Ajali Yauwa Tanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajali Yauwa Tanga

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Apr 12, 2008.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Apr 12, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Habari nilizozipata sasa hivi zinasema kuna ajili imetokea eneo la kitumbi wilaya ya handeni mkoani tanga , jana jioni na watu 7 wamefariki dunia hapo hapo huku wengine wakaendelea kufariki walipokuwa wanapelekwa hospitali na hospitali kwenyewe , wenyeji wahuko wanasema idadi inaweza kuongezeka zaidi kutokana na kutokupata huduma ya kwanza na huduma zingine za afya ambazo ziko mbali na eneo husika pia watu wa huduma ya kwanza hawajaweza kufika , ajali hiyo imehusisha magari mengine zaidi ya 3

  Mpaka sasa hivi magari bado hajatolewa barabarani kwahiyo ni tishio kwa usalama wa wasafiri wengine katika barabara hiyo mtu mwenywe namba 0786 03 4444
   
 2. mbarikiwa

  mbarikiwa JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 507
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35


  Jamani hizi ajali zitaendelea kutumaliza Watanzania hadi lini?
  Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana Yesu libarikiwe. Amen.
   
 3. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 135
  "Ajali haina kinga" na "Kazi ya Mungu haina makosa"-
  Mhe. Rais J.Kikwete
   
 4. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2008
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hivi ni nini chanzo cha ajali bongo???
  May the souls of the dead rest in peace!
   
 5. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2008
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Mungu awaweke marehemu mahala pema peponi Amen!

  Mbaya zaidi gari la Bi Harusi kugongana na gari iliyokuwa linasafirisha maiti!

   
 6. Allah's Slave

  Allah's Slave JF-Expert Member

  #6
  Apr 13, 2008
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 564
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Basi la Meridian laua 8

  Written by Bakhya Said, Tanga
  Sunday, 13 April 2008
  WATU nane tisa wamekufa katika ajali mbaya iliyohusisha basi la Meridian lililokuwa likisafirisha maiti kwenda Moshi ambalo lilivaana na Toyota Hiace lililokuwa limembeba bibi harusi mtarajiwa, Bi. Stephern Hiza (22) na wapambe wake.

  Katika ajali hiyo watu 12 walijeruhiwa vibaya na watu watatu kati yao kukimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi. Majeruhi wengine wamelazwa katika hospitali ya Bombo mkoani hapa.

  Dereva wa basi la Meridian alikimbia baada ya ajali hiyo kutokea na hajulikani alipo.
  Watu walioshuhudia ajali hiyo waliliambia gazeti ili kuwa ilitokea juzi saa 1 usiku katika eneo la Kitumbi, Handeni.

  Kondakta wa Meridian , Bw. Godfrey Joseph, alisema chanzo cha ajali hiyo ni basi la kampuni moja (jina tunalo) lililokuwa likitokea Uganda kuelekea jijini Dar es Salaam kutaka kulipita lake wakati mbele kuna gari nyingine aina ya Fuso.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Bw. Nyakolo Sillo, alisema ajali hiyo ilitokea juzi saa 1 usiku, wakati dereva wa Meridian alipogonga kwa nyuma gari aina Toyota Hiace.

  Waliokufa katika ajali hiyo mbali na bibi harusi mtarajiwa ni ni Latipha Undole (1), Neema Cheddy (26), mkazi wa Kawe, Stephern Hiza (11) ambaye ni mdogo wake na marehemu bibi harusi mtarajiwa na mwanafunzi wa darasa la tano Zuberi Mohamed (35).

  Wengine ni Joseph Matunda (23), mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ambaye ni mkazi wa Namanga, mwanamke aliyefahamika kwa jina la moja la Mama Maswapu mkazi wa Mbagala na mwingine aliyefahamika kwa jina moja la Mariam.

  Maiti zimehifadhiwa chumba cha maiti Hospitali Teule ya Bombo, Tanga na majeruhi wamelazwa hospitalini hapo.

  Kwa upande wake Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabara, Bw. James Kombe, ambaye alikuwepo katika eneo la tukio alisema wahusika waliosababisha ajali hiyo watafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake. Alisema Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema, ametuma salama za pole kwa wale wote waliopata msiba.
   
Loading...