Ajali ya Nungwi ni fundisho au muendelezo wa porojo za wanasisa wetu?

chama

JF-Expert Member
Aug 6, 2010
8,001
2,418
Watanzania bado tupo kwenye majonzi ya ajali iliyoikuta MV. Spice Islander. Hakuna ukweli usiokificho ajali hii ingeweza kuepukwa kama watu walio kwenye mamlaka husika wangetekeleza majukumu ya kikamilifu, uzembe na tamaa ndio sababu kubwa ya ajali hii. Kinachosikitisha ni serikali na wanasiasa wetu wanapoigeuza ajali hii kisiasa zaidi. Serikali imetoa mil.300 watanzania tunapaswa kujiuliza serikali imetoa pesa kwa kuwajali waathirika au ni moja ya porojo za wanasiasa wetu? Mil. 300 hazilingani na thamani ya maisha yaliyopotea hasa ukitilia maanani ajali hii haikusababishwa na natural disasters, wanasiasa wetu wamekimbilia kusema ajali imetokea kwa mapenzi ya mungu, je Mungu hakuwapa akili ya kutekeleza majukumu yao kikamilifu? Ni aibu wanamkimbilia Mungu kuficha ukweli wa mambo. Kitu kingine ni Mwanasiasa/mwanahabari Reginald Mengi siku ya ajali ITV haikupa uzito habari yenyewe, walikuwa wakiwaburudisha watamazaji kwa ndombolo , ajabu Mengi amekurupuka kutoa cheki ya mil.40 je ametoa pesa hizo kwa upendo au ni mbinu zake kuboresha public image? Ukichunguza tukio zima limetawaliwa na ulagahai wa hali ya juu wote ni kama Vodacom hawana tofauti. Serikali inapaswa kuwajali wananchi wake hii kujigeuza kama shirika la BIMA kila zinapotokea ajali zinazosababishwa na uzembe ni ulaghai wa hali ya juu.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Si ungechangia tu kwenye mada zilizo tangulia?!, mbona huna jipya hapa!, MOD muvuzisha hii makitu isitujazie seva yetu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom