Noti mpya tz
JF-Expert Member
- Mar 23, 2011
- 974
- 244
Jamani Baada ya ajali ya Meli iliyoua ndugu zetu, jamaa zetu na marafiki zetu zanzibar nimekuwa nikifikiria sana kuhusu ajali, moja ya fikra zilizonijia ni kuhusu maisha ya watanzania kupotea ktk ajali za barabara na majini, miaka michache iliyopita Meli ya MV NYAMAGENI iliua watu mwanza na mmiliki wake alijaribu kufuatiliwa kwa sababu alikuwa ameshaambia aifanyie matengenezo na hakufanya hivyo mpaka inakuja kuua watu, sijui iliishaje maana sisi tz hatuna utamaduni wa kuwashitaki wenye pesa. Ajali za barabarani hata usiseme anajua Mungu tu.. Nimekuwa nikijiuliza pia, hivi hawa watu wanaopata ajali, kufa au kupata vilema vya maisha wamekuwa wakilipwa fidia kiasi gani??