Ajali ya Meli: Clouds FM na msaada wa maboya

nguvumali

JF-Expert Member
Sep 3, 2009
4,923
1,325
hiyo ni ishara kuwa taifa halina wafikiriaji wa kina, wakati kina mwanakijiji wakionya juu ya majanga hakuna aliejishughulisha, hawa clouds wanaendeleza utamaduni wa kinafiki, wakufikiri baada ya Tatizo, Unafiki a kujitafutia ujiko katika msiba kwa kutoa fedha nyingi, Je walikua wapi siku zoote wakati mgonjwa akiimwa kabla ya kufa....!
hao ni wanafiki tu
 
Opportunist wakuda sana hao. So magari yakianguka na kuua watu kwa kukosa mikanda watachangisha seat belts? PR ya kitoto hiyo. Wapeleke mabox ya condoms fiesta huko watasave thousands of lives
 
Hapa lazima tuangalia kwanini ajali ilitokea na tuone ni vipi tunaweza kufanya ili isitokee tena au kuwasaidia waliokumbwa na huu mkasa..

Sababu ya ajali kutoka ni kujaza sana boti.., na lazima watu wajue kwamba kila boti/meli ikitengenezwa na kuanza kazi inakuwa na maboya ya kutosha kutokana na idadi ya watu amabo wanatakiwa kuingia kwenye chombo.., hivyo basi kwa Clouds kuongezea hayo maboya ni kama kusema kwamba watu waendelee kujazwa kupita kiasi na hawa wa ziada ndio tuwape maboya...

Jambo la maana ni kuhakikisha vyombo husika vinasimamia ili kuepusha meli/boti kujaa (na wanaweza kufanya hivyo kwa kuongeza vyombo vingi vifanye kazi ili kuepusha msongamano) pia inabidi kusaidia vyombo vya kuokolea kuwa na vyombo vya kisasa vya kutosha kama Helicopter, boti n.k.

Hivyo Clouds cha kufanya ni eitheir kuwasaidia waliopatwa na maafa kwa hali na mali au kuwabana wahusika wawajibike ili kuacha kujaza vyombo..., hili la maboya ni good gesture lakini sidhani kama itasaidia tatizo (sio kwamba kuna uhaba wa maboya na kama mmiliki chombo atashindwa kununua maboya basi inabidi abadilishe aina ya biashara)
 
SWAHILI ORIGINAL WORLDWIDE
wapeni salaam zao , hao wanafiki tu, wanapenda kusikika na kutafuta huruma za wananchi na hapo wameona ndio wanapoweza kupata huruma kuwa wao ni sehemu ya jamii Damn
 
Kwa nini wasiwasaidie wahanga kwanza ili tuone kweli wanajali?sasa hizo life jacket wanazisaidia hizo kampuni na sio wanachi,POOR THINKERS.
 
Hapa lazima tuangalia kwanini ajali ilitokea na tuone ni vipi tunaweza kufanya ili isitokee tena au kuwasaidia waliokumbwa na huu mkasa..

Sababu ya ajali kutoka ni kujaza sana boti.., na lazima watu wajue kwamba kila boti/meli ikitengenezwa na kuanza kazi inakuwa na maboya ya kutosha kutokana na idadi ya watu amabo wanatakiwa kuingia kwenye chombo.., hivyo basi kwa Clouds kuongezea hayo maboya ni kama kusema kwamba watu waendelee kujazwa kupita kiasi na hawa wa ziada ndio tuwape maboya...

Jambo la maana ni kuhakikisha vyombo husika vinasimamia ili kuepusha meli/boti kujaa (na wanaweza kufanya hivyo kwa kuongeza vyombo vingi vifanye kazi ili kuepusha msongamano) pia inabidi kusaidia vyombo vya kuokolea kuwa na vyombo vya kisasa vya kutosha kama Helicopter, boti n.k.

Hivyo Clouds cha kufanya ni eitheir kuwasaidia waliopatwa na maafa kwa hali na mali au kuwabana wahusika wawajibike ili kuacha kujaza vyombo..., hili la maboya ni good gesture lakini sidhani kama itasaidia tatizo (sio kwamba kuna uhaba wa maboya na kama mmiliki chombo atashindwa kununua maboya basi inabidi abadilishe aina ya biashara)

Point taken

How comes mmiliki/clouds anashidwa kununua maboya ???

$20x10000=$200000
 
Point taken

How comes mmiliki/clouds anashidwa kununua maboya ???

$20x10000=$200000

Mkuu ukifanya shopping unapata life-jacket China kwa 2usd...

Light weight foam thickening type marine life jacket(LV09)

23 Similar from this Supplier1.waterproof oxford, highlight reflective belt
2.light wight inflatable foam
3.buoyancy >150N , for adults
4.size:S M L XL...

Min. Order: 200 Pieces
FOB Price: US $2.00-5.00 / Piece

Anyway point yangu ni Kwamba kwa kutoa hizi life-jackets elfu kumi wanamsaidia nani? (sababu mmiliki wa chombo.. boti/meli inabidi abanwe na ahakikishe kwamba kuna maboya ya kutosha ya wasafiri wote..., labda kama hizi extra jackets wapewe wale watu ambao watakuwa ni zaidi ya idadi inayotakiwa ili waingie nazo kwenye boti... ( na kwa kufanya hivyo Je haitakuwa kwamba unaruhusu meli kujazwa kupita capacity yake...?)

Point yangu ni kwamba huu msaada unamsaidia msafiri au unampunguzia mwenye chombo (meli /boti) kufanya kazi yake ya kuhakikisha kwamba kuna maboya ya kutosha...???

Au kila msafiri aanze kusafiri na Boya lake...!!
 
Sounds weird, nadhani tatizo kubwa ni kutokuwa na chombo cha uhakika na unafuu kutoka na kwenda Pemba. MV mapinduzi ilikuwepo enzi hizo na ilikuwa inasaidia sana, kwani kulikuwa na standards na ethics. Baada ya serikali ya mapinduzi kuiuza wakasahau kufanya replacement kitu kinacholeteleza wafanya biashara waroho wa fedha kuleta vyombo vyao substandard na kufanya biashara hiyo bila kufuata standards na ethics, hivyo kusababisha vyombo hivyo kujaa sana na kusababisha ajali kama hizo.

Mtu mwenye akili akitaka kupunguza maafa inabidi afikirie kununua meli kubwa na imara itakayokidhi mahitaji ya wananchi wa Pemba kama ambavyo waasisi wa mapinduzi walivyofikiria.

Kununua maboya 10,000 ni sawa na kusema ziwekwe ambulance nyingi kwenye blackspots barabarani, sidhanii kama busara inadictate hivyo.

No please.
 
My concern is who monitors hii misaada isije ikawa mingine inaishia mikononi mwa watu
Si unajua kufa kufaana,mwisho wa siku kuna haja ya kupata report ya idadi ya misaada na matumizi yake
 
m nkajua wanatangaza kwamba fiesta ijayo watajitahidi kusambaza na condom nyingi ili kuzuia maambukizi.................Ruge antaka sifa tu hlo wameliona leo
 
Clouds entertainment group kupitia mkurugenzi wa Ruge wametangaza mchakato wa kununua life jackets elfu kumi kwa ajili ya usalama wa vyombo vya usafiri majini. Huu ni mchango wao wa ajali ya meli Pembe katika kuzuia janga kama hili lisitokee tena. Hongereni Clouds..

Bongo bana mpaka watu wafe ndo misaada itolewe na wajanja wanaponea hapo hapo si tumeona Mbagala, Gongo la Mboto na Huko Moro.
 
Misaada ya goms sijui iliishia wapi!

Mama mkwe wangu aliishia kupata kilo 2 za maharage na Unga ndo basi tena huku kwenye luninga wanaonyesha flani katoa magunia ya mchele, mara mablanketi mara mashuka mara mafuta lakini inaishia kwa waratibu.
 
Nimewasikia eti wameanza kampeni ya kuchangisha fedha za kununulia maboya ya kwenye meli, hivi ni kweli mmefikiria vizuri kitu mnachoenda kufanya au ndo mnaendeleza lile wimbi la kukurupuka?? Je mnajua procedure zinazopitiwa mpaka meli kupewa kibali cha kupakia abiria??

Mmehoji kwa nini hiyo meli haikua na maboya ya kutosha na bado ikaendelea kufanya biashara?? au mnaogopa kuwahoji kwa sababu ya kuhofia kukichafua chama chenu?? Embu jaribuni kukuna kichwa kidogo mmajidhalilisha kwa kweli...
 
Back
Top Bottom