Ajali ya Treni ya TRL yatokea Morogoro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajali ya Treni ya TRL yatokea Morogoro

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by GM7, Aug 8, 2009.

 1. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kwa mujibu wa TBC taifa treni ya abiria iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma imeanguka usiku wa kuamkia leo nje kidogo ya mji wa Morogoro ambapo imejeruhi watu kadhaa. Mmoja wa wafanyakazi wa TRL amesema treni hiyo ilipita Morogoro saa 6:15 usiku. Imeelezwa kuwa takribani mabehewa 6 yameanguka na chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika.

  Taarifa kamili ya ajali hiyo itaendelea kutolewa ktk taarifa za habari zijazo.
   
 2. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2009
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,218
  Trophy Points: 280
  Du kazi kweli kweli
   
 3. Baridijr

  Baridijr Member

  #3
  Aug 8, 2009
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  poleni ndugu zetu, ila na nyie wahindi kama mmeshindwa si muondoke kwani hela mlizochukua si zinatosha
   
 4. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #4
  Aug 8, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mimi nadhani sasa tunahitaji kusimama na kusema imetosha! Tunahitaji mashirika yetu yarudishwe.
   
 5. b

  bnhai JF-Expert Member

  #5
  Aug 8, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Wasiwasi wangu isije ikawa ni hujuma. Maana Watanzania tunamatatizo makubwa. Km mtakumbuka ajali iliyopita inasadikiwa kusababishwa na watu waliokuwa wanataka kuiba mafuta. Sasa km ni hujuma kwakweli ni lazima kukomesha hali hii.
  Pia nadhani upande mwingine wa TRL watu hawaambiwi ukweli. Hawa TRL ni wabia wa serikali, wao wakiwa na majority shareholders (51%) kwa hiyo serikali ni minority. Wakati wanaingia mkataba na serikali kila mtu alitakiwa achangie kiasi fulani cha pesa ili treni iweze kufanya kazi zake vizuri. Maajabu ni kwamba jamaa wamejitahii kufanya part yao ikiwa ni pamoja na kukopa. Sasa ikija upande wa Serikali wao wanasahau kama wana own share pale na wanatoa pesa kidogo wakati shirika linahitaji significant capital.
  Kwa msingi huo tatizo si Wahindi bali ni Serikali kutotimiza upande. Kwa ule mkataba, serikali ikijifanya inauvunja pesa zetu nyingi zitatokomea. Nadhani kwa kuanzia waweke wazi mchawi ni nani na siasa ziweke kando tunahitaji professionalism.
   
 6. Mopao Josee

  Mopao Josee JF-Expert Member

  #6
  Aug 8, 2009
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  rais anaona ajali za mabasi haoni ya TRL.
  TANZANIA TUNAHITAJI VIONGOZI STAILI YA MNALI (FORMER DC `KATERERO`)
   
 7. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #7
  Aug 8, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  we share same theory
   
 8. Komamanga

  Komamanga JF-Expert Member

  #8
  Aug 8, 2009
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 221
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kazi kweli kweli, unategemea nini sasa kama humlipi vizuri mpishi anayekupikia kila siku, lazima utegemee kuumwa tumbo tuuuuu.Pole kwa wote waliopata ajali.
   
 9. b

  bnhai JF-Expert Member

  #9
  Aug 8, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Hujuma si njia njema ya kutafuta muafaka. Ni kiashirio cha ubinafsi wa hali ya juu. Zingatia shirika limeajiri watu wangapi na hao watu wanategemewa na watu wangapi. Likiendelea kuhujumiwa na likafilisika utamhujumu nani? Maana hata kazi utakuwa huna. Upande mwingine, ni watu wangapi wanategemea usafiri wa shirika lile?? Ukiondoka hapo nini mchango wake kwa uchumi. Kumbuka mizigo na abiria wengi wa ndani na nje ya nchi wanategemea shirika lile.
  Ni lazima tuwe wazi TRL tatizo ni capital licha ya kuwa kuna maswala ya kiutendaji kiasi fulani. Hao Watanzania tuliowaamini miaka yoote wamefanya madudu ya kutosha. Watu wamesafiri bure kama ATCL, hakuna nidhamu, yaani mambo ovyo ovyo.
  Kubwa ni kuboost capital kwenye shirika kuwa na plan hiyo, then wafloat share kwenye market tuone nini kitafuata.
   
 10. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #10
  Aug 8, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,064
  Trophy Points: 280
  Uliyosema ni kuntu kabisa.
  Tuwe wachambuzi kabla kuanza kulaumu wahindi. Reli hii imekuwa ikihujumiwa na wanareli wenyewe kidogokidogo hadi ikafikia mahala serikali kutafuta mbia. Kwa mtindo huu hata mbia akitoka kwa Obama hatoweza maana sisi hadi sasa hatujatambua wala kukubali kuwa tatizo ni sisi. Serikali inatupa majukumu lakini tunaishia hivyo tuu na ndiyo maana mashirika karibu yote ya umma leo hayapo tena.
  Wengine wanasema wahindi waondolewe turejeshewe wenyewe mimi muota njozi natabiri kuwa tutauza hata mataruma kama skrepu.
   
 11. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #11
  Aug 8, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Poleni waliopatwa na ajali.

  Wafanyakazi wa TRL walikuwa kwenye mgomo isijekuwa wengine waling'oa mataruma kwa hasira na kusahau kuyarudishia mgomo ulipoisha.
   
Loading...