Ajali ya Meli: Utata wa umiliki wa meli na tamko la Serikali

Wadau ndani ya Jf

kila nisikilizapo habari kupitia vituo mbalimbali watu na hata wafanyakazi wa bandalini wamekuwa ni wazito kuwataja wamiliki wa meli iliyozama

kwani kuna nini hapa? yaani hata viongozi wa wakuu wa serikali pia wamesikika wakiwa na kigugumizi cha kuwataja wahusika tunachosikia ni kuwa meli ilitengenezwa mwaka 1966 na wamiliki walikuwa wakibadilishana umiliki siku hadi siku

lakini mmiliki wa mwisho hadi meli ina zama amekuwa kama mungu kila mtu anaogopa kumtaja

kweli Tanzania tumefikia hapa tulipo kwa kuwaficha waliotuumiza?

wadau tunaomba tujue majina kamili ama kampuni iliyokuwa ikimiliki meli hiyo

KARIBUNI
Hivi mmiliki anahusika vipi?

Maswaali yako mengi ni zuga tuu,wewe unataka kuuliza kwa nini walaumiwe voda??? hayo mengine danganya toto!!

Watu wanaosema voda ni ya kulaumiwa wanalao jambo, hao wanataka kutufanya wa TZ tuache kuangalia chanzo cha ajali. Wapo wa kulaumiwa kuliko kuilaumu voda, kwani voda ndio chanzo..ni ujinga kuacha kuangalia chanzo na kuangalia mengine. Kulaumu voda hiyo haisaidi hata kidogo.

Ngoja nijaribu, kama mtihani wa hisabati umekuwa wa multiple choice, nadhani ntabahatisha tu.
1.Meli ni ya nani?-Makame
2. Msiba ni wa nani?-wazanzibari
3. Kwa nini lawama zimehamishiwa voda?-kwakuwa wameshindwa kuheshimu "articles" of union

4. Kwa nini tunawaza kichovu hivi? - kwa sababu tumechoka kuomboleza

5. Meli ilianza kuzama usiku. Hadi asubuhi meli ilikuwa inaelea urefu wa magoti. Huo muda haukutosha kuokoa?-tulikuwa tunasubiri wapiga mbizi toka sauzi
6. Pasingekuwa na shindano lawama zingekwenda wapi?-bado nafikiria!
Mwisho wa siku wa kulaumiwa ni mfumo. Wanaoilaumu na kuilaani voda ni wehu tu. Watz tutapelekeshwa hadi lini. Leo airport haina umeme. Nani alaumiwe? Nawasihi watz wenzangu, tuwe radical. Tuwe na uwezo wa kuhoji vyanzo ya matatizo na sio matokeo yake. Hii nchi ingekuwa inaendeshwa kwa WHAT IF fomula ladda tungekuwa mahala.

Nchi inaendeshwa kwa RULE OF THUMB. Siku tutakapokuwa na akili za kupambanua ndipo tutakuwa na uhuru wa kweli. Wazanzibari poleni, ila na nyie msiingie kwenye huu mkumbo wa kulaani msivyojua. Pokeeni misaada ya voda. Misiba na majanga vitatokea ila maisha LAZIMA yasonge

Mwenyemeli amahusika kwa kuwa na limeli libov lililoongezwa uref kinyemela na lisilona matengenezo

Said Salim Bhakresa ndiye aliyekuwa mmiliki wa AWALI - lakini miaka kama mitano hivi iliyopita aliiuza hii meli kama "chuma chakavu" kwa wajasiliamali wa vyuma chakavu - @ a throw away price ... na hakutarajia kama mnunuzi angeweza kuendelea kuitumia kama MELI!

Nimejaribu kuangalia katika wavuti mbalimbali na zote ninakutana na sentensi hii, kauli ya Muhammed ABoud
"The government is holding the chief engineer for questioning in order to gather details," Mr. Mohammed said. "The captain of the ferry is still missing, and the government doesn't know precisely the owner of the ferry."

Sasa ikiwa serikali inathibitisha kuwa haimjui mmiliki wa meli, kama vile ambavyo mpaka leo hajulikani mmiliki wa Dowans, hawa viongozi wetu wanatupeleka wapi? Kwa mtu yeyote mwenye uungwana (utu) japo kidogo asingethubutu kutamka maneno hayo. Inakuwaje mnakaribisha wawekezaji vivuli?

Mambo yakienda sawa aibu zenu zinafichika, lakini kwa tukio kama hili inathibitisha wazi kuwa Tanzania tuna "Bora viongozi", viongoz ambao wakishakuhongwa suti, pesa na hongo nyengine, hawajali yatayowafika wananchi; na ndio maana Tanzania kunaingizwa vyakula vibovu, madawa yaliyopitiwa na muda, na kila aina ya "uchafu wa dampo". Baadaye bila haya, wanamsingizia Mungu. Ikiwa kila linalotokea ni kwa amri ya Mungu, kwa nini tena mnakamata na kuwafunga wahalifu (wezi wa kuku na bata) au hawa hawana Mungu? Masikini Watanzania.

Hapo kwenye red.... Mimi nimesoma gazeti moja la kimarekani wameandika vile vile kama ulivoandika hapa, sasa nilipatwa na maswali lukuki kwamba hawa jamaa wanaisingizia serikali yetu.. yaani meli ifanye kazi bila hata kufahamika mmilik wake, kweli?

Ina maana hawa jamaa wenye meli walikuwa hawalipi kodi? na kwanini hawafahamiki? Ni kweli Aboud kasema kuwa hawafahamiki na hili ni tatizo kubwa...

Aibi, aibu,aibu............hapa tanzania tofauti na nchi nyingi za Africa ni nchi pekee ambayo ni rahisi ku-locate owner of any thing. Kama system inafanyakazi vizuri basi BRELA ni one stop shop ambapo unaweza kupata mmiliki wa anything in a munite- nashauri tuache kujadiri hili kwani paparazo mmoja tu anaweza kwenda pale akapewa detail za ownership wote waliowahi kuimiliki. Kutipatikana kwa taarifa hizi means hili dude lilikuwa linasanya bila kulipa kodi?!.
Nimejaribu kuangalia katika wavuti mbalimbali na zote ninakutana na sentensi hii, kauli ya Muhammed ABoud

"The government is holding the chief engineer for questioning in order to gather details," Mr. Mohammed said. "The captain of the ferry is still missing, and the government doesn't know precisely the owner of the ferry."

Sasa ikiwa serikali inathibitisha kuwa haimjui mmiliki wa meli, kama vile ambavyo mpaka leo hajulikani mmiliki wa Dowans, hawa viongozi wetu wanatupeleka wapi? Kwa mtu yeyote mwenye uungwana (utu) japo kidogo asingethubutu kutamka maneno hayo. Inakuwaje mnakaribisha wawekezaji vivuli?

Mambo yakienda sawa aibu zenu zinafichika, lakini kwa tukio kama hili inathibitisha wazi kuwa Tanzania tuna "Bora viongozi", viongoz ambao wakishakuhongwa suti, pesa na hongo nyengine, hawajali yatayowafika wananchi; na ndio maana Tanzania kunaingizwa vyakula vibovu, madawa yaliyopitiwa na muda, na kila aina ya "uchafu wa dampo". Baadaye bila haya, wanamsingizia Mungu. Ikiwa kila linalotokea ni kwa amri ya Mungu, kwa nini tena mnakamata na kuwafunga wahalifu (wezi wa kuku na bata) au hawa hawana Mungu? Masikini Watanzania.

Wadau ndani ya Jf

kila nisikilizapo habari kupitia vituo mbalimbali watu na hata wafanyakazi wa bandalini wamekuwa ni wazito kuwataja wamiliki wa meli iliyozama

kwani kuna nini hapa? yaani hata viongozi wa wakuu wa serikali pia wamesikika wakiwa na kigugumizi cha kuwataja wahusika tunachosikia ni kuwa meli ilitengenezwa mwaka 1966 na wamiliki walikuwa wakibadilishana umiliki siku hadi siku

lakini mmiliki wa mwisho hadi meli ina zama amekuwa kama mungu kila mtu anaogopa kumtaja

kweli Tanzania tumefikia hapa tulipo kwa kuwaficha waliotuumiza?

wadau tunaomba tujue majina kamili ama kampuni iliyokuwa ikimiliki meli hiyo

KARIBUNI

Bila shaka ni yale yale. Akitajwa nchi itatikisika na usalama wa nchi utakuwa hatarini. Si tumeshaambiwa mambo mengine ni nyeti hamuelewi tu???

Mwenyemeli amahusika kwa kuwa na limeli libov lililoongezwa uref kinyemela na lisilona matengenezo

Mmiliki
Waziri mwenye dhamana ya usafirishaji
Watu wote waliopewa dhama ya kuangalia usalama wa vyombo hivi vya majini
Nahodha wa meli
wakata tickets
wafanyakazi wote wa meli
Mkurugenzi wa nanihii
Mkurugenzi wa nanihii
mapolisi wa bandari ya malindi
Na wengine wengi

Lakini kwa vile nchi hii haina utamaduni wa kuwajibishana, basi tushukuru Mungu tungoje janga lingine.

serikali ikisha kubali kuendeshwa na wafanya biashara
kamwe haiwezi kuwakemea !!! sishangai kwa mmiliki kutofahamika
au mnataka kampeni zifurugike???

8Dw8jarSfjcbEAAAAASUVORK5CYII=

Ayoub Hashim Jaku ni mbunge na mwakilishi wa CCM Muyuni Unguja

source. mwanahalisi

Back
Top Bottom