Kibo10
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 11,277
- 8,837
Watu wanne wamefariki dunia papo hapo na wengine 32 wamejeruhiwa ,baada ya basi la kampuni Polepole walilokuwa wakisafiria toka mkoani Arusha kuelekea mjini Babati mkoani Manyara kuligonga trekta, pikipiki ya magurudumu matatu na gari dogo aina ya Toyota katika eneo la Changarawe lililopo katika barabara kuu inayotoka mjini Babati kuelekea mkoani Arusha.