kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 268
WATU 24 wamekufa papo hapo na wengine 56 wamejeruhiwa katika ajali ya basi la AM iliyotokea jana jioni eneo la mpaka kati ya Nzega na Igunga mkoani Tabora.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa 10: 15 jioni katika vijiji vya Kitangili na Migua baada ya basi aina ya Scania lililokuwa likitoka Arusha kwenda Mwanza kupinduka.
Waliokufa ni wanaume 14, wanawake sita na watoto wanne huku majeruhi ni wanaume 35, wanawake kumi na watoto 7 majeruhi wanne wamepelekwa katika Hospitali ya Bugando mkoani Mwanza kwa matibabu zaidi.
Mganga wa wilaya ya Nzega, Dk John Mwombeki alisema maiti pamoja na majeruhi hao wapo katika hospitali ya Nzega.