Ajali ya Meli: Serikali yetu na utata wa idadi ya abiria walioangamia

Mi binafsi siwezi kuita tukio hili kuwa ni ajali ajali ni nini kwanza ?wanasema hivi hawa jamaa "An accident or mishap is a specific, unpredictable, unusual and unintended external action which occurs in a particular time and place, with no apparent and deliberate cause but with marked effects. It implies a generally negative outcome which may have been avoided or prevented had circumstances leading up to the accident been recognized, and acted upon, prior to its occurrence."
Tukio la kuzama kwa hili dude ni la kizembe hivyo sio ajali kamwe HAKUNA AJALI INAYOTOKEA WATU WAKAANZA KUSALI SALA ZAO ZA MWISHO NA KUAGA NDUGU NA JAMAA ZAO ,zAIDI YA MASAA MANNE HII SI AJALI KABISA?

Tume itakayoundwa itatumia fedha za walipa kodi sisi na majibu yake hayatafanyiwa kazi kamwe
hawa watu wawajibike na si kulindana tu

Msiba umelikumba Taifa na haitabadili chochot kwa udogo au ukubwa wa msiba wenyewe ingawaje bado nina maswali juu ya idadi ya watu 3,000 - hapa kadiria mfano wa vikosi 3 - 4 vya jeshi ndani ya meli moja?

katika picha zinazowekwa najaribu kutafakari meli ya ukubwa huo, hata kama watu walisimama kama daladala.

Mi nadhani ifike wakati jamani tuandamane tu hata sisi wana JF maana haya mambo yanaudhi sana aisee na sintoacha kuyalipua tu.

Habari nzuri ila hilo la kuandama sikuelewi, yaani tuandamane kama JF??

with our user IDs au?? vipi kuhusu wengine wako mmoja au wawili manzini au quito, sasa hata wakiandamana kuna mtu atawatambua kweli??

aisee

Asante sana ndugu.. Nimeipenda habari hii na nimeisoma kwa kina. Hapa kuna maswali ya kujiuliza sana. Ila yote tumwachie mola.

Mkuu tumwachie mola ili iweje? hii haikubaliki popote pale bana lazima watu wawajibishwe kwa hili, kila janga linalotukuta sisi tunasema mapenzi ya mola

hamna cha mapenzi ya mola bana

Si rahisi kuthibitisha kama walikuwa 3000 kamili, lakini ni rahisi kuthibitisha idadi halisi yoyote kwani waliofariki na kuonekana, walionusurika na waliopotea ni watu ambao wana jamaa zao. Ni suala la kupita kila shehia (jina la kata kwa ZNZ) na kujua waliopotea, walionusurika na waliokufa na kuonekana.
Kutokana na takwimu zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini, idadi hiyo ni 2511. Kuna uwezekano wa kuwa watu 489 hawajaonekana ili kutimiza idadi ya 3000? Sielewi kama ambavyo serikali haielewi mmiliki wa meli.
Ulicho kisema kinawezekana zanzibar ingawa Tanganyika kilishindwa kufanyika mpaka leo hatujui idadi kamili ya waliokuwemo na waliokufa kwenye meli ya MV Bukoba...

Ajabu serekali kusifu sana vyombo
vya ulinzi na usalama kwa uokoaji wakti vyombo vilitoa mchango mkubwa sana katika juhudi ya uokozi. Sea Express na Azam Marine kwa kweli wanastahili pongezi za pekee. Both reacted fast to distress calls hence minimizing loss of life. Disaster management leaves a lot to be desired.

Mkuu tumwachie mola ili iweje? hii haikubaliki popote pale bana lazima watu wawajibishwe kwa hili, kila janga linalotukuta sisi tunasema mapenzi ya mola

hamna cha mapenzi ya mola bana
nakubaliana na wewe ndugu yangu. Hapa hakuna cha kumwachia mola.. Kuna watu tuwawajibishe..

Kuna watu wanadai kuwa idadi ya watu waliokuwa kwenye meli - Zanzibar ferry ilikuwa kubwa mara mbili hadi tatu ukilinganisha na idadi iliyotangazwa na serikali, haya ni ya kweli? Inasemekana wanaodai hivyo ni watu ambao walikuwa na tickets kwa ajili ya hiyo safari lakini walipoona watu wamejaa mno wakaahirisha. Mie sijui nimesikia, fanyeni uchunguzi.

Habari hii ni ya UONGO meli hii haikuzama kamaunavyotaka tumini MV Spice Islander ilipinduka na kuzama, kwahiyo hakukuwa na chance ya kupanda mlingoti, Source yako itakuwa imekudanganya

Wewe source yako itakuwa ni picha ya uongo iliyooneshwa na Mwananchi na ambayo hapa JF kama ni mfuatiliaji ilikwishalalamikiwa kuwa ni picha ya ajali iliyotokea Phillipines.Hii Spice mimi naijuwa na siyo hiyo iliyopinduka.Zaidi ni kuwa waliopiga simu wakasema wako juu ya mlingoti mimi binafsi nawajuwa.Namba zao nimezitoa hapa JF ili tusaidiane kuwatafuta na mpaka sasa ziko kimya.
Ukiwa na shaka nitakueleza zaidi MV spice ilivyozama.

Kupitia udanganyifu katika hii ajali napata picha ya udanganyifu katika kura.

Habari nzuri ila hilo la kuandama sikuelewi, yaani tuandamane kama JF??

with our user IDs au?? vipi kuhusu wengine wako mmoja au wawili manzini au quito, sasa hata wakiandamana kuna mtu atawatambua kweli??

aisee
mh hii kali sasa

Mi nadhani ifike wakati jamani tuandamane tu hata sisi wana JF maana haya mambo yanaudhi sana aisee na sintoacha kuyalipua tu.

Kama JF hatujakaa kimya, hadi sasa tunaandamana hapa kupitia KEYBOARD zetu!

Back
Top Bottom