Ajali yaua ndugu watano wakitoka msibani Mbeya

Maisha yalivo mafupi,huwa nashangaa sana kuona watu wanagombania wanawake,viwanja,mashamba, etc.
Kitu kikubwa unachopaswa kugombania duniani ni afya njema na furaha baasi,ile ya moyoni unaamka unasalimia watu,unakula, unashiba baasi
Kabisa
 
Hii gari huenda iliruka bump kwa speed ikapaa usawa wa scania sababu haieleweki Raum inaichakazaje Scania namna hii!?
Nilisikia Kamanda wa Mkoa wa Mbeya akielezea ajali hii kwamba Toyota Raum imegongwa, ktk maelezo yake ajali ilihusisha magari matatu gari moja lenye mchanga au kokoto lilikuwa limeharibika limesimama, gari lingine la mizigo lilikuwa linatoka Dar kwenda Mby ndo liliyagonga hayo magari mengine ikiwemo hiyo Raum. Siyo kwamba Raum ndo iligonga hilo lingine
 
Kuna haja tuachane na mambo mengi yasiyokua na maana..Mbeya Lango kuu la nchi za kusini mwa afrika na Hata Congo pia...Hivyo malori ni mengi sana eneo hilo.

Barabara za Mbeya Ni finyu na zimechoka sana unapokua unaingia Mjini na hata unapotoka kuelekea Songwe.

Kuna Haja Wabunge wa Mkoa huu mjiulize kwann msibebe agenda ya hii barabara kupanuliwa iwe njia 4 au 6 isaidie Kupunguza vifo...
 
Unaweza kukuta kabisa ajali imesababishwa na ubovu wa barabara. Lakini waafrika tulivyo kama manyani wala huwezi kuona kiongozi yoyote anajali na kusema turekebishe hiyo sehemu kabla watu wengi zaidi hawajapata madhara.
Sawa kabisa , watu wanaangalia cha karibu kulaumu
Mlandizi to chalinze ni kipande hatari sana cha barabara , ajali kila siku ila wanalaumiwa madereva na mwendokasi,, kutoka uyole hadi igawa barabara ni mbaya sana ila hutasikia hilo likiongelewa na wadau hasa askari wa barabarani,
 
Ajali za aina hii watoto huwa wanapona, sijui kuna siri gani hapo? au ni udogo wa miili yao ndio kinga yao? au ni utukufu wa Mungu na andiko waache wadogo waje kwangu, kwamba anawalinda kwasababu ni kama malaika?

Marehemu wapumzike kwa amani.
Mwili wa mtoto bado laini unauwezo wa kuabsorb forces bila kupata damage kubwa. Mfano akianguka mtoto analia atainuka na kuendelea kucheza baada ya muda wakati ukianguka mtu mzima unaweza ishia kulazwa. Samahani kwa kiswanglish.
 
Kuna haja tuachane na mambo mengi yasiyoua na maana..Mbeya Lango kuu la nchi za kusini mwa afrika na Hata Congo pia...Hivyo malori ni mengi sana eneo hilo.

Barabara za Mbeya Ni finyu na zimechoka sana unapokua unaingia Mjini na hata unapotoka kuelekea Songwe.

Kuna Haja Wabunge wa Mkoa huu mjiulize kwann msibebe ajenga ya hii barabara kupanuliwa iwe njia 4 au 6 isaidie Kupunguza vifo...
Tatizo letu kubwa hatuna mipango ya muda mrefu, ilitakiwa iwepo plan ya miundo mbinu ya muda mrefu hapa hadi afe mkubwa (siombei wala sitamani) ndo bara bara itafumuliwa na kutengenezwa ndani ya muda mfupi.
 
Punguza ujuaji basi duuh umekazana majina ya Moshi majina ya Moshi kwa taarifa yako sasa, huku mkoa wa Songwe wilaya ya Ileje kuna eneo linaitwa kwa Mboya wala hawana uhusiano wowote na KLM achilia mbali hiyo kulowea uliyong'ang'ania.
Badae utasema hata yule Tom Mboya wa Kenya nae ni mchaga.
UMEMALIZA ndugu. Mie nimewaambia kuna Wasafwa akina MBOYA, wamenishambulia sana, utadhani kuna mtu mwenye COPYRIGHT na majina. Upumbav.u mtupu.
 
UMEMALIZA ndugu. Mie nimewaambia kuna Wasafwa akina MBOYA, wamenishambulia sana, utadhani kuna mtu mwenye COPYRIGHT na majina. Upumbav.u mtupu.
Mapumbavu sana hayo majitu yanapenda sana kulazimisha ukabila.
Kitu wasichokielewa majina ya kibantu hufanana mno.
 
Kuna haja tuachane na mambo mengi yasiyokua na maana..Mbeya Lango kuu la nchi za kusini mwa afrika na Hata Congo pia...Hivyo malori ni mengi sana eneo hilo.

Barabara za Mbeya Ni finyu na zimechoka sana unapokua unaingia Mjini na hata unapotoka kuelekea Songwe.

Kuna Haja Wabunge wa Mkoa huu mjiulize kwann msibebe agenda ya hii barabara kupanuliwa iwe njia 4 au 6 isaidie Kupunguza vifo...
Pointi ya msingi sana hii. Barabara za mkoa wa Mbeya zina plan ya zamani ya miaka ya 1990, wakati kuna ongezeko kubwa la watu na shughuli za kiuchumi. Hii inaathiri sana utoaji huduma, kwa sababu muda wa asubuhi na jioni mawasiliano kati ya Uyole na Mwanjelwa ni shida. Ni vema wabunge wa mikoa ya Mbeya na Songwe wakatambua umuhimu wa kuomba pesa ili kufanya upanuzi wa barabara kuanzia Tunduma hadi Makambako iwe angalau njia 6. Hii itasaidia kupunguza ajali na mikwamo kwenye foleni.
 
Maisha yalivyo mafupi, huwa nashangaa sana kuona watu wanagombania wanawake, viwanja, mashamba, etc.

Kitu kikubwa unachopaswa kugombania duniani ni afya njema na furaha baasi, ile ya moyoni unaamka unasalimia watu, unakula, unashiba baasi
RIP
 
Ajali mbaya ya gari leo asubuhi maeneo ya Itewe-Inyala Mbeya imegharimu maisha ya ndugu zetu watano wa familia moja walio kuwa wakitokea msibani Mbeya kurudi Dar es salaam. Waliofariki ni

Thomas Mboya,
Isabella Mboya,
Joyce Mboya,
Magreth Masaka,
Sevelina Mgalla

Ajali hii ilihusisha gari ndogo aina ya Toyota Raum pamoja na Lori kugongana uso kwa uso. Majeruhi ni mtoto wa jina lake ni Erick Mboya.

Walitoka kumzika shangazi yao.
Bwana alitoa na Bwana ametoa Jina lake lihimidiwe

I know this family we lived neighbors for years

View attachment 1947533View attachment 1947534View attachment 1947535View attachment 1947537
Tatizo wengi wetu akiendesha gari mitaa ya Dar Es Salaam basi anaona ana uwezo wa kuendesha kwenye barabara kuu zenye malori na magari mengi,poleni wafiwa.
 
Tatizo wengi wetu akiendesha gari mitaa ya Dar Es Salaam basi anaona ana uwezo wa kuendesha kwenye barabara kuu zenye malori na magari mengi,poleni wafiwa.
Dereva wa gari ndogo alikua dereva wa JWTZ huenda alileta ubabe njiani
 
Back
Top Bottom