Wangari Maathai
JF-Expert Member
- Aug 13, 2018
- 34,962
- 70,472
Mimi nilipata ajali hapo nikiwa naenda kilimanjaro october 1996 tukiwa ndani ya SAWAYA basi yetu ilifeli break lkn derva alimudu kuongoza kwenye zile kona, wakati tunaanza tu kuingia kwenye daraja tayari upande wa pili TAYASARI ikitokea tanga ilikuwa imefika katikati ya daraja. yule dereva kule alikuwa mtu mzima sana alichoamua ni kufunga break na kusimama maana ilishakuwa too late hata kurudi nyuma.
Ile collision ilitokea pale asikuambie mtu ni kama tulikuwa tumebeba stool tumekalia, tuliokuwa nyuma tuliondoka na viti hadi mbele ingawa wakati huo kule mbele yalikuwa mabati yameshikana na kiasi hata cha milango yote kubanwa na tuliokuwa na afadhali tulitokea madirishani.
Mambo ni mengi ila niseme tu kama tayasari isingesimama tungetumbukia wote mtoni maana ile ndio ilikuwa kama kinga yetu. RIP kwa madereva wote wawili pamoja na abiria maana pale pale palikuwa na death kama 20 kwa ujumla wao na wengine walienda kufariki baadae tumbi na muhimbili.
Wakati ule hakukuwa na msaada wa haraka maana ajali ilitokea saa nne na majeruhi walianza kuchukuliwa saa kumi na gari ya jeshi. yani mtu anapoteza damu hadi anafariki.
Duh...! Ilikuchukua muda gani kusahau tukio??duh inatosha Sana...hukuachwa na majeraha makubwa?pole sana