Ajali ya moto msitu wa Amazon: Wataalam Wizara ya Maliasili, Jeshi la zimamoto wamekaa kimya tu mpaka sasa. Mahusiano na umma imekaa vipi hapa?

Kisoda James

JF-Expert Member
Jun 11, 2020
1,113
2,000
Shikamooni wakubwa zangu wote wa humu jamiiforums. Mimi mdogo wenu Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya.

Baada ya shambulizi ya kigaidi katika chuo kikuu cha Garisa nchini Kenya, mkuu wa jeshi la Polisi kamanda Simon Sirro alijitokeza mbele ya umma na kusema ya kuwa wanasikitishwa sana na shambulio lile na kutoa salama za pole kwa ndugu zetu wa Kenya kisha akatoa assurance kwa wanavyuo ya kuwa usalama umeimarishwa meneo yote ya vyuo hapa nchini katika kuhakikisha ya kuwa hakutakuwa na tukio la namna ile hapa nchini.

Baada ya ajali ya gari la wanafunzi wa shule ya msingi ya Lucky Vincent iliyopo jijini Arusha, mkuu wa kitengo cha usalama barabarani mkoani hapo aliamuru kuwe na ukaguzi yakinifu kwa gari zote za wanafunzi ili kutathmini roadworthiness ya kila school bus.

Kuna habari zina trend sana kwenye vyombo vya habari vya kimataifa juu ya kuungua moto msitu wa Amazon uliopo nchini Brazil ambapo mpaka ninavyoandika, thousands of hectors have been consumed by that deadly blaze.

Kwanini sijaona Waziri wa Maliasili wala Commissioner mkuu wa Jeshi la zimamoto na uokoaji hapa Tanzania akitoa assurance kwa watanzania hususan wanaokaa maeneo jirani na misitu yetu pamoja na mbuga za wanyama na kueleza wamejipanga vp katika kukabiliana na suala hili endapo litajitokeza????

Mimi ninafikiri labda kungeundwa jopo la Wataalam wa Wizara ya maliasili pamoja na wale wa kutoka jeshi la zimamoto ili kuweza kutathmini loopholes zilizopo zinazoweza kusababisha mlipuko wa moto pamoja na kutoa assurance ya usalama kwa watanzania waishio karibu na hifadhi na misitu mikubwa

OUR MOTTO: KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Kilimanjarooooooooo
 
KUTATABHETAKULE

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
3,312

Nakupongeza sana Poti, uliona mbali. Sasa hivi ndio wanajadili ununuzi wa ndege za kupambana na moto katika hifadhi za Taifa wakati moto umepamba moto pale Mlimani. Kawaida yetu tunafanya maaamuzi kwa matukio. Kama hakuna moto, tupo kimya. Ukiwaka tu ndo utasikia njia ambazo zitatumika kuuzima moto huo jambo ambalo lilipaswa kufanyika kabla ya hapo. Wakati wa kiangazi tupo kimya. Mvua ikinyesha na mafuriko yakitokea ndio tunafikiria kujenga barabara imara pale Msimbazi na pia kutoa mabilioni ya fedha kwa ujenzi wa madaraja. Kwa mwendo huu tunajidanganya miaka nenda miaka rudi na hatufiki popote.
 
KUTATABHETAKULE

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
3,312
2,000
Inasikitisha sana mkuu. Ila ninahisi ni kwa sababu ya uhaba wa pesa kwa hizi nchi zetu za uchumi mdogo huku Afrika...
Mkuu usisahau kupanga ni kuchagua. Tunachagua kufanya mambo makubwa sana na kuyasahau yake madogo ambayo pengine ni ya muhimu zaidi. Barabara ya Msimbazi ni ya siku nyingi na tatizo la mafuriko hapo linafahamika miaka nenda miaka rudi. Hatuoni nia ya dhati ikifanyika kuwaondolea wakazi wa Jiji adha hii. Fedha ya kufanya haya ipo, lakini hili si kipaumbele chetu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom