Ajali Yauwa Tanga

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Habari nilizozipata sasa hivi zinasema kuna ajili imetokea eneo la kitumbi wilaya ya handeni mkoani tanga , jana jioni na watu 7 wamefariki dunia hapo hapo huku wengine wakaendelea kufariki walipokuwa wanapelekwa hospitali na hospitali kwenyewe , wenyeji wahuko wanasema idadi inaweza kuongezeka zaidi kutokana na kutokupata huduma ya kwanza na huduma zingine za afya ambazo ziko mbali na eneo husika pia watu wa huduma ya kwanza hawajaweza kufika , ajali hiyo imehusisha magari mengine zaidi ya 3

Mpaka sasa hivi magari bado hajatolewa barabarani kwahiyo ni tishio kwa usalama wa wasafiri wengine katika barabara hiyo mtu mwenywe namba 0786 03 4444
 
Habari nilizozipata sasa hivi zinasema kuna ajili imetokea eneo la kitumbi wilaya ya handeni mkoani tanga , jana jioni na watu 7 wamefariki dunia hapo hapo huku wengine wakaendelea kufariki walipokuwa wanapelekwa hospitali na hospitali kwenyewe , wenyeji wahuko wanasema idadi inaweza kuongezeka zaidi kutokana na kutokupata huduma ya kwanza na huduma zingine za afya ambazo ziko mbali na eneo husika pia watu wa huduma ya kwanza hawajaweza kufika , ajali hiyo imehusisha magari mengine zaidi ya 3

Mpaka sasa hivi magari bado hajatolewa barabarani kwahiyo ni tishio kwa usalama wa wasafiri wengine katika barabara hiyo mtu mwenywe namba 0786 03 4444



Jamani hizi ajali zitaendelea kutumaliza Watanzania hadi lini?
Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana Yesu libarikiwe. Amen.
 
Hivi ni nini chanzo cha ajali bongo???
May the souls of the dead rest in peace!
 
Mungu awaweke marehemu mahala pema peponi Amen!

Mbaya zaidi gari la Bi Harusi kugongana na gari iliyokuwa linasafirisha maiti!

Bibi harusi wapambe wafa ajalini wakielekea Tanga kufunga ndoa
Na Burhani Yakub,Tanga

WATU wanane akiwamo bibi harusi wamekufa papo hapo na wengine 12 kujeruhiwa vibaya baada ya magari manne kugongana.

Magari hayo yaligongana katika Kijiji cha Kitumbi wilayani Handeni kwenye Barabara ya Segera�Chalinze Ijumaa saa 1:30 usiku.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Nyakoro Sirro alisema ajali hiyo ilihusisha basi la Kampuni ya Meridian lililokuwa limebeba maiti likitokea jijini Dar es salaam kupeleka Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.

Watu walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa ajali hiyo ilitokea wakati basi la Meridian lililopokuwa likijaribu kulipita gari aina ya Toyota Hiace ambalo nalo ilikuwa ikitokea Dar es Salaam likiwa limewabeba bibi harusi na wasindikizaji waliokuwa wakielekea Tanga kwa ajili ya kufunga ndoa.

Walisema wakati Meridian ikilipita gari hilo mbele kulikuwa na lori la mizigo huku basi jingine la Kampuni ya Scandinavia lililokuwa likitokea Kampala kuelekea Dar e salaam likija kwa kasi.

Meridian iliivaa hiace kwa nyuma iliyokuwa imefunga breki baada ya kushindwa kulipita lori kwa kuwa mbele yake ilikuwa ikija Scandinavia kwa kasi,�alisema Hassan Samhando na kwamba magari mawili ambayo ni Scandinavia na lori yalipinduka.

Mwananchi
 
Basi la Meridian laua 8

Written by Bakhya Said, Tanga
Sunday, 13 April 2008
WATU nane tisa wamekufa katika ajali mbaya iliyohusisha basi la Meridian lililokuwa likisafirisha maiti kwenda Moshi ambalo lilivaana na Toyota Hiace lililokuwa limembeba bibi harusi mtarajiwa, Bi. Stephern Hiza (22) na wapambe wake.

Katika ajali hiyo watu 12 walijeruhiwa vibaya na watu watatu kati yao kukimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi. Majeruhi wengine wamelazwa katika hospitali ya Bombo mkoani hapa.

Dereva wa basi la Meridian alikimbia baada ya ajali hiyo kutokea na hajulikani alipo.
Watu walioshuhudia ajali hiyo waliliambia gazeti ili kuwa ilitokea juzi saa 1 usiku katika eneo la Kitumbi, Handeni.

Kondakta wa Meridian , Bw. Godfrey Joseph, alisema chanzo cha ajali hiyo ni basi la kampuni moja (jina tunalo) lililokuwa likitokea Uganda kuelekea jijini Dar es Salaam kutaka kulipita lake wakati mbele kuna gari nyingine aina ya Fuso.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Bw. Nyakolo Sillo, alisema ajali hiyo ilitokea juzi saa 1 usiku, wakati dereva wa Meridian alipogonga kwa nyuma gari aina Toyota Hiace.

Waliokufa katika ajali hiyo mbali na bibi harusi mtarajiwa ni ni Latipha Undole (1), Neema Cheddy (26), mkazi wa Kawe, Stephern Hiza (11) ambaye ni mdogo wake na marehemu bibi harusi mtarajiwa na mwanafunzi wa darasa la tano Zuberi Mohamed (35).

Wengine ni Joseph Matunda (23), mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ambaye ni mkazi wa Namanga, mwanamke aliyefahamika kwa jina la moja la Mama Maswapu mkazi wa Mbagala na mwingine aliyefahamika kwa jina moja la Mariam.

Maiti zimehifadhiwa chumba cha maiti Hospitali Teule ya Bombo, Tanga na majeruhi wamelazwa hospitalini hapo.

Kwa upande wake Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabara, Bw. James Kombe, ambaye alikuwepo katika eneo la tukio alisema wahusika waliosababisha ajali hiyo watafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake. Alisema Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema, ametuma salama za pole kwa wale wote waliopata msiba.
 
Back
Top Bottom