Ajari kwa viongozi zazidi kuongezeka!

G.MWAKASEGE

Senior Member
Jun 29, 2007
153
15
Na Ramadhan Semtawa

AJALI za magari zimezidi kuwaandama viongozi wa serikali, baada ya Naibu Waziri wa Afrika Mashariki, Dk Diodarus Kamala, kunusurika baada ya gari aina ya Mitsubishi Prado aliyokuwa akisafiria kuchomoka gurudumu ya mbele.

Tukio hilo limetokea jana mkoani Kagera wakati Dk Kamala akitokea Kata ya Kasambya Kanazi kuelekea Kakunyu na gari hiyo mali ya serikali mkoa wa Kagera.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu kutokea eneo la tukio, Dk Kamala alisema hakupata madhara.

"Tupo Kakunyu, kutokea Kasambya Kanazi, gari lilichomoka gurudumu la mbele lakini nashukuru niko salama," alisema Dk Kamala.

Dk Kamala alisema katika msafara huo alikuwa na watu wengine watatu wakiwemo Benjamin Rwegasira na Raymond Wanai ambao ni waandishi wa habari na dereva ambaye hakumtaja jina na kwamba hakuna aliyejeruhiwa.

Dk Kamala alikwenda Kagera juzi akitokea Mkoa wa Mara, ambako alikuwa katika ziara ya kiserikali kueleza utekelezaji wa falsafa ya maisha bora kwa kila Mtanzania.

Hivi karibuni kumekuwa na ajali zinazokumba viongozi wa serikali, miongoni mwao ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Profesa Juma Kapuya aliyepata ajali mkoani Tabora na Mbunge wa Mchinga, Mudhihir Mudhihir, aliyepata ajali mkoani Lindi iliyosababisha mkono wake
 
AJALI za magari zimezidi kuwaandama viongozi wa serikali, baada ya Naibu Waziri wa Afrika Mashariki, Dk Diodarus Kamala, kunusurika baada ya gari aina ya Mitsubishi Prado aliyokuwa akisafiria kuchomoka gurudumu ya mbele.

Mkuu hii Mitsubish Prado ndio gari gani? Inawezekana serikali wameanza kununua magari mapya mengine hili litakuwa sio shangingi bali ni baraguzi
 
Sasa naona kasi imewageukia sasa kasi inaelekea ni kifo au kukatika shingo...utasikia tu lengine masiku haya haya...hadi wakome ujambazi wao wa kutotumia silaha..
 
Mkuu hii Mitsubish Prado ndio gari gani? Inawezekana serikali wameanza kununua magari mapya mengine hili litakuwa sio shangingi bali ni baraguzi

Hili gari litakuwa very special kwani kwa haraka naona ni makampuni mawili yanachangia gari moja yaani Mitsubishi na Toyota. Kama sio waandishi wetu uchwara na kuharibu maana halisi--nafikiri ni Mitsubishi Pajero sio Prado
 
Back
Top Bottom