Ajali ya Basi la Dar Express Kibaha

Ukwaju

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
13,370
11,088
Kumetokea ajali saa 11:30 ya basi la Dar express picha ya ndege Kibaha linaloingia Dar jioni hii na Semi ya mafuta na imetokea upande wa kulia nje ya barabara namaanusha basi lilitoka nje ya sight yake
Pole majeruhi na tuombeane salama na mie pia nipo barabarani
Wenye Updates mtujuze

Basi MUNGU ashukuriwe km hakukutokea majeruhi mpaka sasa na washukuriwe waliofuhabarisha kuwa chanzo ni pikipiki (Bodaboda) iliyokatiza
attachment.php
 

Attachments

  • ajali.jpg
    ajali.jpg
    21.4 KB · Views: 3,854
Poleni sana majeruhi.
Hizi taarifa sasa zimekuwa nyingi sana, kwa siku hazipungui tatu.
Tutaendelea kutolewa kafara mpaka lini? Nani awajibike kwa hilo?
 
Mtoa roho sasa amehamia barabarani, wiki chache zilizopita alikuwa kwenye kuangusha majumba, Dar, Bangladesh, India na china. pamoja na watu kujiangusha maghorofani. baadae atahamia kwenye maji na angani
 
Poleni Mkuu na wote mliopata majeraha Mungu awawezeshe mfke salama,hii ni ajali ya tatu kama sijakosea kwa leo,mbeya,kibaha na nilioshuhudia leo asubuhi maeneo ya magomeni.
 
Ndio nimepita hapo kama dakika tano baada ya ajali but seems Dereva WA basi alikua anamkwepa mwendesha pikipiki aliengia barabarani ghafla. Lile tanker lilikua liko bondeni linaoshwa. Pikipiki iko chini kwenye lami
 
Ndio nimepita hapo kama dakika tano baada ya ajali but seems Dereva WA basi alikua anamkwepa mwendesha pikipiki aliengia barabarani ghafla. Lile tanker lilikua liko bondeni linaoshwa. Pikipiki iko chini kwenye lami

Vipi wote wote wametoka salama?
 
Jaman nini tena Tanzania mbona ajali za mabasi na maloli zimezidi kuwa nyng sana aisee tatzo ni nini jaman
 
Dah!! hayo maeneo ya kuanzia TANITA, Kwa Mbonde, Picha ya Ndege hadi huku TAMCO huwa ni sehemu mbaya na hatarishi...ajali nyingi hutokea hilo eneo...
 
Jaman nini tena Tanzania mbona ajali za mabasi na maloli zimezidi kuwa nyng sana aisee tatzo ni nini jaman

Tatizo ni pamoja na madereva kutokuzingatia sheria za Usalama barabarani.
Hebu angalia picha hizi alafu niambie kama ajali nyingine kama si za kujitakia wenyewe!


a1.jpg


Madereva ku-ovateki kwenye Kona/Milima na tena kuovateki gari zaidi ya moja!

accident.jpg


IMG_1679.jpg


Uendeshaji+huu+ni+hatari+ni+moja+ya+basi+la+kwenda+Mikoani+lilitaka+kulipita+Lori+kwenye+kona+bila+kuchukua+tahadhari..JPG


12.jpg
MUREFU
 
Nimepita pia ajali mbaya ya basi na Lori mkoani Tanga Barbara ya segera chalinze
 
Haujaweka wazi mdau


attachment.php

Mkuu uwazi wenyewe ni kuwa hapo Picha ya ndege kulikuwa na Semi la Tanki la mafuta likioshwa bondeni
Dar-Express ilikuwa ikitokea maeneo ya Chalinze kwenda Dar ikakutana na Bodaboda iliyokatiza sasa dereva alipojaribu kumkwepa akatoka nje ya barabara upande wake wa kulia na kuligonga lori hilo
Idadi ya majeruhi bado hatujaipata
 
Na nani? Kwanza ukiwakagua kwenye makoti yao wamejaza viroba, bodaboda ni janga la kitaifa afadhali hata ukimwi kuliko pikpik
Dereva wa boda boda wawe wanapimwa kilevi.
 
We acha tu siku hizi ukisafiri ukifika na kurudi salama lazima umshukuru mungu because magari yanavyokimbizana barabara kuu inatisha. Pole sana majeruhi wa dar express.
 
Na nani? Kwanza ukiwakagua kwenye makoti yao wamejaza viroba, bodaboda ni janga la kitaifa afadhali hata ukimwi kuliko pikpik

Umeona hilo janga tu maderava wa boda boda wanavunja sana ndoa za watu, wanawake wako penda sana dereva wa boda boda
 
  • Thanks
Reactions: ram
Back
Top Bottom