Ajali ya MV Bukoba: Makosa yamerekebishwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajali ya MV Bukoba: Makosa yamerekebishwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kimeo, May 21, 2009.

 1. K

  Kimeo Member

  #1
  May 21, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 65
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  "MV Bukoba was a passenger steamer that sank in Lake Victoria, 30 kilometers from Mwanza, Tanzania on May 21, 1996, killing nearly 1000 people. The boat transported passengers and cargo between Bukoba and Mwanza ports. The steamer's capacity was 430, but around 800 people drowned as the boat sank to the bottom of Lake Victoria. The manifest showed 443 passengers in the first and second class cabins, but the cheaper third class compartment had no manifest. Abu Ubaidah al-Banshiri, who was at the time second in command of the Al Qaeda organization, died in the accident. The lack of equipment and divers were partially to blame for the death toll. Rescue teams from South Africa were flown in to salvage the ship and retrieve bodies that sank 25 meters under water. President Benjamin Mkapa of Tanzania declared three days of national mourning after the tragedy.

  MV Bukoba was a passenger steamer that sank in Lake Victoria, 30 kilometers from Mwanza, Tanzania on May 21, 1996, killing nearly 1000 people. The boat transported passengers and cargo between Bukoba and Mwanza ports. The steamer's capacity was 430"


  Tuikumbuke siku hii jamani,naona magazeti yote ya leo hakuna linaloikumbuka.rest in peace all those who are in the coffin called MV.BK wreakage
   
 2. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  RIP Kabula, Zaina na wengine wote.
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Asante kwa hii info Mkuu Kimeo.
  Huyu AlQaeda boss alikuwa anaishi TZ au??? just curious
   
 4. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Nakumbuka kuteketea wanafunzi waliokuwa wanarejea nyumbani baada ya kumaliza kidato cha nne/sita! Mungu awarehemu wote waliopoteza maisha katika ajali ya MV Bukoba.
   
 5. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #5
  May 21, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Inasikitisha sana na inauma sana wengi tuliwapoteza kutokana na tamaa za watu wachache hapo TRC.
   
 6. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #6
  May 21, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,661
  Likes Received: 21,879
  Trophy Points: 280
  Miaka 13 sasa tokea ajali hii mbaya itokee, jee Nchi yetu imejifunza lolote la ziada kuhusu jinsi ya kukabiliana na majanga? sasa hivi tunavyo vikosi vyetu imara vya uokoaji au bado tutasubiri toka SA? Au tumekalia "siasa" tuu?
  Maana angalia Busanda, Mawaziri wangapi wako huko? badala ya kuwaachia wakina Makamba wao wanaacha shughuli nyeti za kiserikali kwenda kupiga domo huko na Wizara zao zinadorola na hawajali.
  Kwa hali hiyo tutegemee majanga yakijitokeza wokovu ni mdogo.
   
 7. K

  Kimeo Member

  #7
  May 21, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 65
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Wanasiasa huwa wanataka kukumbuka vitu vinavyowapa credit,na sio vinavyo wa discredit.when you go through the story of Mv.BK tragedy everything is clear that mhusika mkuu ni serikali circumstantially.hope in future the matter will errupt as the ufisadis we can see right now.
  i believe kuna ufisadi ulitendeka pale
   
 8. R

  Rutakyamilwa JF-Expert Member

  #8
  May 21, 2009
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 1,869
  Likes Received: 1,161
  Trophy Points: 280
  Mungu azilaze roho za wapendwa wetu Peponi. AMEN
   
 9. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #9
  May 21, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkuu Kimeo, Mungu akuzidishie sana, unajua niliwahi kufanya training katika Engine Room ya hii meli, kabla sijahamia MV. Liemba na MV. Mwongozo inasikitisha sana, maana ninawakumbuka Crew wote waliokuwemo ambao nilishirikiana nao sana katika kujifunza ndani ya ile Meli,

  - Mungu awaweke pema wale wote waliopoteza maisha yao.

  FMEs!
   
 10. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #10
  May 21, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Marehemu wote wa Mv.Bukoba wapumzike kwa amani.
   
 11. T

  Tsidekenu Senior Member

  #11
  May 21, 2009
  Joined: May 7, 2009
  Messages: 141
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Jana usiku niliona kipindi kwenye star tv kikizungumzia kumbukumbu ya miaka 13 toka meli ya MV Bukoba izame kule victoria na kuuwa mamia ya watu.Mambo mengi yalizungumziwa na mwendesha kipindi hicho yaliki kuna mambo mawili ambayo yalinisikitisha na kunipa hasira ambayo sikuwa nayafahamu. Pengine kuna mliyokuwa mnayajua na mnayajua mengi lakini mimi sikuyajua labda kwa sababu by then nilikuwa bado mdogo.

  1. watengenezaji wa meli hiyo - Ubelgiji katika moja ya service waliyoifanyia meli hiyo kabla ya ajali walisema meli ina matatizo na wakarekomendi kiasi cha abiria na uzito ambao bado meli ingeweza kumudu kubeba pampja na matatizo yake.

  2. mafundi wa kutoka denmark walikuwa wanafanyia meli hiyo service pia wliliona tatizo na wakarecomend pia kiasi cha uzito na abiria wanaoweza kubebwa na meli hiyo.

  Ninachojiuliza ni umma ulipewa taarifa sahihi au kuelimishwa kuhusu findings hizi za mafundi tangu zilipotolewa ili kuwafanya watu wasing'ang'anie kupanda maana ni wazi maisha yao yalikuwa hatarini? Pengine wahusika walioruhusu watu walikataliwa kupanda meli bukoba na hivyo kukimbilia Kemondo bay kupanda walikwisha chukuliwa hatua za kisheria kwasababu najua serikali zetu zote ni mbovu lakini hapa ni obvious kulikuwa na uzembe mkubwa wa management kuanzia senior mpanka kwa mhusika wa mlangoni mwa meli(sijui anaitwa nani - ingekuwa basi ningesema kondakta).

  Ninajiuliza do we really learn? kwasababu natumaini katika bodi hii lazima kuna watu wamewahi kuingia jengo la PPF Towers hapa DSM. Lifti za jengo hili zinasikitisha sana na wakati mwingine huwa najiuliza tunasubiri mpaka catasprtophe itokee ndipo viongozi wa nchi waje na mataji ya maua mazuri mazuri ili kuonyesha kuwa tuna masikitiko? Ukikuta pale chini pako Nyomi na lifti ikija kila mtu anapotaka kupanda unaweza kujiuliza kama hapa kwenye confined space hivhi watu wanang'ang'ania na wanajua kuwa obvious possibility ya kukwama ni kubwa huko kwenye vyombo veytu vya usafiri haswa wa majini hali ikoje?

  Mitumbwi kila siku inazama na kuuwa watu -

  kwa nini sisi abiria tusiwe wakali? - utaniambia shida ya usafiri
  Kwa nini shida ya usafiri - tuliwaweka kusimamia haya mambo hawaperfom inanvyopaswa.

  hawa inabidi kuwatoa lakini suplliment kwenye kuwatoa hebu tuanza kugroom watoto wetu kwa kuinstill civivc education. Mtoto alkianzia kujua toka mdogo kwamba he/she need to be fair and perform our duties properly. Hii ni long term measure but at one pt in time it will pay off.

  Back to safety of marine vessels. - kwanini kusiwe na utaratibu wa kila wamiliki wa vyombo hivi vya majini kutoa taarifa publicly juu ya usalama wa vyombo vyao na recomendations za walivifanyia tathmini kama makampuni wanavyotoa taarifa za mahesabu yao ya fedha. - kwa mawazo yangu nahisi labda hii itasaidia kuongeza knoweledge kwa wananchi to take care of their own safety. na pili pia wenye hivi vyombo watakuwa more responsible.

  au mnaonanje wadau?
   
 12. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #12
  May 21, 2009
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,216
  Trophy Points: 280
  Nawakumbuka wanafunzi wa Rugambwa ndo kwanza walitoka kwenye graduation siku hiyo na wakachukua teksi handi kemondo bay kuwahi meli baada ya kuambiwa pale bukoba imejaa,MUNGU walaze mahali pema peponi wale wote waliofikwa na mauti kutokana na ajali hii
   
 13. senator

  senator JF-Expert Member

  #13
  May 21, 2009
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Miaka imekwenda Kweli toka wapendwa wetu watangulie mbele ya Haki...Daima tutawakumbuka.Hili ni moja kati ya matukio yaliyoleta simanzi kubwa kwa taifa letu (mwanzoni kabisa kwa kipindi cha Mkapa)

  Mwanga wa Milele uwaangazie na Raha ya milele uwape ebwana..wapumzike kwa AMANi..Amen
   
 14. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #14
  May 21, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Nilimpoteza rafiki yangu aliyekuwa anatoka kupeleka mahari yeye na mchumba wake wote walipumzika! RIP
   
 15. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #15
  May 21, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Asante kwa kutukumbusha juu ya hili, ni kweli nakumbuka wakati ule nikiwa pale DAR TECH siku hizi Institute jinsi taarifa hizi zilivyoleta simanzi ukizingatia tulikuwa na wenzetu waliyotokea kanda hiyo ya ziwa. Lakini huku tukiaendelea kuangalia makosa mbalimbali yanayosababishwa na watendaji katika sekta mbalimbali, ni vyema kuangalia upande mwaingine wa shilingi. Je na sisi tunaohudumiwa tunajifunza nini?. Tukikumbumba siku hii pale Bukoba meli ilikuwa imejaa na watu wakamua kuchukua hatua ya kwenda kupanda katika kituo kingine. Je leo hii tukiona basi limejaa, tunaacha kupanda au tunangoja litokee la kutokea na kuwatupiwa lawama watendaji. Wakati mwingine watendaji hulazimika kutenda makosa kutokana na pressure ya wahudumiwaji, pale tunapoambiwa hili haliwezekana na kuwataka watendaji wafanye jambo ili kufanikisha matakwa yetu.

  BWANA ALITOA na BWANA ALITWAA JINA LAKE LIBARIKIWE!!!
   
 16. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #16
  May 11, 2010
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Tunapotimiza miaka 14 ya kuzama kwa meli ya MV Bukoba hapo 21/5/2010, Hivi kuna umuhimu wowote wa kuadhimisha kwa namna yoyote na kuikumbuka siku hiyo? Au ni kutiana machungu ya ndugu zetu waliofariki kifo kibaya katika meli hiyo ndani ya ziwa victoria.

  Ebu tujiulize, maadhimisho haya yana maana yoyote?
   
 17. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #17
  May 11, 2010
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  [​IMG][​IMG][​IMG][​IMG]
  Hizi ni baadhi ya picha za ajari ya MV Bukoba,
  No 1 Meri ikiwa kichwa chini miguu juu, ndani kuna abiria wako hai
  ,, 2 Mnara wa kumbukumbu ya ajari kwa mbari
  ,, 3 Mnara wa kumbukumbu kwa karibu
  ,, 4 Meri ya mv Bukoba kabla ya kuzama (enzi za uhai wake)
   
 18. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #18
  May 11, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kaitaba please usinitoneshe kidonda ambacho kilishaanza kukauka.
  Nilipoteza watu wangu wa karibu sana katika ajali hiyo.
  Ni vizuri tukawa tunaadhimisha kila inapofikia tarehe hiyo kwa kuwaombea waliotutoka.
  Ni vizuri tukaadhimisha.
   
 19. M

  Mutabora Member

  #19
  May 12, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13

  Tarehe uliyoitaja inawezekana ndiyo tarehe aliyofika Ben Mkapa pale uwanja wa Nyamagana kusitisha zoezi la kuwatafuta ndugu zetu baada hata ya wataalamu kutoka South kuchemsha na kuondoka na siri moyoni kwa kile walichokishuhudia chini ya maji.

  Umenikumbusha mbali,,,,,kwani ile ripoti ya uchunguzi wa ajali ilisha toka?
  KUMBUKUMBU ZINANIONYESHA Mv BUKOBA ILIZAMA USIKU WA KUAMKIA TAREHE 21/MAY/199,kuna lipi jipya la kutufanya tuadhimishe tarehe 25?hata hayo maadhimisho yenu sipendi kuyasikia.

  K
   
 20. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #20
  May 17, 2010
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Basi tutoe utaratibu wa kuadhimisha bila kutoneshana vidonda, maana wakati huo ukifika picha zote za tukio lile uoneshwa upya kwenye TV, ni kwa nini kila mtu asiadhimishe kivyake? wengine tunaonaje ? maana siku zinakaribia.
   
Loading...