Ajali ya Trafiki wa Ikulu na mwendo kasi! Sheria inasemaje

bhikola

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,130
1,660
Habarini za J3 wapendwa wote wa JF
Kwa bahati mbaya sana ajali za barabarani zimeendelea kuchukua maisha ya watanzania wenzetu. Inapotokea kwa usafiri wa wote (public trans) imekuwa ni kawaida kusikia kuwa sababu ni mwendo kasi, na ikiwa kwa wadogo au ndugu zetu wa pikipiki (maarufu kama bodaboda) wanasema ni wazembe, na hawafuati sheria za balabalani.
Wiki imeyopita tumesikia ajali mbili zintokea kwa watu wa ikulu, RIP kwa dreva wa ikulu na pole zako bwana afande. Kwa mshangao binafsi sijasikia chanzo cha ajali ya marehemu ni nini, na hiki cha mhe afande tunaambiwa ni tuta, na utelezi katika eneo hilo la kimara.
Sasa kwa kawaida tungetegemea kitengo cha usalama barabarani wangekuja na uchunguzi makini na siyo kuwa wanawahi kutoa sababu za kitoto na zisizo na mashiko kama hizo, kwasababu, siku zote mvua dar zinanyesha na pia hilo tuta halikuwekwa jana wakati raisi anapita, kwa hiyo kwa vyovyote vile hizo haziwezi kuwa sababu za ajali ya mhe afande.
Kama ingekuwa hapa uholanzi (nilipo kwa sasa) kwanza wangemchunguza huyo trafiki mwenyewe (inawezekana alikuwa amlewa, au alikuwa na tatizo la kifamilia, kikazi, binafsi, kijamii na mengine kama hayo, au hakupenda kuendesha kwenye mvua hivyo alilazimishwa kwahiyo alikuwa na stress au frastration; pili wangechunguza chombo kilichotumika, inawezekana ni technical issues za pikipiki, maana siajabu hazifanyiwi matengenezo vizuri (wote tunajua mambo ya kibongo, na hatujasahau gari za ikulu zilivyotumia mafuta yaliyochakachuliwa, pia gari la raisi lilivyochomoka tairi katika msafara), au pia tairi zake si kwaajili ya barabara iliyolowa (tunajua mambo ya bidhaa fake ilivyo bongo). SASA KWA BONGO IMEKAAJE WAPENDWA??

Great thinkers! mi sielewi hiyo conclusion waliyofikia kirahisi hivyo imekaaje kaaje. Wanasheria watujuze pia, maana ingekuwa ni raia wa kawaida tungesikia anaandaliwa mashtaka kama siyo faili kupelekwa kwa DPP.
Nawasilisha
 
Kuna speed maalum kwa Rais au waziri mkuu, wakiwa barabarani na iwapo uzembe au bahaati mbaya ikitokea yaweza kusababisha maahafa au kifo kama vile cha Sokoine.so akuna kosa lolote.Alilolifanya huyu trafic.
 
Aliyekuwa dereva wa Ikulu chanzo cha kifo chake yasemekana ni ajali ilosababishwa na unywaji Pombe ambayo ilimfanya ashindwe kuimudu driving yake na kuingia uvunguni mwa Lory ambalo lilikua limeharibika barabarani
 
Asante sana kwa ufafanuzi huo chipukizi
lakini je alikuwa kwenye speed hiyo inayotakiwa? kumbuka everything must have a cause
 
Aliyekuwa dereva wa Ikulu chanzo cha kifo chake yasemekana ni ajali ilosababishwa na unywaji Pombe ambayo ilimfanya ashindwe kuimudu driving yake na kuingia uvunguni mwa Lory ambalo lilikua limeharibika barabarani

Unaona sasa!!!!!!!!!!! balaaa
 
Hyo ajali alipata akiwa kwenye msafara wa rais au alikua anaendesha pikipiki yake?
 
kila kazi ina risks zake ikiwemo hiyo ya udereva wa pikipiki kwa kasi kama kina Valentino Rossi....kumbukeni siku zote bodi ya pikipiki ni mwili wa mwendeshaji, bila shaka hawa watu watakua wanakatiwa bima za ajali ili familia zao zisipate shida wakati wa maafa kama kifo.
 
Back
Top Bottom