Ajenda hatari: Mishahara ya watumishi

Narudia tena Ukamongo wako mwisho mtaa wa Lumumba kwa makamongo wenzio siyo humu.

Kwani shule ya kata ukisoma inapelekea kuwa na mtindio wa akili? acha uzwazwa squared! kabiliana na ajenda
 
Kwani tusipowapandisha cheo na tusipowaongezea mishahara lakini mnapita kwenye flyovers na mnapanda dream liner hamuoni hayo ni maendeleo makubwa?
 
Safi
Mkuu umegusa mahali sensitive sana.

Kuna watu hawaitambui nguvu ya watumishi kwa sababu ya viburi vya Madaraka,hawafanyi maamuzi kulingana na miongozo iliyopo bali kwa utashi wao kupitia kauli zao wazitoazo.

Hili ni time bomb,watumishi anaowadharu atake asitake ndio watekelezaji wa Ilani ya chama chake na ndio watekelezaji wa shughuli mbalimbali za Serikali yake.

Haboreshi hali ya utendaji kazi zao,haboreshi maslahi yao halafu anawaamuru tena kwa ubabe wafanye kazi kwa bidii,hii si uongozi bora,anapaswa ajitafakari ingelikuwa ni yeye angekuwa na morali ya kufanya kazi kwa bidii?

Morali ya utendaji kazi ya watumishi wengi sana hasa wa ngazi za kawaida wasiokuwa wakuu wa idara au vitengo ambao ndio wengi serikalini imeshuka sana ktk kipindi hiki cha uongozi cha awamu ya 5,hii kikubwa ni sababu wamejikatia tamaa kwa kudhulumiwa haki zao kwa hoja zisizo na mashiko.

Kama serikali inawaona ni mzigo na wage bill ni mzigo mzito kwake,ifanye rentranchment kubwa,iwape chao,iache watumishi wachache walioboreshewa maslahi yao kuliko kung'ang'ania halafu unashindwa kuwatumia.
 
Sidhani kama wafanyakazi hasa wa umma nchini Tanzania wanaweza kuamka, kushikamana na kufanya maamuzi yoyote yenye tija kwa maslahi yao..
Wengi wao hawajui tofauti kati ya utumishi wao, kutetea maslahi yao, uzalendo na kutumika kisiasa..
Wengi wao wanajiona kama sehemu ya usalama wa taifa vile au kama watumishi waandamizi wa Magogoni..
Wanasahau kuwa wapo kwenye utumishi wa umma kwa sababu ya mikataba yao ya ajira na si vinginevyo...!
Liko tatizo kubwa
 
Kwani tusipowapandisha cheo na tusipowaongezea mishahara lakini mnapita kwenye flyovers na mnapanda dream liner hamuoni hayo ni maendeleo makubwa?
Kha....!
Hii ni hoja kali ya mwezi.
Kumbe dream liner zinapandwa bure bila transport fee.
Ngoja leo nijiandae nika ruke na ka dream liner kamoja.
Kama Wasabato Masalia waliweza mimi nitashindwaje
 
Back
Top Bottom