Ajali ya moto msitu wa Amazon: Wataalam Wizara ya Maliasili, Jeshi la zimamoto wamekaa kimya tu mpaka sasa. Mahusiano na umma imekaa vipi hapa?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa humu jamiiforums. Mimi mdogo wenu Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya.

Baada ya shambulizi ya kigaidi katika chuo kikuu cha Garisa nchini Kenya, mkuu wa jeshi la Polisi kamanda Simon Sirro alijitokeza mbele ya umma na kusema ya kuwa wanasikitishwa sana na shambulio lile na kutoa salama za pole kwa ndugu zetu wa Kenya kisha akatoa assurance kwa wanavyuo ya kuwa usalama umeimarishwa meneo yote ya vyuo hapa nchini katika kuhakikisha ya kuwa hakutakuwa na tukio la namna ile hapa nchini.

Baada ya ajali ya gari la wanafunzi wa shule ya msingi ya Lucky Vincent iliyopo jijini Arusha, mkuu wa kitengo cha usalama barabarani mkoani hapo aliamuru kuwe na ukaguzi yakinifu kwa gari zote za wanafunzi ili kutathmini roadworthiness ya kila school bus.

Kuna habari zina trend sana kwenye vyombo vya habari vya kimataifa juu ya kuungua moto msitu wa Amazon uliopo nchini Brazil ambapo mpaka ninavyoandika, thousands of hectors have been consumed by that deadly blaze.

Kwanini sijaona Waziri wa Maliasili wala Commissioner mkuu wa Jeshi la zimamoto na uokoaji hapa Tanzania akitoa assurance kwa watanzania hususan wanaokaa maeneo jirani na misitu yetu pamoja na mbuga za wanyama na kueleza wamejipanga vp katika kukabiliana na suala hili endapo litajitokeza????

Mimi ninafikiri labda kungeundwa jopo la Wataalam wa Wizara ya maliasili pamoja na wale wa kutoka jeshi la zimamoto ili kuweza kutathmini loopholes zilizopo zinazoweza kusababisha mlipuko wa moto pamoja na kutoa assurance ya usalama kwa watanzania waishio karibu na hifadhi na misitu mikubwa

OUR MOTTO: KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Vp kuhusu swali langu??
Labda wanaona hayo ni masuala ya mafahari wa Dunia (i.e. G7) kuyashughulikia. Ila kama ulivyosema tungechukua kama somo kujiandaa na janga kama hilo endapo litaikumba misitu yetu. Ila ujue Amazon ni msitu wa Dunia kwani unachangia kupunguza 20% ya green house gas Duniani, hivyo madhara yake yataiathiri Dunia nzima. Msitu nambari 2 ni wa Congo huko
 
Labda wanaona hayo ni masuala ya mafahari wa Dunia (i.e. G7) kuyashughulikia. Ila kama ulivyosema tungechukua kama somo kujiandaa na janga kama hilo endapo litaikumba misitu yetu. Ila ujue Amazon ni msitu wa Dunia kwani unachangia kupunguza 20% ya green house gas Duniani, hivyo madhara yake yataiathiri Dunia nzima. Msitu nambari 2 ni wa Congo huko
Sawa brother nimekuelewa ipasavyo
 
Back
Top Bottom