Ajali ya basi yaua raia wa Kenya, wanane wajeruhiwa

Bishop Hiluka

Verified Member
Aug 12, 2011
6,478
2,000
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Naibu Kamishina wa Polisi, Ferdinand Mtui amemtaja marehemu kuwa ni Edwin Samba, Mhandisi raia wa Kenya, mkazi wa Kakamega aliyekuwa akisafiri kutoka Arusha kuelekea Burundi.

Ajali hiyo ilitokea jana jioni katika Kijiji cha Busunzu wilayani Kibondo katika Mkoa wa Kigoma. Basi lililohusika na ajali hiyo ni NBS lenye namba za usajili T 185 AGB lililokuwa likiendeshwa na dereva Hamisi Chora ambaye alikimbia baada ya ajali.

Eneo ambalo ajali imetokea lina kona kali na wakati wa kiangazi kama huu kunakuwa na vumbi, hivyo inasemekana dereva alishindwa kudhibiti gari katika kona hiyo kutokana na mwendo mkali…
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom