Ajali ya Meli Zanzibar: Meli kama chombo na mazingira ya ajali

kwa TZ hii kupata idadi ya waliokuwepo kwenye meli ni ndoto na ni vigumu kujua idadi ya waliokufa................Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi Amina.
 
mi nafkiri ifike wakati sasa tujue serikali iko kwa maslahi yao bonafsi...tulianza na mv bukoba wakasema wamejianda ikitokea dharura ya meli kama ile sasa huu upuuzi wa meli kuzama saa nane usiku wanaenda saa kuminambili na dk 45 kama umesikia waliopolewa kule clouds unaweza lia kwa kweli mmoja anasema alikuwa na kazi ya kuwarushia wenzake magodoro yaliokuwa store ila kuna wengi wakazama nayo na kuanza kuyashikilia lakini upepo ulivyokuwa mkubwa ndivyo na wengi wakaanza kuchoka na kuyaacha magodoro kuambulia maiti zilizoopolewa...yule kaka amenisikitisha sana sana anasema kuna mama amengangana nae akaona mtooto mmoja anazama akamkimbilia na kumfunga kwenye shati ya ke kwa juu huku wanashikilia godoro gafla yule mama akaachia akamwambia bora nife kuliko kuteseka hivi mwanga umeanza kuonekana akuna hata wa kunisaidia
Hii nchi ni ya kishetani sumtra mashetan watupu na wenzao wote....,
 
Awali habari zilipoanza kutoka kuhusu kuzama kwa meli ya mv Spice ilielezwa kuwa zaidi ya watu 2000 wanahofiwa kufa.

Habari zimebadilika mpaka vyombo vya habari vinatangaza watu 163 kufa na zaidi ya 500 kuokolewa.

Kwa wajuzi wa safari za meli na hali ilivyokuwa siku meli ilipoanza safari na kwamba meli yenyewe imezama tena katikati ya bahari zipo kila sababu kuamini kwamba maisha ya watu yamepuuzwa kwa faida za kisiasa.

Ukweli utabaki ni ule wa mwanzo kwamba watu 2000 wanahofiwa kufa. Binafsi nina sababu za kuamini kuwa zaidi ya 1000 watakuwa wamekufa iwapo watakaookolewa watajumlisha idadi ya 2000.

Watanzania tusiendekeze huu utamaduni wa exaggeration. Idadi hiyo ya 2000 ni kubwa mno kwa meli ile. Tukubaliane kwamba idadi inayotajwa na vyombo vya habari baada ya kuhakiki tukio la uokoaji wa walionusurika na uopoaji wa miili turidhie kwamba ni taarifa sahihi kwa sasa na kama kuna kupishana ni kidogo tu kwa vile kuna uwezekano wa baadhi ya miili kusombwa mbali na mawimbi ya bahari.
 
Awali habari zilipoanza kutoka kuhusu kuzama kwa meli ya mv Spice ilielezwa kuwa zaidi ya watu 2000 wanahofiwa kufa.

Habari zimebadilika mpaka vyombo vya habari vinatangaza watu 163 kufa na zaidi ya 500 kuokolewa.

Kwa wajuzi wa safari za meli na hali ilivyokuwa siku meli ilipoanza safari na kwamba meli yenyewe imezama tena katikati ya bahari zipo kila sababu kuamini kwamba maisha ya watu yamepuuzwa kwa faida za kisiasa.

Ukweli utabaki ni ule wa mwanzo kwamba watu 2000 wanahofiwa kufa. Binafsi nina sababu za kuamini kuwa zaidi ya 1000 watakuwa wamekufa iwapo watakaookolewa watajumlisha idadi ya 2000.
Hii ni Afrika bwana, ambapo roho ya mtu haina thamani. Utapigwa risasi, utafungwa jela, utapata ajali na hata ndugu zako wasitambue... Ipo siku Mungu naye atakuwa upande wetu.
 
hata mimi ningependa kujua.......najaribu kupiga picha akilini mwangu.....usiku na baharini kulivyo na giza.....hao waliozama na meli si watakuwa waliteseka sana.....unatakiwa ujiokoe kwa wakati huo huo huoni vizuri......Mungu awarehemu kwa kweli....
 
inahusiana na mambo ya kimazingara kama ya majini,,wanadai majini ya baharini yanakuwa yamelala usiku
 
Hii meli ikilinganishwa na meli za kubeba ndege za kivita ni ndogo sana lakini tofauti na meli hizo  hii ilikuwa ni neema kubwa kwa wakulima wa Tanzania nzima.Siku ikifika kule Tanga huwa ni sherehe kwa wafanyabiashara wa bidhaa za aina zote.Mara nyingi wafanyabiashara hao huwa wameagiza mazao kutoka umbali hata Iringa na Arusha wachilia mbali Lushoto ili kuwahi soko.Mafuso pale bandarini yasiyo idadi hupanga foleni kupeleka bidhaa kuanzia Jumapili inapotia nanga mpaka Jumanne inapoondoka
Hivyo tofauti na meli za kivita hii meli ilikuwa inazalisha mamilioni ya fedha
Anayetilia shaka idadi ya abiria zaidi ya 2000 hajui maana ya meli na uwezo wake wa kubeba.
Jee umewahi kuona feri za pale Mtongwe na Likoni Mombasa zinaposhusha watu na magari?.Huwezi kuamini,utadhani wanatoka uwanja wa taifa Temeke.Basi hii meli mv spice kwa abiria ni zaidi.na abiria wenyewe wengi watoto
 
Niliwahi kumuuliza jamaa mmoja anayefanyakazi humo humo kwenye Meli akanambia ni kwasababu ya upepo ambapo mchana unakuwa mlali sana kuliko usiku. Sina hakika na jibu hili lakini! Ila kama ulisoma sea breeze na land breeze unaweza kuwa na jibu linalokaribia ukweli!
 
Niliwahi kumuuliza jamaa mmoja anayefanyakazi humo humo kwenye Meli akanambia ni kwasababu ya upepo ambapo mchana unakuwa mlali sana kuliko usiku. Sina hakika na jibu hili lakini! Ila kama ulisoma sea breeze na land breeze unaweza kuwa na jibu linalokaribia ukweli!
<br />
<br />
ukisema kuhusu izo breeze sidhani kama utakua upo sawa mkuu,, kwa sababu, usiku, maji yanakua yamepata moto kutokana na jua la mchana, na maji yanacool taratibu sana, soo maji yanakua low pressure zone, wakati huku ardhini, kunakua high pressure zone since it is colder, so the breeze will move towards the sea, and hence create more disturbances kwenye bahari kulinganisha na mchana, ama nimekosea wadau??
 
Meli zote dunia tena zile zinazofanya safari ndefu kutoka bara moja mpaka lingine huwa zinaaza safari zake usiku.
Hakuna tatizo lolote tatizo meli zetu ni mbovu
 
Natamani Mungu angekuwa anashuka at the moment pindi mtu hasa kiongozi mkubwa wa cnhi au idara unaudanganya umma,hivi ni kweli waliokolewa hai wanafika idadi hiyo,na je waliokufa ni idadi hiyo tu?kama ni hivyo manifesto iwekwe wazi mbona kama imepotea?na je meli ilikuwa imebeba tani ngapi za mzigo na je capacity ya meli ni kubeba tani ngapi?je Nani alisaini Meli kuondoka bandarini,nani aliifanyia ukaguzi kabla ya kuondoka?Je report za kitaaluma zinasema meli ilikuwa na tatizo gani kwa kipindi japo cha miezi mitatu ya nyuma na je ilipatiwa matengenezo?Je ilituwaamini hawa kwa siku zijazo wananchi na waathirika wote wa majanga makubwa haya tufanyaje?maana ya MV Bukoba,ya Treni pale Nsagali-karibia Dodoma na la MV Spice kutokea inamaana hakukuwa na fundisho lolote kwa matukio ya nyuma na mambo yaliendelea kufanyika kwa mazoea.Tuambie ukweli tujue watanzania wenzetu wangapi wamepoteza maisha,jamani wenzetu mlioko Zanzibar shirikianeni na walioko Pemba mjue ukweli wa ndugu waliofariki,wala msitumie JF kutoa habari zisizo rasimi semeni ukweli tutawaamini kuliko wenzetu wa Chama chetu na mwenzao B.


Kwani Gongo la Mboto na Mbagala aliwajibika nani? Subiri si muda utasikia tena kwenye kambi nyingine "kumesanuka" hatimaye tunakuwa kama Somalia na Sudan na wengineo kwamba tumezoea matatizo,majanga na vifo sema tu kwetu vinatokea periodically! Nashangazwa sana ninaposikia mtu mzima na mvi kichwani tena ni muhusika anajibu huku akitabasamu eti hajui meli ilibeba watu wangapi? kwani hiyo ni Sumry kusema kwamba ilipakia watu wengine njiani?? F***k 'em up! Tunatafuatiana ban bureeeeeeeeeeee!
 
Hivi kuna sababu yoyote ya kisayansi juu ya hili?? Maana MV BUKOBA ilikuwa alfajiri na hii ya zanzibar nayo ilianza safari usiku, kuna sababu yoyote ya kutembea usiku!!
mi nadhani ni ratiba tu coz kulikuwa na mv mapinduzi, mv maendeleo, mv flying horse, na nyenginezo mbona zilikuwa na nyengine bado zinatembea vizuri tu mchana. mi nadhani kwa kuwa hizi ni meli huwa zinasubiri harakati za mizigo na abiria hivyo huona ni vyema mara nyingi kutumia muda wa usiku kwa safari zao. kuh; "majini hakuna ukweli" kila wakati wazee hao wapo tu. simply ni mambo ya logistics.
 
Hivi kuna sababu yoyote ya kisayansi juu ya hili?? Maana MV BUKOBA ilikuwa alfajiri na hii ya zanzibar nayo ilianza safari usiku, kuna sababu yoyote ya kutembea usiku!!
Katavi taingi juzi nakuambia hii ni Boti (Ferry) sio Meli, anyway hakuna tatizo kufanya safari usiku tena ni vizuri sababu maji yanakuwa yametulia.
Tatizo ni nchi yetu hawapo makini kuangalia safari za majini usalama wake!
 
bahari huwa inatema kila kitu, kama wenye nchi watakuwa tayari kupata idadi kamili mbona itapatikana.
 
Poleni waTanzania wote kwa msiba huu mzito. Roho za marehemu zipumzike kwa amani, Amen.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom