Ajali ya Gari Karatu Arusha: Coaster yaua Wanafunzi na walimu wa Lucky Vincent (karibu wote)

mimi najifanya jasiri kwenye misiba lakini mama praise na baba rebeca wamenifanya nimelia kwa kweli....
yaani mama anasema mwanangu kwa nini usingekuja mount meru nikutundikie drip, mimi ni nurse naokoa maisha ya wengine nishindwe wewe mwanangu!!
ooh my God!! watie nguvu wazazi wale
Aiseee
 
mimi pia nimejitahidi sana kutokuangalia hizi picha maana moyo unahamia mgongoni, ikija wasap yyt nikiona ina dalili ya kuwa na picha za wtt wetu wapendwa nazifuta haraka sana,,
Kweli mkuu sina picha zao kabisa
 
Unadhani ni kwa nini huwa tunakumbushia kuzaliwa na kufa kwa yesu
Ya Yesu ni tofauti.

Inawapa Wakristo matumaini mapya kutokana na kufa na kufufuka kwake

Hii hapa zaidi ya kukumbushia majonzi sioni mantiki.
 
Ya Yesu ni tofauti.

Inawapa Wakristo matumaini mapya kutokana na kufa na kufufuka kwake

Hii hapa zaidi ya kukumbushia majonzi sioni mantiki.
Hii itawakubusha wazazi,wamiliki wa shule na vyombo moto,madereva pia kuwa makini wawapo barabarani ili isije kujirudia May 06 2017) nyingine
 
Nimepata habari isiyo na shaka kuwa gari aina ya coaster limeua watoto karibu wote waliokuwa wanaelekea mjini Karatu kwa ziara ya kimasomo including(joint examinations), taarifa zinasema wamebaki watoto(3) tu wengine wamefariki,

shule inaitwa Lucky Vincent Nursery & Primary School ipo Arusha ni medium schools,kwa wenye updates tunaomba mtupe
.............
UPDATES:Ajali imetokea mlima marera kijiji cha rhotia,km chache sana kutoka Karatu mjini,mlima huo una mteremko mkali na daraja na pia kulikuwa na ukungu

Picha: Soon nitaziapload ni ajali ya muda huu
Mungu awalaze mahali pema peponi
----------------------

UPDATE: Coaster inasadikiwa kuwa na zaidi ya abiria 30 na wote wanasadikiwa wamefariki,maiti zimepelekwa hospitalini na watu wameondoka eneo la tukio,mvua inanyesha

UPDATE: Picha zinakuja soon ripota yuko eneo la tukio..

19a4fcd1c935e4c031670cd880a46bc5.jpg

.........................
UPDATES:Magari ya polisi yametanda kila kona na maiti zimebebwa na magari ya polisi
Tayari kuhifadhiwa
...................
UPDATES:Ni watoto watatu (3) wanasadikiwa wako hai ila wako mahututi kabisa na kuna wasiwasi vifo vikaongezeka
UPDATES:Lucky vincent nursery school bus
62d62ef75dec257e496254f5cfb2808e.jpg

UPDATES:Shughuli za uokozi
a198eaa3cab45eec73b51943888b0a63.jpg

UPDATES:Gari lilikuwa na zaidi ya abiria 30 wanafunzi 25,waalimu (4) wote wa kiume na dereva 1
................
UPDATES:Kati ya majeruhi watoto watatu(3) wawili wako mahututi kabisa na mmoja amepasuka kichwa
................
UPDATES:Maajabu ya ajali hakuna damu zozote zilizotapakaa licha ya watu wengi sana kufa!
..................
UPDATES:Majeruhi mmoja kati ya( 3) amefariki kabla ya kufikishwa hospitali,kwa hiyo taarifa zinasema wamebaki majeruhi wawili walioko ICU
...............
UPDATES:Kuna mkanganyiko mwingi kuhusu chanzo cha ajali ila nature ya eneo la ajali ni mteremko mkali na kuna daraja,ni eneo ambalo dereva anatakiwa kuwa makini kabisa,kwa dareva asiyemwangalifu inaweza tokea lolote,hebu angalia hapo gari lilipotumbukia na haikuwa ina over take ,u can diagnose the nature of an accident
efc42e9814d84a123b6aa5a8a92fed7c.jpg

UPDATES:Mwonekano wa gari kwa mbele baada ya kupata ajali
1b9b2ef92a5648b20c71d3e04a5e5f65.jpg

UPDATES:RPC Wa arusha amethibitisha jumla ya vifo 31 vya waalimu na wanafunzi
...................
UPDATES:Taarifa kutoka mjini Karatu zinasema kuwa majeruhi hali zao ni mbaya zaidi na wanakimbizwa hispitali ya rufaa ila mtoto mmoja ni mzima
6d688744c79e95ed10fb0d0ea09e695e.jpg

...............

UPDATES:Mtoto pekee alienusurika amesimulia chanzo cha ajali na amesema kuwa gari lilifeli break tokea mwanzo wa kushuka mlima hali iliyopelekea watoto na waalimu kupiga makelele na kilichofuata ni gari kupaa na kupinduka kwani nature yake sio slope kivile kuna miinuko kidogo

My take:Kulingana na maelezo hayo inaonekana gari lilifeli break,kupoteza mwelekeo na kupinduka ingawa bado polisi hawajatoa taarifa za chanzo cha ajali Bali walitaja idadi ya vifo 31 tu
...............
UPDATES:Majina ya waliofariki
470862a5c10126e56155ee706126acdd.jpg

fbf2939173eaa07ff41af774c40b5eed.jpg


MUNGU AWALINDE NA KUWAREHEMU ITS SO SAD
d60caf7575f56820b6c8c35459ed5a35.jpg


R.I.P all

Client:Jf member
Poleni ndugu zetu wa huko Ntwara
 
Back
Top Bottom