Ajali ya MV Bukoba: Makosa yamerekebishwa?

daladala200x200.jpg
SIKU KAMA YA LEO MWAKA 1996, WATANZANIA TAKRIBANI 1000 walizama maji na kufa kutokana na ajari ya MV BUKOBA,
ilikuwa ni siku ya majonzi, mimi nakumbuka familia ya rafiki yangu kuzama majini karibu yote walipokuwa wakitoka msibani huko kagera, lilikuwa simanzi kubwa sana na bado litabaki kuwa simanzi kwa watanzania
toka kutokea ajari ya MV bukoba meli zetu na vyombo vingi vya usafiri bado vinakiuka sheria za usafirishaji (majini na barabarani) na watendaji wa serikali wenye dhamana na mambo ya usafiri ni wanufaika wakubwa wa rushwa zinazotoka na kuvunjwa sheria za usafiri
jiulize swali ni mara ngapi umeshuhudia dereva hakitoa rushwa kwa trafic kwa kuhatarisha maisha yako na wewe ukiwaangalia bila kusema neno?
je ni serikali tu ya kulaumiwa au na wananchi pia?
ni wangapi waliwahi kupanda basi na linapofika kwenye mizani wanaambia wasogee nyuma au mbele ya basi ili kupotosha mzani?
kwa hali iliyopo sasa sababu za kuzama MV bukoba zimepatiwa dawa?
kwa wasiojua ni kwamba MV Bukoba ilizama kwa kuzidisha mzigo kuliko uwezo wa meli na mpaka sasa sina hakika kama kuna mtu aliyechukuliwa hatua, yawezekana meli ilikuwa na matatizo mengine lakini la kuzidisha mzigo ilikuwa ni kichocheo kikubwa cha hii ajari
je kuna umuhimu hii siku kukumbukwa kwa matamasha na elimu kwa umma kuhusu sheria za usafirishaji na haki za msafiri?

wakuu naomba kuwakilisha
 
Hakijarekebishwa chochote.
Mambo yanapo haribika ni ulaji kwa wajanja.
Wanatamani hata MV Victoria nayo izame ili wafaidike.

mkuu umeongea kitu muhimu lakini mishindwa ku click wanafaidika vipi hapo?
vifo vya watu? au ni wao kujiingiza kwenye biashara hiyo ya usafirishaji?
lakini kama ndivyo ina maana maisha yetu bado yako hatarini hata wakifanya hizo biashara hao wajanja
 
je hii itasaidia kwa upande wa barabara au miradi wa wakubwa kama ilivyokuwa speed gavana

Wamiliki mabasi wapewa miezi mitatu kufunga kidhibiti mwendo
Saturday, 21 May 2011 09:47
Mwandishi Wetu, Morogoro
KAMANDA wa Kikosi cha Usalama barabarani, Mohamed Mpinga, ametoa miezi mitatu kwa wamiliki wa mabasi kufunga kifaa cha mfumo wa kuonyesha mwenendo magari.

Pia, ameagiza makamanda wa mikoa wa usalama barabarani nchini kutohuisha leseni za usafirishaji au kutoa mpya kwa magari ambayo hayajafunga kifaa hicho.

Mpinga alisema muda huo unaishia Agosti mwaka huu, umetolewa kutokana na wamiliki wengi kulalamika kwamba hawajapata elimu ya mfumo huo unavyofanya kazi na gharama zake.

Akizungumza kwenye maonyesho kwa kamanda wa usalama barabarani nchini na maofisa wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi kavu na Majini (Sumatra) juzi, Kamanda Mpinga alisema hata waliofunga licha ya kubainika kukiuka sheria za barabarani, hawajaanza kuwachukulia hatua.

"Hivi sasa hatujaanza kuchukua hatua hata kwa wale waliofunga, bali tunachofanya ni kuwapigia simu tunapobaini kwenye mfumo kuwa wanakwenda kasi, kwa sababu tulitarajia awamu ya kwanza kufunga mabasi 500, lakini hadi sasa ni 48 pekee yaliyofunga," alisema.

Kamanda Mpinga alisema kufungwa kwa kifaa hicho kunakofanywa na Kampuni ya Utrack Africa Ltd, kutapunguza kwa kiwango kikubwa ajali ambazo zimekuwa zikitokea.

Aliendelea kuwa kifaa hicho ambacho pia kina kamera kitasaidia polisi na wamiliki, kwa sababu anaweza kuona abiria waliopo kwenye basi lake muda wowote.

Pia, Mpinga alisema hivi sasa anafanya mawasiliana ili serikali isimamie mradi huo, badala ya Chama cha Wamiliki wa Mabasi yaendayo mikoani (Taboa), kwa sababu una manufaa zaidi.

Akitoa maelezo jinsi kifaa hicho kinavyofanya kazi, Mkurugenzi Mkuu wa Utrack Africa Ltd, Zulfikar Mohamed, alisema mifumo yao siyo tu kwa ajili ya kurekodi mwendo kasi kwenye mabasi, bali pia una faida nyingi kwa wamiliki.

Mohamed alisema mmiliki anaweza kufuatilia tabia za uendeshaji wa madereva wanapokuwa safarini, taarifa za safari, kamera za kupiga picha ili kujua idadi ya watu waliopo ndani ya basi na kwa maslahi yake kujua idadi ya abiria na usalama pale linapotokea tukio la uhalifu.

Pia, alisema mfumo huu unatumiwa na wenye malori ya mizigo na mafuta, kampuni za wawindaji, kampuni za utalii, mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO's) , kampuni za kutengeneza barabara, madini na kampuni binafsi zinazofanya biashara mbalimbali.


NILIPOKUWA UK hakuna upuuzi huu ila kila gari inafuata ratiba na hivyo kuzibiti mwenzo, wanakamela mabarabraba lakini sisi tukiweka ratiba ni njia bora zaidi,
ratiba ya gari ndio kipimo kizuri, kwa nini kila stand kubwa ya mabusi kusiwe na kituo cha trafic wanaoweza kuratibu ratiba ya mabasi kwa kutumia ratiba?
kama basi litafika mapema ya muda wanapigwa fine
mimi nadhani hii inaweza kuwa bora zaidi kama wao polisi watatumia mfumo ya pc kujua basi linaingia na kuondoka saa ngapi kwenye kila kituo kuliko haya maduu wanayoweka
 
kuna mkuu anajijulisha hapa kwamba kama taratibu za kitaalamu zingefuatwa kwenye kuokoa watu kama kutotoboa meli kwa kukurupuka kwa shinikizo la wana siasa kulikuwa na uwezekana wa kuokoa watu wengi zaidi
kwa maana nyingine mkuu anasema serikali kwa kupitia wakuu wake waliwabana sana waokoaji kufanya lolote linalowezekana bila risk assessment ya hatuo ya kutoboa meli
 
Moja ya sababu mimi kuikana ccm ni huu mchezo wao kufanya maisha ya watanzania kama pipi
wameuwa tarime wanataka kuwalipa wafiwa milion 3
sijui kama hawa wa mv bukoba walipata kitu
kama sheria kali hazita wekwa na kufuatwa tutakishwa
mpaka leo hakuna mabadiliko pamoja na hiyo meli kuzika maelfu ya watanzania

siku kama ya leo mwaka 1996, watanzania takribani 1000 walizama maji na kufa kutokana na ajari ya mv bukoba,
ilikuwa ni siku ya majonzi, mimi nakumbuka familia ya rafiki yangu kuzama majini karibu yote walipokuwa wakitoka msibani huko kagera, lilikuwa simanzi kubwa sana na bado litabaki kuwa simanzi kwa watanzania
toka kutokea ajari ya mv bukoba meli zetu na vyombo vingi vya usafiri bado vinakiuka sheria za usafirishaji (majini na barabarani) na watendaji wa serikali wenye dhamana na mambo ya usafiri ni wanufaika wakubwa wa rushwa zinazotoka na kuvunjwa sheria za usafiri
jiulize swali ni mara ngapi umeshuhudia dereva hakitoa rushwa kwa trafic kwa kuhatarisha maisha yako na wewe ukiwaangalia bila kusema neno?
Je ni serikali tu ya kulaumiwa au na wananchi pia?
Ni wangapi waliwahi kupanda basi na linapofika kwenye mizani wanaambia wasogee nyuma au mbele ya basi ili kupotosha mzani?
Kwa hali iliyopo sasa sababu za kuzama mv bukoba zimepatiwa dawa?
Kwa wasiojua ni kwamba mv bukoba ilizama kwa kuzidisha mzigo kuliko uwezo wa meli na mpaka sasa sina hakika kama kuna mtu aliyechukuliwa hatua, yawezekana meli ilikuwa na matatizo mengine lakini la kuzidisha mzigo ilikuwa ni kichocheo kikubwa cha hii ajari
je kuna umuhimu hii siku kukumbukwa kwa matamasha na elimu kwa umma kuhusu sheria za usafirishaji na haki za msafiri?

Wakuu naomba kuwakilisha
 
Tatizo la Tanzania Human is not a Resource. Human is just the way to justify their filthy, gready deals including aids from IDA. By saying we are more than 40 million of whom more than 50% are in poor state, they justify the way to get money from donors... Such a mess like power supply/generation can just be an history if we are serious and spend the dividend we get just from one gold mine. Our leaders/politicians they are not considering the wellness of their people they there just to suck their veins.

In just one tragedy like this we commemorate this day, was a lesson to what should be done to avoid such a loss of natinal power. But no one is ready to take any action as long as there is food on his/her table. There are so many things to relate... Tanzania is poor because it lacks leaders who are patriotic.

I wish one day we make them suffer.
 
Tatizo la Tanzania Human is not a Resource. Human is just the way to justify their filthy, gready deals including aids from IDA. By saying we are more than 40 million of whom more than 50% are in poor state, they justify the way to get money from donors... Such a mess like power supply/generation can just be an history if we are serious and spend the dividend we get just from one gold mine. Our leaders/politicians they are not considering the wellness of their people they there just to suck their veins.

In just one tragedy like this we commemorate this day, was a lesson to what should be done to avoid such a loss of natinal power. But no one is ready to take any action as long as there is food on his/her table. There are so many things to relate... Tanzania is poor because it lacks leaders who are patriotic.

I wish one day we make them suffer.


huo ndio ukweli wenyewe na kama tutaendelea kusubiria serikali iwe tayari tutendea haki watanzania basi kuna siku tutauzwa kabisa utumwani na hawa watawala wetu
 
yulijifunza nini hapa kwenye ili tukio

kabla na maada ya ajali, nchi bado haina team za kueleweka za uokoaji?
wanajeshi wetu ni wengi sana na hana kazi kwani wasifundishwi uokoaji kama mataifa mwingine?
Jeshi lazima liwe na kikosi cha kueleweka cha uokoaji wakati wa vita na wakati wa ajali hii ni pamoja na moto na matukio yote
yanayoweza kuteketeza maisha ya watu

wana jeshi wanapashwa kuwa na ramani za meli zote nchini ili waweze kufanya uokoaji kwa haraka pale inapobidi.
 
Ndugu zangu watanzania nasema hivi kwa sababu serikali ya tz imewekwa mifukoni mwa wafanyabiasha, sisi sote ni mashaidi kwa hili, nauli wanapanga wao, bei za nishati wao, chombo cha usafiri ni salama au kibovu wanaamua wao, serikali iko wapi? Tunashudia mabasi yana matairi ya vipara hakuna hatua inayochukuliwa, tumeshudia meli na boti katika bahari zikizima baharini na abiria kukaa majini zaidi ya masaa 5 hapa zanzibar aidha kwa kukosa mafuta au kwa ubovu lakini kesho yake meli/boti hiyo inasafiri tena, serikali iko wapi?. Inauma sana kilichotokea lakini ukweli ni kwamba kwa sasa tz haina serikali makini kwa raia wake ila kuna genge la wafanyabiashara ndiyo wanaotufanya tuishi haya maisha. POLENI SANA WOTE MLIOGUSWA NA MSIBA HUU MOJA KWA MOJA, na iko siku yao kwa wale wote anaosababisha haya yote . "TUNATAKA MABADILIKO KATIKA UTENDAJI WA SERIKALI LASIVYO TUTAANDAMANA NCHI NZIMA SIKU SI NYINGI"
 
"MV Bukoba was a passenger steamer that sank in Lake Victoria, 30 kilometers from Mwanza, Tanzania on May 21, 1996, killing nearly 1000 people. The boat transported passengers and cargo between Bukoba and Mwanza ports. The steamer's capacity was 430, but around 800 people drowned as the boat sank to the bottom of Lake Victoria. The manifest showed 443 passengers in the first and second class cabins, but the cheaper third class compartment had no manifest. Abu Ubaidah al-Banshiri, who was at the time second in command of the Al Qaeda organization, died in the accident. The lack of equipment and divers were partially to blame for the death toll. Rescue teams from South Africa were flown in to salvage the ship and retrieve bodies that sank 25 meters under water. President Benjamin Mkapa of Tanzania declared three days of national mourning after the tragedy.

MV Bukoba was a passenger steamer that sank in Lake Victoria, 30 kilometers from Mwanza, Tanzania on May 21, 1996, killing nearly 1000 people. The boat transported passengers and cargo between Bukoba and Mwanza ports. The steamer's capacity was 430"


Tuikumbuke siku hii jamani,naona magazeti yote ya leo hakuna linaloikumbuka.rest in peace all those who are in the coffin called MV.BK wreakage
It's now 17 years ago since the tragedy.
 
Ni siri nzito iliyojificha nyuma ya ajali hii! Lakini yote ni katika watu kuwa selfish kujiangalia wao tu na kuweka maslahi yao mbele zaidi ya maslahi ya binaadamu wenzao! Sie tunafanya kazi na mmoja ya waliokoka akihadithia utatokwa na machozi... Ni majonzi sana kukumbuka kwani tulipoteza ndugu na marafiki wengi kwa tamaa za wachache!
 
Ni kwaneema tu hata kuiona siku ya leo. Tuwaombee ndugu zetu waliotutangulia mbele za haki haswa wale wa mv. Bukoba mungu awarehemu na awapokee toharani
 
Tunapotimiza miaka 14 ya kuzama kwa meli ya MV Bukoba hapo 21/5/2010, Hivi kuna umuhimu wowote wa kuadhimisha kwa namna yoyote na kuikumbuka siku hiyo? Au ni kutiana machungu ya ndugu zetu waliofariki kifo kibaya katika meli hiyo ndani ya ziwa victoria.

Ebu tujiulize, maadhimisho haya yana maana yoyote?

mkuu sio 14 ni 17 years (since 21, May 1996)
 
Back
Top Bottom