Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,280
- 25,858
Kilichotokea Arusha kimeshatokea. Majonzi yametupata kama taifa kwa kupoteza nguvu kazi na watanzania wenzetu waliokuwa kwenye uga wa elimu kwa maendeleo ya taifa letu pendwa. Tunamshukuru Mungu kwa kila jambo lililotukuta na tunapaswa kusonga mbele kama taifa imara na wamoja zaidi.
Lakini, tukio la Arusha linapaswa kutupa mafunzo. Kama wazazi, walimu, wanafunzi, wasafirishaji, watumiaji wa vyombo vya moto na washika dau wa elimu, tuna jambo moja au lingine la kujifunza. Tukio la Arusha linatufunza nini katika hasa usafirishaji wa watoto/wanafunzi na kwa kuzingatia miundombinu yetu?
Tukio la Arusha linatuachia mabadiliko gani katika sheria zihusuzo usafirishaji na kadhalika? Kama watanzania tunapaswa kujadiliana na kukubaliana juu ya nini cha kufanya, kama funzo, kutoka kwenye ajali ya Arusha iliyopoteza maisha ya wapendwa wetu wanafunzi, walimu na dereva (jumla wakiwa 35) wa Lucky Vicent