Ajali ya moto Morogoro: Je, Serikali itafanya DNA test investigation ?

Tukana tu Ila najua maneno yamekuingia vilivyo..yamekuchoma vilivyo...
Nenda kwa Mungu katika roho na kweli ukaombe msamaha kwa maneno yako..
Narudia tena, weka picha ya mama yako baba yako na mkeo na watoto wamechomeka kwenye huo Moto..je you will call them vibaka?
Haiwezi kutokea, familia yangu haina vibaka au mataahira
 
Wakati wa kusajiliwa vitambulisho vya Taifa niliwauliza maafisa wa NIDA kuwa baada ya kuchukuliwa alama za utambuzi wa vidole, ni lini tutachukuliwa sample za DNA ili yanapotokea majanga kama haya ya moto na kufa maji ambapo miili huharibika ili utambuzi wa kisayansi utoe majibu haraka walinijibu ni awamu nyingine nikashangaa baada ya muda napewa kitambulisho.
 
Uliwaza mbali lakini majibu yamekuwa mepesi sana
 
Nimemsikiliza mama mmoja hapa Itv yeye anasema jana wamechukuliwa DNA na majibu yametoka leo na mwili umetambuliwa kwa vipimo vya DNA!!! Hii DNA ya majibu ndani ya saa 24 kama majibu ya malaria!!!sijawahi kuisikia. Mamlaka zina kazi sana kuna mwingine kaja kutambua mwili wa jirani anaulizwa jina halijui
 
Attachments

  • 20190811_122550.jpg
    20190811_122550.jpg
    143.6 KB · Views: 15
Nilitaka nitumie neno forensic investigation lakini hii ni tofauti na DNA kwakuwa hii inajumuisha pamoja na ushahidi mwingine eneo la tukio... Wakati hili la Morogoro ni kutaka kupata utambuzi wa wahanga.....

Mida kama hii usiku wa jana hakuna aliyefhani nini kinaweza kutokea leo... Hata marehemu wote walilala wakiwa na afya tele na pengine wakiwaacha ndugu na jamaa wakiwa wagonjwa mahospitalini... Waliamka wakiwa kila mmoja ana mipango yake....
Ajali huwa haipangwi hivyo ajali ya Moro ilivuruga mipango ya wengi... Wakaahirisha shughuli zao kujipatia riziki ya bure... Kilichotokea baada ya hapo kinajulikana.. Ni msiba mkubwa wa watu waliokufa kwa kuungua na moto beyond recognition
Ni wazi ndugu jamaa na marafiki watapenda kila mmoja wapate mwili halisi wa ndugu yao ili wakafanyie mazishi kwao... Lakini hili ni jukumu zito mno kwa serikali
Miili yote ile karibia miamoja iliyochomeka kiasi kile kuufanyia kila mmoja uchunguzi wa kitaalam kupata utambulisho wake halisi si kazi ya kitoto wala ya muda mfupi...
Sina hakika sana na hili lakini nadhani serikali haina maandalizi ya dharura ya kufanya jambo kubwa kama hili
Kuna changamoto ya nguvu kazi
Kuna changamoto ya timu za wataalam
Kuna changamoto ya sehemu za kuhifadhia miili yote ile kwa muda mrefu
Kuna changamoto ya madawa na vifaa tiba vya kushughulikia miili kama ile
Kuna changamoto ya miundombinu....

Ni wazi eneo ilipohifadhiwa miili hapafai kwa harufu ya nyama iliyoiva... Huyu unaweza kuitwa uchafuzi wa mazingira pia... Harufu husika pamoja na picha za miili iliyoungua vinaweza kuwafanya baadhi wasile nyama tena
Kwa jinsi hali ilivyo pengine serikali itachukua hatua za haraka za kufanya mazishi ya pamoja na kutamatisha janga husika.... Itakusanya majina ya wanaoweza kuwa wako kwenye ajali kutoka kwa ndugu na jamaa... Lakini kwa hakika haitakuwa kwa asilimia miamoja

Morogoro ni mji wenye wakazi wengi wahamiaji... Je wanatambulika wote kwenye mfumo rasmi wa utambuzi serikalini?
Ajali imetokea njia kuu.. Inawezekana kabisa kuna wapita njia ambao si wakazi wa eneo hilo nao wakawa ni wahanga..
Nina hakika kuna ambao walitoka alfajiri kwenda mbali na hapo nje kabisa ya mji kusiko na mawasiliano wakajumuishwa humo... Siku wakirudi watu wasiwakimbie
Kuna wengine watakufa ama watapotea nje kabisa ya ajali husika nao watajumuishwa humo....
Kwenye hili tusiilaumu sana serikali yetu bali sasa ione umuhimu wa kujiandaa na dharura kama hizi... Miili ya ajali nje ya moto inaweza kutambulika kwa urahisi lakini ya moto huunguza mpaka nyaraka muhimu hivyo tunahitaji neno la serikali kwenye hili...
Huu si msiba mdogo hata kidogo
Taifa limepoteza nguvu kazi kubwa kwa mara moja
Vipaji na vipawa
Viongozi watarajiwa
Baba na mama
Shangazi na mjomba
Dada na kaka
Marafiki na jamaa
Yatima, wagane na wajane wameongezeka...
Tuomboleze kwa pamoja
Askari kanzu.
 
Nimemsikiliza mama mmoja hapa Itv yeye anasema jana wamechukuliwa DNA na majibu yametoka leo na mwili umetambuliwa kwa vipimo vya DNA!!! Hii DNA ya majibu ndani ya saa 24 kama majibu ya malaria!!!sijawahi kuisikia. Mamlaka zina kazi sana kuna mwingine kaja kutambua mwili wa jirani anaulizwa jina halijui
kwahyo ni masaa mangap mkuu kufanya DNA testing?
 
Hiyo inaitwa noma Kg1 unusu
Miaka ile ya 90 kuna ajali ilitokea pale Tanga mjini siku ya ijumaa kuna bus liligongana na treni na walikufa watu si chini ya 30 palepale..
Kulikuwa na mtumishi wa halmashauri ya Lushoto ambaye aliaga kazini kuwa anaenda Tanga kumbe kufika korogwe alishuka na kubadili mwelekeo akienda handeni bila kuwataarifu aliowaaga
Baada ya taarifa za ajali kuenea kukawa kuna mwili ambao mavazi yake yalishabibiana na yule mtumishi wa halmashauri ya Lushoto
Hivyo watu wa Lushoto wakajiandaa na msiba... By then hakukuwa na simu za mkononi wala tv na bishost alikoenda pengine hakukuwa na redio au hakupata muda wa kusikiliza
Alirejea Lushoto Jumapili jioni na kukuta kwake kumeweka msiba wake....
 
Jana nilipita kijiwe fulani nikasikia jamaa wanasema kuna kibaka mzoefu wa Kihonda Mbuyuni naye kapoteza maisha kwenye hiyo ajali, jamaa wakawa wanafurahia kweli maana huyo kibaka alikuwa tatizo sana mtaani
Maisha ni kitu cha ajabu sana na wanadamu ni watu wa kushangaza mno.... Hapa kuna watu wanafurahia kimyakinya hii ajali
Wadeni wamekufa
Wauza boda boda hii ni fursa mpya
Wauza majeneza
Watafuta ajira za boda boda
Wanasiasa

Wahenga walisema: kufa kufaana... Machozi ya wengi yatakuwa ya mamba
 
Jana nilipita kijiwe fulani nikasikia jamaa wanasema kuna kibaka mzoefu wa Kihonda Mbuyuni naye kapoteza maisha kwenye hiyo ajali, jamaa wakawa wanafurahia kweli maana huyo kibaka alikuwa tatizo sana mtaani
 
Miaka ile ya 90 kuna ajali ilitokea pale Tanga mjini siku ya ijumaa kuna bus liligongana na treni na walikufa watu si chini ya 30 palepale..
Kulikuwa na mtumishi wa halmashauri ya Lushoto ambaye aliaga kazini kuwa anaenda Tanga kumbe kufika korogwe alishuka na kubadili mwelekeo akienda handeni bila kuwataarifu aliowaaga
Baada ya taarifa za ajali kuenea kukawa kuna mwili ambao mavazi yake yalishabibiana na yule mtumishi wa halmashauri ya Lushoto
Hivyo watu wa Lushoto wakajiandaa na msiba... By then hakukuwa na simu za mkononi wala tv na bishost alikoenda pengine hakukuwa na redio au hakupata muda wa kusikiliza
Alirejea Lushoto Jumapili jioni na kukuta kwake kumeweka msiba wake....
Aaiiiighoooo
 
Itabidi tuanze kutumia vitambulisho vya chuma.

Itabidi ndugu tuanze kuvaa vitu vitakavyo tutambulisha, visivyo ungua kirahisi mfano cheni (naonaga wajeshi wakiwa vitani akifa mmoja wao hua wanakata cheni yake na kuipeleka katika familia take).

Sema ajari ilihusisha moto ila samahani jamani hivi tungefanya hivi..... Sijui ingependeza??? Yani yale mazishi ya kihindi, miili yote ingechomwa kwa pamoja hadi kua majivu na kila mtu akapewa majivu kiasi akazike anavyojua..... Sema sio utamaduni wetu ila angalau unakua na uhakika kwamba kwa kiasi flani kutakua na jivu la ndg yako kuliko kupewa mwili usio wa ndg yenu kabisaa
 
Mmh umewaza mbali lakini tuna safari ndefu hadi kufika huko!
 
24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom