Ajari mbaya yatokea Lusaunga, watu wengi wahofiwa kufa, ni Basi la Taqwa na Roli

Bongo Pix Blog

JF-Expert Member
Sep 13, 2011
213
33
Taarifa nilizozipata toka eneo la ajari Lusaunga ni kuwa basi la Taqwa toka Dar es Salaam limengongana na roli la mizigo na watu zaidi ya 30 wanahofiwa kuwa wamekufa, shuhuda wa ajari ambaye amenipigia simu muda si mrefu, amesema ameona maiti wengi sana, wamelazimika kusitisha safari yao ya kikazi na kubeba majeruhi kuwaleta hospitali ya Biharamulo, Ninaelekea hospitali nitawajuza zaidi kilie kinachoendelea.

Updates:
Nimetoka Hospitali Teule Biharamulo, nimeshuhudia miili ipatayo 10 ikishushwa toka katika fuso, pia niliongea na afande mmoja akanambia kuwa walishaleta miili 2, hivyo inafanya idadi kuwa 12, majeruhi ni zaidi ya ishirini, hata hivyo idadi kamili na majina itapatikana baada ya kuongea na mamlaka husika RPC na Mganga Mkuu wa Hospitali, hali ni mbaya sana, yamegongana uso kwa uso, hivyo idadi ya vifo yaweza kuwa maradufu. Tembelea HAPA kwa picha na taarifa zaidi
 
Hata mie nimeambiwa kuwa basi limegogana na scania ya azam na maiti ni wengi sana ,Lusahunga n Bibaramulo hapa Kagera karibu na njiapanda ya kuelekea Kigoma na si mbali na mipaka ya Burundi na Rwanda. Ni pia karibu na mpaka wa Kagera na Shinyanga
 
Pole sana wafiwa.

Kuna haja ya kujiuliza, tumejifunza nini hizi ajali za kila siku?. Tatizo ni madereva au ni ubora wa magari?.

Kuna haja ya kufanya uchunguzi, bila hivyo tutakwisha wote.

Poleni sana majeruhi.
 
Jamani poleni sana; inasikitisha sana! Binafsi nilitegemea kupiitia njia hiyo hivi karibuni kwa kweli nimeshtuka sana. Anyway hatujui siku wala saa! Mwenyezi Mungu naomba atusaidie jamani!
 
Jamani poleni sana; inasikitisha sana! Binafsi nilitegemea kupiitia njia hiyo hivi karibuni kwa kweli nimeshtuka sana. Anyway hatujui siku wala saa! Mwenyezi Mungu naomba atusaidie jamani!

Ni ajari mbaya kwa kweli, nimeshuhudia maiti zaidi ya kumi zikishushwa toka kwenye Fuso zikiwa zimekatikakatika vibaya sana. Tutapada idadi kamili ya majeruhi na vifo baada ya kuongea na Mamlaka husika.
 
Mungu awapokee marehemu wote.Wafiwa poleni sana sote tutaonja maut japo ni vgum kufaham ni kifo kip kitatukuta!
 
Back
Top Bottom