Ajali za kihistoria na mustakabali wa Taifa

MBATATA

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
542
209
Tanzania (kwa maana Chama Tawala) haina utamaduni wa kuwandaa viongozi hasa kwa kiti cha Urais. Watu wakiwa wanashika nafasi mbalimbali - hasa uwaziri hujifunza humo humo majukumu ya kiuongozi, lakini pasipo kuwa na uhakika kesho watakuwa wapi

1985: Wakati watu wengi wakikuna vichwa na kuchambua kwa kila lugha nani atamrithi Baba wa Taifa Julius Nyerere, busara zilimfunua Mwalimu na wengine, wakatambua na kukubali kwamba Tanzania hii ni ya muungano wa nchi mbili na kwa hivyo, je, haukuwa wakati muafaka wa kuwapa hao wa upande wa pili nafasi ya kuongoza nchi pia? Zipo hadithi nyingi kuhusu alivyopatikana Mzee Ali Mwinyi, lakini ukweli ni kwamba hakuna aliyetegemea toka awali yatakuwa hivyo – Ajali ya Kwanza

1995: Nani aliyetegemea Uncle Ben angechukua Urais? Mkutano wa Wana CCM wenyewe ulimpa nafasi ya 3! Kwa busara tena (au safari hii Mzee aliingiza kaujanja ujanja?), Baba wa Taifa akajenga hoja iliyopelekea Uamuzi wa kumpa Uncle Ben Urais kupitia CCM….Ajali ya Pili!

2005: Mikakati ilikuwa mizito lakini tofauti na chaguzi zilizotangulia. Wapo watu waliojipanga kuuchukua Urais kwa kuwa walijiaminisha kuwa wanastahili ama wanaweza kwa kuwa walisoma mazingira, na kutambua kuwa kama fedha ipo basi inatosheleza kuupata huo Urais. WaTanzania (Wana CCM) wakaaminishwa kuwa fulani ndiye anafaa. Na pesa iliyotumika hapo ilikuwa balaa! Utaratibu wa Chama ni kwamba kipenga kikipulizwa ndio ruksa kuanza kampeni. Lakini watu wakajiamulia, miezi kabla ya ruksa ya Chama, kujitangaza tena kwa uzinduzi wa aina yake na shamra zikaanza …….aisee tulizinywa! Kumbe …….Hoja yake Braza JK ilikuwa nini? Nguvu Mpya, Ari Mpya, Kasi Mpya? Uduni wa utambuzi wa Watanzania……..Ajali ya Tatu!

2015: Funga kazi. Waliotangaza Nia kupitia Chama Tawala – 40! Wenye pesa zao, Wenye Vyeo vyao, Wenye Hasira zao, Wenye Tamaa zao, Wenye Uchungu na Nchi yao, Wenye Woga wao, Wenye Kutafuta Sifa tu (mifano yote mnaijua), wakachukua fomu na kupita huko na huko, wengine wakizimwaga pesa kwa kwenda mbele, lakini Mchezo ulipoisha……Hee! JPM? Kwanza hapo awali hata majina yake tu yalikuwa yanafana na utani utani! Watu hoi! Wengine (tena viongozi wa juu) wakakikosoa Chama chao hadharani, wengine wakakihama na Chama kwenda kuutafuta huo Urais kupitia kwingine…..Ajali ya Nne!

Fanya tafakari: Leo hii sauti za kusema huu ni muungano, vipi “zamu yao” ama “zamu yetu’ zimefia wapi?

Awamu ya 2 kwa ugeni wake wa mambo tukaingizwa kichwa kichwa kwenye huria na kuishia kwenye holela.

Awamu ya 3 tukaimbishwa Ukweli na Uwazi ndipo ubinafsishaji, ugenishaji ukashika kasi, leo tunawataka waturudishie viwanda vyetu.

Awamu ya 4 doh – Acha tu….Tunayaona mengi leo!

Cha kushukuru Mungu, Heri ajali hii ya Awamu ya 5 yenye kuonyesha matumaini, kuliko Ajali ambayo ingetupata ya kuongozwa na aliyegombea kupitia upinzani Mkuu – Bwana EL
 
Mmmh!. Tafakari yako nzito kaka, ila huoni kwamba pamoja na hizo unazoziita AJALI, kila awamu na mazuri yake pia yapo?
 
Mmmh!. Tafakari yako nzito kaka, ila huoni kwamba pamoja na hizo unazoziita AJALI, kila awamu na mazuri yake pia yapo?
Yapo ingawa hatukujengewa matumaini makubwa katika awamu hizo - la msingi...tujifunze tokana na ajali hizo, utaratibu wa kubambikiwa viongozi pasipo kuwa na mwelekeo ni hatari! Leo tuna Magufuli kesho sijui...?
 
Back
Top Bottom