figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Hii imetokea Maweni nje kidogo na mji wa Manyoni Mkoani Singida. Kuna ajali mbaya sana imetokea maeneo ya Maweni kati ya Dodoma na Manyoni . Basi moja lilikuwa linatokea Dar kwenda Mwanza na lingine lilikuwa litatokea Shinyanga kuja Dar
Ni ajali ya mabasi ya kampuni moja ya "City boy" yaliogongana, inasemekana yamegongana uso kwa uso na kusababisha vifo kadhaa Ila hatujui hasa idadi bila shaka jeshi la polisi ndio wenye mamlaka kusema madhara na idadi ya majeruhi na vifo na tupo. Barabara imefungwa kwa muda.
Mbaya zaidi kabla ya hii ajali, Polisi walikuwa washampiga faini na Onyo kali mmoja wa madereva hao kwa kosa la kukimbiza gari. Hata hivyo hakuweza kuzingatia maelekezo matokeo yake ndo ikatokea ajali mbele.
Pole sana wahanga wa ajali hii.
========
Updates;
========
Kamanda wa polisi mkoa singida Thobias Sedoyoka amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba ajali hiyo inahusisha basi lenye usajili wa no T 531 BCE likitokea dar kwenda kahama na basi T 247 linalotoka kahama kwenda Dar yote ya kampuni moja CITY BOYS, yamegongana uso kwa uso na kuawa abiri 24 papo hapo na kujeruhi wengi idadi zaidi ya vifo itaendelea kutolewa.....
Kamamnda Mpinga akizungumzia ajali ya Singida

Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali na abiria aliyekuwepo moja ya magari yaliyo pata ajali leo huko Singida na kuua watu 30 amesema kuwa madereva wote wawili walikuwa wanachezesha magari yao kwa mzaha barabarani eti ni ishara ya salamu.
Amesema waliwashiana taa halafu wote wawili wakaanza kuhama ktk upande wao na kurudi huku wakiyachezesha magari yao kwa muda mpaka walipo gongana.
Shuhuda anadai alipo wauliza wenzie kwa nini wanayayumbisha magari hivi, abiria wenzie wakamwambia madereva wanasalimiana.
Hivi kwa nini watu wanavituko vya hatari hivi? Chanzo ITV habari SAA 8.00 usiku.