Ajenda ya Corona na Wazee wa Dar es Salaam; Usizunguke zunguke, nyooka kama rula

Nigrastratatract

JF-Expert Member
Sep 4, 2019
686
1,000
WAZEE WATATULIWE CHANGAMOTO ZAO, WASITUMIKE KUHALALISHA MATAKWA YA WATAWALA

Jana Rais Samia Suluhu Hassan alikutana na wanaoitwa "wazee wa Dar es Salaam" katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City.

Kama kawaida, wazee walipigwa "sound", wakapiga makofi, wakapiga picha, wakala FUTARI wakarejea nyumbani kama walivyokuja.

Matarajio ya kuondoka na majawabu ya changamoto zao yaliyeyuka, badala ya majibu waliambulia ahadi za miaka yote. Kwa ufupi hakuna jipya na kutumainia katika mkutano wao na mzee mwenzao, Mama Samia (Miaka 61).

Wazee walitegemea bima zilizoimarishwa, kiinua mgongo, mikopo ya riba nafuu, kuwajibishwa kwa wanaochelewesha mafao yao na mengine mengi lakini hakuna lililotatuliwa bali walichagizwa kuwa wavumilivu.

Unahubirije subira na uvumilivu kwa mzee mwenye miaka 70 au 80, umri wa kufa kwa mujibu wa Biblia Takatifu? Mzee anakuelewa kweli?

Mahitaji wa kundi la wazee yalipaswa kushughulikiwa kwa uharaka wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa sababu wengi wao wamefikia umri wa kuondoka duniani muda wowote na pia wazee ni kundi dogo sana nchini lisilofikia milioni 4.

NYUMA YA PAZIA

Rais alitumia muda mwingi kuwaomba wazee waiunge mkono serikali yake badala ya kutumia muda huo kuondosha changamoto zao. Kumbe nia ya wanasiasa kukutana na wazee ni kutafuta uungwaji mkono na baraka katika mambo yao na katu lengo siyo kushughulikia masuala ya wazee kama wanavyolaghaiwa.

Jana Rais ametumia fursa kuwaomba wazee waunge mkono masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na

πŸ‘‰Kurejesha ziara katika nchi mbalimbali kwa kivuli cha kusalimia majirani

πŸ‘‰Kuitumbukiza Tanzania katika biashara ya Corona

πŸ‘‰Kufanya uteuzi wa viongozi anavyojisikia

πŸ‘‰Kutoshughulikia kero za wananchi wakiwemo wazee kwa kisingizio cha kishuka kwa uchumi. Yaani uchumi ni mbaya kwenye kero za wazee lakini uchumi uleule ni mzuri katika kufanya ziara za kujitambulisha kwa majirani.

Narudia tena, wazee wanastahili kuheshimiwa na namna moja ya kuwaheshimu wazee ni kumaliza changamoto zinazowakabili. Wazee wasitumiwe kupata uhalali wa maamuzi ya wanasiasa hasa maamuzi yasiyo na manufaa kwa taifa.

Nawasalimu kwa Jina la Mwenyezi Mungu aliyeumba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Kazi Iendelee πŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡Ώ
 
Tui

JF-Expert Member
Jun 2, 2018
1,099
2,000
Hivi unasoma unachokiandika? Isije ukawa kama kasuku anatamka maneno kwa kukariri lakini hajui analotamka lina maana gani.
 
Torque vs HP

JF-Expert Member
Jan 7, 2021
1,782
2,000
Jiwe alitatua changamoto gani za wazee?

Jamaa aliwaondolea mpk dawa za ma pressure wazee huko nhif.

Mtetezi wa wanyongeeeeee.
 
Kambaku

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
3,981
2,000
Kwanini 'mungu' wako hakusovu vyote hivyo katika miaka yake sita aliyotawala na unataka mama asovu katika miezi yake 2?
 
Pac the Don

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
708
1,000
Hivi unasoma unachokiandika?Isije ukawa kama kasuku anatamka maneno kwa kukariri lakini hajui analotamka lina maana gani.
Achana na taga hilo kazi yake kubwa ni kum-prove wrong Rais Samia.
 
Distant Relatives

JF-Expert Member
Nov 21, 2020
420
1,000
Kwa hiyo mzee wewe umeamua kuwa hater wa Rais Samia. Pole sana maana kuwa hater ni kazi ngumu sana.

By the way, hakuna mtawala asiyetaka kuungwa mkono na makundi ya kijamii. Ni kanuni ya utawala. Hata JPM unayemsuhudu alifanya haya.

Swali, hivi mzee anaweza kukopeshwa? Akafanye biashara gani? Huo uwezo wa kufanya biashara anao? Mzee anahitaji kutunzwa, kulelewa na kuhudumiwa na sio kukopeshwa.
 
Abunuas

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
8,772
2,000
WAZEE WATATULIWE CHANGAMOTO ZAO, WASITUMIKE KUHALALISHA MATAKWA YA WATAWALA

Jana Rais Samia Suluhu Hassan alikutana na wanaoitwa "wazee wa Dar es Salaam" katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City.

Kama kawaida, wazee walipigwa "sound", wakapiga makofi, wakapiga picha, wakala FUTARI wakarejea nyumbani kama walivyokuja.

Matarajio ya kuondoka na majawabu ya changamoto zao yaliyeyuka, badala ya majibu waliambulia ahadi za miaka yote. Kwa ufupi hakuna jipya na kutumainia katika mkutano wao na mzee mwenzao, Mama Samia (Miaka 61).

Wazee walitegemea bima zilizoimarishwa, kiinua mgongo, mikopo ya riba nafuu, kuwajibishwa kwa wanaochelewesha mafao yao na mengine mengi lakini hakuna lililotatuliwa bali walichagizwa kuwa wavumilivu.

Unahubirije subira na uvumilivu kwa mzee mwenye miaka 70 au 80, umri wa kufa kwa mujibu wa Biblia Takatifu? Mzee anakuelewa kweli?

Mahitaji wa kundi la wazee yalipaswa kushughulikiwa kwa uharaka wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa sababu wengi wao wamefikia umri wa kuondoka duniani muda wowote na pia wazee ni kundi dogo sana nchini lisilofikia milioni 4.

NYUMA YA PAZIA

Rais alitumia muda mwingi kuwaomba wazee waiunge mkono serikali yake badala ya kutumia muda huo kuondosha changamoto zao. Kumbe nia ya wanasiasa kukutana na wazee ni kutafuta uungwaji mkono na baraka katika mambo yao na katu lengo siyo kushughulikia masuala ya wazee kama wanavyolaghaiwa.

Jana Rais ametumia fursa kuwaomba wazee waunge mkono masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na

πŸ‘‰Kurejesha ziara katika nchi mbalimbali kwa kivuli cha kusalimia majirani

πŸ‘‰Kuitumbukiza Tanzania katika biashara ya Corona

πŸ‘‰Kufanya uteuzi wa viongozi anavyojisikia

πŸ‘‰Kutoshughulikia kero za wananchi wakiwemo wazee kwa kisingizio cha kishuka kwa uchumi. Yaani uchumi ni mbaya kwenye kero za wazee lakini uchumi uleule ni mzuri katika kufanya ziara za kujitambulisha kwa majirani.

Narudia tena, wazee wanastahili kuheshimiwa na namna moja ya kuwaheshimu wazee ni kumaliza changamoto zinazowakabili. Wazee wasitumiwe kupata uhalali wa maamuzi ya wanasiasa hasa maamuzi yasiyo na manufaa kwa taifa.

Nawasalimu kwa Jina la Mwenyezi Mungu aliyeumba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Kazi Iendelee πŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡Ώ
huo uzee wameupata kipindi cha Samia tu? Anyway rekodi yako inajulikana; ulimtukana Kikwete weeee mpaka ukachoka alipokuja magu ukaunga tela, ameondoka magu umerudi kule kule kumsakama Samia, hushangazi kila kukicha ni kuanzisha thread za kumtukana Samia tu humu; kwa nini usingespend huo muda wako kumhudumia mumeo huo uchi wako?
 
imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
28,646
2,000
e39fe5862b98b7c9bbd8e484154e0743.jpg
 
myoyambendi

JF-Expert Member
Sep 13, 2013
102,486
2,000
Uzi kama hizi zinaonyesha kulikuwa na mgawanyiko....Unga mkono tu mkuu maana hakuna namna
 
hydroxo

JF-Expert Member
Oct 19, 2015
1,582
2,000
WAZEE WATATULIWE CHANGAMOTO ZAO, WASITUMIKE KUHALALISHA MATAKWA YA WATAWALA

Jana Rais Samia Suluhu Hassan alikutana na wanaoitwa "wazee wa Dar es Salaam" katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City.

Kama kawaida, wazee walipigwa "sound", wakapiga makofi, wakapiga picha, wakala FUTARI wakarejea nyumbani kama walivyokuja.

Matarajio ya kuondoka na majawabu ya changamoto zao yaliyeyuka, badala ya majibu waliambulia ahadi za miaka yote. Kwa ufupi hakuna jipya na kutumainia katika mkutano wao na mzee mwenzao, Mama Samia (Miaka 61).

Wazee walitegemea bima zilizoimarishwa, kiinua mgongo, mikopo ya riba nafuu, kuwajibishwa kwa wanaochelewesha mafao yao na mengine mengi lakini hakuna lililotatuliwa bali walichagizwa kuwa wavumilivu.

Unahubirije subira na uvumilivu kwa mzee mwenye miaka 70 au 80, umri wa kufa kwa mujibu wa Biblia Takatifu? Mzee anakuelewa kweli?

Mahitaji wa kundi la wazee yalipaswa kushughulikiwa kwa uharaka wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa sababu wengi wao wamefikia umri wa kuondoka duniani muda wowote na pia wazee ni kundi dogo sana nchini lisilofikia milioni 4.

NYUMA YA PAZIA

Rais alitumia muda mwingi kuwaomba wazee waiunge mkono serikali yake badala ya kutumia muda huo kuondosha changamoto zao. Kumbe nia ya wanasiasa kukutana na wazee ni kutafuta uungwaji mkono na baraka katika mambo yao na katu lengo siyo kushughulikia masuala ya wazee kama wanavyolaghaiwa.

Jana Rais ametumia fursa kuwaomba wazee waunge mkono masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na

πŸ‘‰Kurejesha ziara katika nchi mbalimbali kwa kivuli cha kusalimia majirani

πŸ‘‰Kuitumbukiza Tanzania katika biashara ya Corona

πŸ‘‰Kufanya uteuzi wa viongozi anavyojisikia

πŸ‘‰Kutoshughulikia kero za wananchi wakiwemo wazee kwa kisingizio cha kishuka kwa uchumi. Yaani uchumi ni mbaya kwenye kero za wazee lakini uchumi uleule ni mzuri katika kufanya ziara za kujitambulisha kwa majirani.

Narudia tena, wazee wanastahili kuheshimiwa na namna moja ya kuwaheshimu wazee ni kumaliza changamoto zinazowakabili. Wazee wasitumiwe kupata uhalali wa maamuzi ya wanasiasa hasa maamuzi yasiyo na manufaa kwa taifa.

Nawasalimu kwa Jina la Mwenyezi Mungu aliyeumba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Kazi Iendelee πŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡Ώ
Musiba utapata tabu sana.
 
UHURU JR

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
11,320
2,000
Kwanini 'mungu' wako hakusovu vyote hivyo katika miaka yake sita aliyotawala na unataka mama asovu katika miezi yake 2?
Ni kweli hakusovu na ndio maana alikuwa anakosolewa na hadi sasa bado anakosolewa, na kwa sababu Mama kapokea hiyo mikoba na anaendeleza kutokusovu matatizo basi pia kukosolewa kunahamia kwake na lawama anabeba yeye.
 
UHURU JR

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
11,320
2,000
Hili taga litawapozea muda wenu bure, huyo ni anti Samia mpingaji wa Rais kila angle.
Jiwe nae kulikuwa wanaomsifia kwa kila jambo na kuna waliyokuwa wanampinga kwa kila jambo. Hivyo na Samia nae ndio inakuwa hivyo hivyo labda tofauti ni wapinzani ndio kugeuka timu kusifu na wao sasa wamemtengeneza mungu wao wa kike.
 
Pac the Don

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
708
1,000
Jiwe nae kulikuwa wanaomsifia kwa kila jambo na kuna waliyokuwa wanampinga kwa kila jambo. Hivyo na Samia nae ndio inakuwa hivyo hivyo labda tofauti ni wapinzani ndio kugeuka timu kusifu na wao sasa wamemtengeneza mungu wao wa kike.
Hilo usemalo c kwel kuhusu upinzani, nadhan hujasikiliza hotuba ya mbowe maana ile hotuba ndio msimamo wa chama chao!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom