Ajali ya Meli: Utata wa umiliki wa meli na tamko la Serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajali ya Meli: Utata wa umiliki wa meli na tamko la Serikali

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bajabiri, Sep 12, 2011.

 1. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nimeshtushwa sana na taarifa kuwa serikali haimjui mmiliki wa meli ya M,V Spice Islander ambayo imepata ajali hivi karibuni.......akizungumza na waandishi wa habari waziri Mohamed Aboud amesema"Sisi hatumjui mwenye kumiliki meli hii la ukweli lazima tuliseme,shirika la bandari ndilo lenye taarifa zote".
  Lakini SUMATRA walipoulizwa walisema kuwa meli hiyo inamilikiwa na SAID BACWASH kupitia kampuni ya ALHUBRA SHIPPING CO.
  sosi:mwananchi la 12/09/2011
   
 2. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,078
  Likes Received: 7,287
  Trophy Points: 280
  Unashangaa nini sasa?
  Kama waliweza kusema hawawajui wamiliki wa Kagoda ndio itakua hiyo meli?
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (au serikali ya umoja wa kitaifa) imetangaza kupitia waziri wake wa uchukuzi Mohammed Abud kwamba haijui mwenye meli iliyozama SPICE ISLANDERS ni ya nani! Hii inawezekana? Inasemekana ni meli ya kigogo mmoja wa huko visiwani. mambo yanaanza kufichwa kabala hata ya tume ya uchungzi kuundwa.

  Pia serikali hiyo imetangaza kwamba mhandisi mkuu wa meli hiyo katiwa mbaroni na viombo vya dola. Hiyo ni sawa kabisa. Lakini cha kushamgaza ni kwamba Mkuu wa bandari (harbour Master) aliyeruhusu meli kung'oa nanga na kuanza safari ikiwa imejaza abiria na mizigo kupita kiasi bado hajakamatwa. Inasemekana ni mtoto wa kigogo mmoja wa serikali hii ya sasa au ile ya zamani.

  Aidha nahodha wa meli hiyo hajulikani hadi sasa aliko. Hili linawezekana kwani huenda ni kati ya wale waliofariki na mwili kutopatikana.
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Eti nini???!!!! This is a real b.f. country! Wanaanza kuficha mambo!
   
 5. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />
  hata sishangai.! Wangeweza hata kukanusha kwamba meli haijazama.!
   
 6. N

  Ngoiva Lewanga Senior Member

  #6
  Sep 12, 2011
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo ujue kuwa ni chakula cha vigogo. Kagoda part 2.
   
 7. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #7
  Sep 12, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Hilo jibu huwa wanatumia. Pale muhusika anapokuwa. Ni mwenzao.
   
 8. M

  Mwera JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwamujibu wa chanelten abiria waliokata niketi ni 1700,na mmiliki wa meli ni salum said batashi.
   
 9. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #9
  Sep 12, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Built in 1967 as Marianna for an unknown owner,she was later sold to Thelogos P Naftiliaki, Piraeus, Greece. In 1988, Marianna was sold to Apostolos Shipping and renamed Apostolos P. She was later sold to Saronikos Ferries and placed in service on the Piraeus - Aegina -Angistri route.
  In 2005, Apostolos P was registered to Hellenic Seaways. In 2007, she was sold to Makame Hasnuu, Zanzibar, Tanzania. and renamedSpice Islander I. On 25 September 2007, Spice Islander I was off the coast of Somalia when she experienced engine problems due to contaminated fuel. After the alarm had been raised via Kenya, USS Stout from Combined Task Force 150 was sent to her aid.The ship was on a voyage from Oman to Tanzania and was not carrying any passengers. USS James E. Williams also responded. Stout provide the ship with 7,800 US gallons (30,000 l; 6,500 imp gal) of fuel and supplied the ten crew with food and water. After her engines were restarted, she resumed her voyage to Tanzania.

  At 21:00 local time (19:00 UTC) Spice Islander I sailed from Unguja for Pemba Island. She was reported to have been carrying in excess of 800 passengers.Her capacity was 45 crew and 645 passengers.At around 01:00, (local time) on 10 September (23:00, 9 September UTC)Spice Islander I sank between Zanzibar and Pemba. Of those on board, 235 were rescued, with 40 of them suffering serious injuries. At least 200 people were killed.
   
 10. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #10
  Sep 12, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,287
  Likes Received: 22,047
  Trophy Points: 280
  Aibu kubwa sana, watu wazima kudanganya uwongo wa watoto. Hiyo meli mwenye nayo anajulikana, ila wanamlinda kwa maslahi yao ya KICHAMA
   
 11. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #11
  Sep 12, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  'kimjini mjini'
   
 12. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #12
  Sep 12, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Hata umaskini hawajui unatokana na nini....hii ndo tz, zaidi ya tuijuavyo
   
 13. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #13
  Sep 12, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,507
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  kwelui ukistaajabu ya musa ya tanzania ni kiboko.... Kodi wanachukua kwa kampuni hewa? hapo kweli hii selikali ni legelege....ndio maana hata ndege ilichukua wanyamapori bila wao kuiona wala kuchukua hatua yoyote.....
   
 14. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #14
  Sep 12, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,887
  Likes Received: 6,072
  Trophy Points: 280
  nimesikia mmoja anasema kutumia 'DNA' ...hivi itasaidia nini, kuwatambua wahanga!??? ili iweje!? Kawaida mambo yanajiendea na mtu anaona fahari kutangaza msaada wa milioni 300 wakati hata robo ya hiyo fedha ilitosha kusaidia tatizo kama hilo lisitokee. ...sijui ni laana!!!
   
 15. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #15
  Sep 12, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  waziri wa uchukuzi mpk muda anaulizwa swali hilo angetakiwa awe tayari ameshafahamu mambo mengi sana kuhusu hiyo meli... labda kama alikuwa amekesha Miss Tanzania!!
   
 16. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #16
  Sep 12, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hivi ni kweli mmiliki wa meli iliyopata ajali hajulikani? hii habari niliisikia asubuhi katika kipindi cha Nipashe cha Radio One Sterio ikimnukuu waziri Mohammed Aboud. Jee inawezekana inamilikiwa na kigogo mmoja wa CCM huko Zenji au huku bara?

  Aidha habari hiyo niliiona humu JF asubuhi iliyowekwa na mwanaJF mmoja lakini baadaye ilitoweka ghafla kabla sijaanza kuchangia na ingefaa kujuwa ni kwa nini?. Habri zilisema nahodgha pia hajulikani alipo ingawa kuna habari kuwa yeye na crew wenzake walijiokoa kwa kutumia boya na kwaacha abiria wengine wakihangaika.

  Aidha habari hizo ziliongeza kwa kusema kuwa mhandisi wa meli yuko mbaroni lakini harbaour master, aliyeruhusu meli kuondoka bandarini zanzibar huku ikiwa haijiwezi kwa uzito hajakamatwa, inasemekana ni mtoto wa kigogo huko Zenji.
   
 17. k

  kabombe JF-Expert Member

  #17
  Sep 12, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 15,578
  Likes Received: 8,518
  Trophy Points: 280
  HASNU MAKAME.Google utajua yeye na familia yake ni nani....hapo utajua kwa nini Sumatra ilipigwa zengwe isifike Zanzibar
   
 18. m

  mwana wa africa JF-Expert Member

  #18
  Sep 12, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 490
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  bahari yetu ni vilivyomo ndani yake havitunufaishi watanzania kama madini yetu yanavyowanufaisha watu wa nje. nina wasiwasi kuwa hiyo meli ina mkono wa kigogo ndani ya serikali ya jamhuri ndo maana serikali inajipanga itokeje katika sakata hili. maswali haya yanahitaji majibu ya kina kuwa meli hiyo iliingizwa nchini na nani na ilianza kufanya shuguli zake mwaka gani na kwa sasa wasimamizi wa meli hiyo ni kina nani?
   
 19. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #19
  Sep 12, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hawamjui mumiliki wa meli? Wewe unaongea kitu gani hapa? Mapato alikuwa anachukua mtu yeyote?
   
 20. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #20
  Sep 12, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ni Mzee Ruksa -- Ali Hassan Mwinyi -- ndiye mwenye share kubwa akiwemo Mwarabu mmoja anaitwa Batashi na wahindi flani. Na huyo Harbour Master ni mtoto wa Mzee Abood Jumbe ambaye tayari kasema hahusiki na ajali kwani hakuwa anaendesha yeye.
   
Loading...