Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,498
- 9,279
AJALI zinazosababishwa na magari binafsi zimezidi kuongezeka kwa kasi katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo wa mwaka huu na sasa inazidi hata vifo vya ajali zitokanazo na pikipiki maarufu kama bodaboda ambazo ndizo zilikuwa zikiongoza kwa kusababisha vifo.
Takwimu za Jeshi la Polisi katika kipindi cha miezi sita Januari hadi Juni 2019 zinaonesha kuwa magari binafsi ndiyo yamekuwa vinara wa kusabisha ajali zinazosababisha vifo na hata majeruhi.
Wadau wa usalama barabarani wanaonya kuwa hali inaweza kuwa mbaya zaidi kama hatua za haraka hazitachukuliwa, kwani kwa mujibu wa takwimu rasmi za Jeshi la Polisi (Januari mpaka Juni 2019), magari binafsi yamesababisha ajali 528, vifo 222 na majeruhi 453, kwa wastani; kila siku magari binafsi husababisha ajali tatu, kifo cha mtu mmoja mpaka wawili na majeruhi wawili.
Kwa miezi sita ya mwanzo ya mwaka huu pikipiki zimesababisha ajali 334, vifo 176, majeruhi 319, kwa wastani pikipiki zinahusika katika ajali mbili kila siku na kusababisha kifo cha mtu mmoja tu, na mmoja mpaka wawili.
Takwimu zingine zinaonesha mabasi ya abiria yakipata ajali 103, na kusababisha vifo 61 na majeruhi 195 katika kipindi hicho.
Pia ripoti hiyo inaonesha malori yalihusika katika ajali 167, na kusababisha vifo vya watu 130 na majeruhi 142, wakati daladala zilipata ajali 143, na kusababisha vifo 89 na majeruhi 268.
Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Deus Sokoni alisema wanachukua hatua mbalimbali kudhibiti ajali za magari binafsi ikiwemo kufungia leseni za madereva wanaosababisha ajali kwa uzembe, na kujihusisha na ulevi, mwendokasi na makosa mengineyo.
Alisema pia wanatarajia kufanyika kwa mabadiliko ya kisheria ambayo yatasaidia kudhibiti magari binafsi katika masuala mbalimbali ikiwemo mwendokasi, ulevi pamoja na ufungaji wa mikanda.
Utafiti wa WHO unasema kufunga mkanda wa usalama humsaidia abiria wa mbele kujikinga na madhara ya ajali kwa asilimia 40 mpaka 50, na asilimia 50-75 kwa abiria waliokaa viti vya nyuma.
Ripoti ya Usalama Barabarani ya Shirika la Afya Dunia (WHO) iliyotolewa mwaka 2018, inabainisha kuwa Sheria za Tanzania zina upungufu katika kudhibiti usalama barabarani ikiwamo kuruhusu kiwango kikubwa cha ulevi kwa madereva bila kujali uzoefu wa dereva katika kazi husika.
Kwa mujibu wa taarifa za Polisi nchini, zaidi ya ajali 2,250 zimerekodiwa kuwa zilitokana na ulevi kati ya mwaka 2006 mpaka 2017 huku magari binafsi yakitajwa kuhusika zaidi kwenye ajali hizo.
Chanzo: Habarileo