Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,731
- 40,836
TAARIFA KWA UMMA
__________
YAH. AJALI YA GARI ILIYOTOKEA LEO 18.7.2008 ASUBUHI
ENEO LA GAIRO
Kutokana na ajali mbaya ambayo imetokea leo Ijumaa 18.7.2008 majira ya asubuhi eneo la Gairo Mkoani Morogoro na kusababisha vifo vya watu wawili ambao ni mtoto wa Mheshimiwa Mbunge Saverina Mwijage ambaye anaitwa Stella Silvanus mwenye umri wa miaka 18 pamoja na dereva wa gari hilo ambaye ni Ndugu Anderson Kaindoa mwenye umri wa miaka 40.
Pamoja na waliopata ajali pia wapo watoto wengine wa Mheshimiwa Mbunge ambao ni Gervas Silvanus, Silli Silvanus na Irene Silvanus mwenye miaka 3, pamoja na Imelda Mussa ambaye ni mtoto wa Mheshimiwa Mercy Emmanuel Mbunge.
Wote hawa walikuwa wanatokea mjini Dodoma kuelekea
Dar es salaam baada ya likizo ya shule kumalizika tayari kwa ajili ya kuendelea na masomo yao.
Kwa simanzi kubwa Kambi ya Upinzani inapenda kutoa pole kwa Mheshimiwa Saverina Mwijage kwa kupotelewa na mwanaye kipenzi pamoja na ndugu na jamaa wa dereva aliyepoteza maisha yake.
Tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa wale wote waliohusika katika juhudi za kuokoa maisha ya vijana hawa, na shukrani za kipekee zimwendee Mheshimiwa Mohamed Shabiby Mbunge wa Gairo ambaye alikuwa wa kwanza pamoja na wananchi wake kufika eneo la tukio na kuhakikisha kuwa marehemu, majeruhi na mali zao zote ziko salama pamoja na kuwafikisha wahusika Hospitali.
Pia tunapenda kuwashukuru sana waheshimiwa wabunge wafuatao kwa kuweza kufika eneo la tukio kwa niaba ya Bunge kwa ajili ya kwenda kusaidia kuokoa maisha ya watoto wetu nao ni waheshimiwa Abbas Jecha (Mb), Mkiwa Adam Kimwanga (Mb), Martha Mlata (Mb) na Felister Bura (Mb). Hiyo ndio timu iliowakilisha Bunge katika kuwafikisha marehemu na majeruhi hapa Dodoma.
Pia tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa madaktari wakiongozwa na Daktari mkuu wa Hospitali ya Gairo Dr. Mkoba, Dr. Abdalla wa Kituo cha Afya Berege pamoja na Nesi wa Hospitali kuu ya Dodoma Mery Shadrack kwa juhudi zao za kuokoa maisha ya vijana hawa. Afande Revocatus ambaye ni Trafiki kwa huduma nzuri ya kiusalama.
Mwisho lakini kwa umuhimu mkubwa tunapenda kumshukuru Mama Kippa, Mkurugenzi Msaidizi Huduma kwa Wabunge, kwa kazi kubwa aliyofanya baada ya kupata taarifa za tukio hili la kusikitisha.
Imetolewa na:
Hamad Rashid Mohamed (Mb)
KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI
18.7.2008

Last edited by a moderator: