni mbaya kwenye kero za wazee lakini uchumi uleule ni mzuri katika kufanya ziara za kujitambulisha kwa majirani.
Narudia tena, wazee wanastahili kuheshimiwa na namna moja ya kuwaheshimu wazee ni kumaliza changamoto zinazowakabili. Wazee wasitumiwe kupata uhalali wa maamuzi ya wanasiasa hasa maamuzi yasiyo na manufaa kwa taifa.
Nawasalimu kwa Jina la Mwenyezi Mungu aliyeumba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!
Kazi Iendelee 🇹🇿🇹🇿