Ajali ya Meli: SMZ yakataa misaada ya VODACOM

Apr 28, 2011
41
19
Tumepata taarifa kuwa Smz imekataa misaada ya Vodacom, na tunaambiwa ofisi za Vodacom znz ziko mashakani

Inaonekana kampeni ya kuisusia Voda imeshika moto, Mahmoud Thabit Kombo ndiye anayetumiwa na Vodacom kujaribu kuwaombea msamaha huko serikalini.

Vodacom wameahidi kutoa zaidi lakini taarifa zilizopo ni kuwa tayari bad publicity ishaspread na hata kama Vodacom wakiomba msamaha bado itakuwa ngumu kwa Serikali kujieleza kwa wananchi.

Wazanzibari waliopo UK (Zanzibar UK Trust na Friends of Zanzibar) wameamua kulalamika rasmi kwa ma trustees was Vodafone foundation UK.


Tutaendelea kuwahabarisha.
 
Inaelekea hatutumii "vichwa vya juu" tena kufikiri! Vodacom wamekosa nini?
 
SMZ wako sahihi kabisa kususia hiyo misaada ya Vodacom, ambao walikuwa wakiendesha mashindano ya miss "uchi" wakati nchi iko kwenye maafa, hayo ndio maamuzi magum licha wenzetu wako kwenye matatizo, pia pongezi za dhati zimfikie mh. Rais wa Zenji kwa kuonesha skills zake ktk kusolve issue ya kuokoa watu kupitia kamati husika
 
Wasiisusie tu, waachane nayo kabisa. Hii nchi kila mwenyenacho anafanya anavyotaka akidhani kuwa hakuna atakayemgusa.
Vodacom wakataliwe pia huku bara, tuhamasishane wote ili wajue thamani ya utu.
 
&lt;br /&gt;<br />
&lt;br /&gt;<br />
wasiisusie tu, waachane nayo kabisa. Hii nchi kila mwenyenacho anafanya anavyotaka akidhani kuwa hakuna atakayemgusa.<br />
Vodacom wakataliwe pia huku bara, tuhamasishane wote ili wajue thamani ya utu.

Wamekosea nini vodacom?
 
upumbavu katika rangi zake, kwani VODACOM ndio iliyoendesha ile meli hadi ikazama, kwani vodacom ndio waliruhusu meli ya mizigo ijaze abiria, kwani Vodacom ndio walipaswa kugawa lifejackets baada ya meli kutoboka, ujinga mwinge kwani VODACOM NDIO WALIOVUJISHA MAJI YAINGIE MELINI...HATUFIKIRI KWA KINA ...Tunawaza kipuuzi.

Mbona hawaituni TBC iliyopiga densi mchana kutwa, badala ya kuhabarisha WaTZ, mbona hatusikii wale wakaguzi wa meli kule pemba wamechulkuliwa hatua gani?

kwa serikali kujiingiza katika mgogoro huo ni kutowatendea haki Wawekezaji hao na ni uonezi usiokubalika, by the way aja;li imetokea Huko Znz kwa muda ule hakuna alijua kwa hakika ni janga kubwa kiasi katika siku ambayo Miss Tz ilifanyika
 
Kwa kuanzia mi napiga chini line ya voda na modem yao.
Mtu akiwa na line ya voda pia inabidi nifikirie kwanza kabla ya kumpigia!
 
Kuwasusia vodacom ni kuwaonea. Hata Zitto amenishangaza sana kuizima simu yake kisa eti anawaadhibu vodacom. Badala ya kujiuliza na kutafakari kwnn meli ya mizigo ibebe abiria tena kwa ujazo usiotakiwa tunawalaumu vodacom. Badala ya kumbana mkurugenzi wa bandari zanzibar kwa kuruhusu uozo wote huo bado tunawaonea vodacom. Ukichunguza kwa undani utagundua hata ile meli imezungukwa na ufisadi kuanzia ubora wake,mmiliki wake,uzembe wa sumatra kushindwa kazi yake n.k

Kwanini tusitazame chanzo cha tatizo kuliko kushadadia mambo yasiyoweza kutusaidia kutatua tatizo la uzembe wa serikali ya magamba juu ya usalama wa raia na mali zao
 
Wa-Tanzania na umasikini wetu, VODACOM dhihaka hizi za mmiliki wenu ROSTAM AZIZ hatuzitaki hata tone. Hongereni sana SMZ kwa kulinda heshima yetu kama taifa. Sina wasiwasi na judgement ya uongozi wa Rais Dr Ali Mohamed Shein.

Masikini na maiti yetu, VODACOM na utajiri wao hukoooooo mbali kabisaaaa!!!
 
.............Naunga mkono hoja,nadhani ni kati ya mambo machache ambayo nimekubaliana na wanzanzibar.....VODACOM wanapaswa wajifunze utu,kuendesha shindano la umalaya wakati tuna msiba mkubwa namna hii,sidhani kama ni haki...watu wenye hekima wanajua kuwa Miss Tanzania ni shindano la kutafuta wasichana wazuri watakao uzika kwa mapedeshee.....
 
Kwanza hakuna msiba wa kitaifa kwa mantiki ya Tanzania yaani Tanganyika na Zanzibar ndio maana huku Tanganyika shughuli zimeeendelea kama kawaida. CCM walipoulizwa mbona waliendelea na shamrashamra za uzinduzi wa kampeni igunga walisema bado maombolezo rasmi hayakuwa yametangazwa ndo maana walijimwaga kuzindua kampeni, i thouught tungewachukulia hawa serious zaidi kuliko makampuni ya watu binafsi. nadhani pia Vodacom hawaendeshi Miss tanzania bali wanadhamini!!!. hivyo basi tungegoma kutembelea blog zote ambazo walishiriki kunasa matukio ya miss tz ambapo zanzibar sio washiriki, tungegomea kusoma magazeti yote ambayo walikua bize kunasa tukio hili halafu tususie REDDS, tususie CFAO motors waliotoa Gari na other sponsors, tena tususie vituo vya televisheni ambavyo vilionyesha tukio hilo, tususie kukodisha ukumbi wa mlimani city. kama huu ndio ukomo wetu wa kufikiri kweli tuna uwezo mdogo sana wa kufikiri. aibu yetu kama hiki ndicho kinachotufanya tuitwe great thinkers. hahhahhahahaahhahah
 
Kama ni kweli. Basi wakatae misaada ya CCM kwa kuwa waliendelea na ufunguzi wa kampeni kule Igunga.
 
Kama ni kweli. Basi wakatae misaada ya CCM kwa kuwa waliendelea na ufunguzi wa kampeni kule Igunga.
ccm waliendelea na mbwembwe zao wakati wa msiba, alikua wakikata mauno kama nini kule Igunga , ni unafiki tu
292850_265340876820666_100000342668655_937397_1819611254_n.jpg
 
https://www.jamiiforums.com/members/mtoboasiri.html
Wajiandae ofisi zao kuchomwa moto

Sasa mbona sijasikia mkijiandaa kuchoma moto ofisi ya chombo chenu kinachohusika na usafiri wa majini? au ofisi za wizara inayohusika na usafiri wa majini? Kwa nini watu wa aina yenu huwa hamtaki kujinyooshea kidole wenyewe hata kama wenye makosa makubwa ni nyinyi wenyewe? kwani vodacom ndiyo wamesabisha vifo hivyo? aaaaah ZANZIBARIS ARE NARROW MINDED @$$H#^%$.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom