Ajali ya kizembe Tabata

jitukubwalao

Senior Member
Mar 29, 2011
194
161
Jioni hii ya Jumapili nimeshuhudia ajali ya kizembe sana, kuna jamaa alikuwa na kirikuu yupo mwendo kasi sana akanichonea kunipita mbele akakutana na semitrela jamaa akashika breki kwa ghafla gari akihama ikabiringita hadi mtaroni sijui hali yake ilikuwaje lakini kwa mzinga ule kama hakufunga mikanda atakuwa alitokea kwenye kioo cha mbele.

Wito madereva umakini ni kitu muhimu sana kama mbele huoni vizuri usilazimishe kumpita wa mbele yako. Pia mwendo kama huwezi kumudu gari tusikimbie hovyo
 
Madereva waBoda boda na kirikuu huwa nakaa najiuliza huwa wana haraka gani barabarani maana kwa kuchomekea wanaongoza!! Cha ajabu pamoja na ajali wazipatazo bado hawajifunzi
 
Ajali ni ajali tu.., huwezi jua labda alikuwa na msongo tu wa mawazo. By the way, it seems alikuudhi sana huyo jamaa alipokupita, na nahisi ili kumaliza hasira zako ukamkazia hadi sekunde ya mwisho alipokuwa hana pakupita ndio ikabidi akimbilie mtaroni. Na inaonekana roho yako imesuuzika kweli
Hahahah mkuu una maana jamaa anataamani kama vile aweke fensi barabara ili atumie pekee ake .

Hata hivo barabara ya mandela ina maroli mengi umakini unahitajika sana unapo ovateki
 
Mkuu inamana dereva mwenzio kapata ajali hata kushuka kumpa msaada tu wa Ari umeshindwa!!!! Ata kama ni uzembe ila sio fresh mkuu
 
Wewe ndo wale mnabania wenzio unakuta anawasha indiketa na honi anakupigia bado unakomaa tuu ..not fair
 
Tabia mbaya kabisa. Yaani mtu amepata ajali mbele yako badala ya kusimama utoe msaada wa kuokoa maisha yake wewe ukaona shauri yake ni bora uende zako. Shame on you.
Hahahahaaa mkuu unashangaa hilo dogo mimi juzi **** mtu aliungua moto hadi anateketea mimi nachukua video ili niisambaze clip whatsup au niitume huku uione?? Chezea smart phone ww siku hizi utakauta watu wanauwana wengne tunachukua video! Labda tu nilaumu uzembe wa mtoa post wa kupuuzia kuchukua vdeo!
 
Jioni hii ya Jumapili nimeshuhudia ajali ya kizembe sana, kuna jamaa alikuwa na kirikuu yupo mwendo kasi sana akanichonea kunipita mbele akakutana na semitrela jamaa akashika breki kwa ghafla gari akihama ikabiringita hadi mtaroni sijui hali yake ilikuwaje lakini kwa mzinga ule kama hakufunga mikanda atakuwa alitokea kwenye kioo cha mbele.

Wito madereva umakini ni kitu muhimu sana kama mbele huoni vizuri usilazimishe kumpita wa mbele yako. Pia mwendo kama huwezi kumudu gari tusikimbie hovyo
Nyinyi watu wa Dar muwe mnasaidiana.
 
Kuna siku niliendesha gari kama chiz kumwaisha jamaa hospital akiwa amezimia kwenye gari.... tangu wakati huo nikiona mtu anakimbiza gari nampisha maana hijui anawahi nini.... nilimfikisha TMJ and in 45mins akafa... ilikuwa mbaya sana kwangu...
 
Ajali ni ajali tu.., huwezi jua labda alikuwa na msongo tu wa mawazo. By the way, it seems alikuudhi sana huyo jamaa alipokupita, na nahisi ili kumaliza hasira zako ukamkazia hadi sekunde ya mwisho alipokuwa hana pakupita ndio ikabidi akimbilie mtaroni. Na inaonekana roho yako imesuuzika kweli

We unaleta utani hapa, lakini ukweli wa mambo watu upata ajali za kizembe kwa kukosa common sense - wewe unakuta gari zimesimama taa za nyuma zinaonyesha kwamba zimeshika breki - wewe unatoka nyuma kwa kasi unataka kuzipita ujui kama kuna semitrailer mbele au train au ajali - unajikuta unakwenda kujibamiza!

Siku moja niliwahi kufuatana na mama wa Kichina Barabara ya Nyerere tunakuja mjini, kila mtu akiendesha gari lake - mimi nilimtangulia yeye akanifuata kwa gari lake alikuwa nyuma yangu tumetenganishwa magari mawili, tulipo fika karibu na kituo cha Gerezani tukasimamishwa kwa bendera nyekundu ya msimamizi wa rail crossing, kumbe train ilikuwa inakatiza pale kwenda Bara, yule mama akatu overtake wote kwa kasi bila ya kutafakali kwa nini sisi tulio mtangulia tume simama - gari lake lilikoswa koswa kugongwa na train kimiujiza!!

Nilipo muhoji kwa nini alitu overtake wakati aliona wazi wazi magari yote yame simama - alikosa jibu nilimkuta akitetemeka kwenye gari lake! CHUNGA SANA.
 
Tabia mbaya kabisa. Yaani mtu amepata ajali mbele yako badala ya kusimama utoe msaada wa kuokoa maisha yake wewe ukaona shauri yake ni bora uende zako. Shame on you.
hata kama ningekuwa mimi wala nisingemsaidia,barabarani kuna watu wana akili mbovu sana,ajali ndio dawa yao siku nyingne wajifunze
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom