Ajali ya aina yake iliyoniacha kinywa wazi kwa sekunde nyingi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajali ya aina yake iliyoniacha kinywa wazi kwa sekunde nyingi.

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by cheusimangala, May 3, 2012.

 1. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2012
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Asalam aleykum.

  Mashosti ajali hii inayotuhusu kina mama imetokea hapa kwenye airport kubwa kuliko zote ulaya magharibi ambako niko transit kwa muda sasa nikisubiri boarding time kuelekea kwenye my last destination.


  Katika kupoteza muda bila kusinzia uwanjani hapa niliamua kutembea tembea sehemu mbalimbali zilizoko ndani ya uwanja huu mkubwa na wenye kuvutia.Nimekua naingia kutoka duka moja na kuingia jengine.Nikiwa natoka ndani ya duka fulani la designer mkubwa wa kiitaliano huku nikiwa naelekea kwenye zile ngazi za umeme ili zinifikishe ilipo internet cafe hii ambayo ndimo ninamorusha uzi huu,kwa mbele yangu nilimuona dada fulani aki-srutt kwa madaha juu ya high heels ambayo ina kama inchi saba hivi na yeye akielekea zilimo hizo ngazi.Nikiwa nyuma ya mdada pua zangu ziliweza kufaidi harufu nzuri ya manukato ya bei ya gharama aliyojipulizia mdada huyu,kwa kweli kuanzia kichwani hadi miguuni mdada alivaa vitu vya gharama tuu,nilizipenda nywele zake ndefu nyeusi zenye mawimbi yaliyomwagika hadi mgongoni,ngozi yake nyeusi ilikua nzuri na laini kuonyesha kwamba ilikua ikihudumiwa kwa body cream/lotion za gharama ,kwakifupi mdada alikua kwenye class ya nyota tano.

  Macho yangu yalivutiwa na hizo high heels alizokua amezivaa,moyo wangu ulivipenda hivyo viatu,nikajiapiza kuwa nikijua vinapouzwal azima nivinunue japo vilionekana ni vya ghali sana.Hapa nikajiambia sijui nitapataje mwanya wa kumuuliza huyu mdada aliponunua hivyo viatu vyake.

  Basi tukafika kwenye ngazi mdada akawa wa kwanza kupanda mim nikawa nyuma yake na watu wengine wengi tu pia walikuwepo,wote wakiwa wazungu isipokua mim na huyu mdada tu ndio tulikua weusi.
  Ngazi ikawa ikitushusha taratiibu huku yule mdada akiwa amepouzi kwa mapozi yanayoonesha kuwa alijua amependeza na kweli mdada alikua kapendeza hata sura yake ilikua ni nzuri japo hainifikii yangu,pia dada alionesha kuwa ni mdada mwenye kujiamini.

  Tulipofika chini dada akaanza kunyanyua mguu wake wa chupa ya bia kwa madaha kwa lengo la kutoka kwenye ngazi hizo lakini maskini ya mungu sijui ilikuaje mdada akateleza na kudondoka na kulalia mgongo kitendo kilichofanya yesuuuu initoke.Mara moja kuna mtu akabonyeza kitufe cha kuzima hizo ngazi ziache kuzunguka,na ziliposimama mama mmoja wa kizungu akampa mdada mkono kwa lengo la kumsaidia kunyanyuka lakini mdada aliponyanyuka wazungu woote waliokuwepo pale pamoja na mim cheusie tulijikuta tukibaki midomo wazi huku kauli zikiwa zimetukatika kwa sekunde nyingi,sikuamini nilichokiona,kumbe mdada yule aliyekua mrembo but not now any more alikua kavaa wigi,sasa alipodondoka wigi lake likanasa kwenye zile ngazi na aliposaidiwa kunyanyuka wigi likabaki pale chini ndo sasa kila mtu aliyeko pale akashuhudia kichwa chake halisi kilivyo,yaani yule mdada nywele zake zilikua ni chafu zinanuka uvundo,juu juu ya nywele kulikua na maukoko kama magamba ya vidondo,uwiiii,huko kichwani kulikia kuna kama mauzi mauzi ya mablanketi,kuna upande alikua kasuka mabutu ,upande kasuka mistari kuna upande hajasuka kuna sehemu hakuna nywele zimenyonyoka kama wale watoto wanaokuwaga na yale sijui ndo yanaitwa mapunye sijui mashilingi,kumbe lile wigi lilikua limeficha mengi,dada ana uchogo balaa halafu kichwa chenyewe kidogo ka ngogwe halafu kwa mbele ana komwe sasa,yaani kwaharaka utadhani yule I.T .

  Wanaume wote waliokua wakimkodolea macho hapo mwanzo sikujua waliondoka saa ngapi,mdada alikua anaona aibu,yale mapozi ya najua nimependeza na ya kujiamini yakayeyuka.Wazungu wote wakakaa pembeni wakimshangaa nikabaki mim na mdada na mim nikataka kuondoka maana wazungu walikua wanaangalia kichwa cha mdada halafu wanaangalia lile wigi lililonasa pale chini halafu wanangalia kichwani kwangu nikasema hapa lazima nisepe ila nikakumbuka kuwa nataka anambie alinunua wapi viatu vyake hivyo nikasema huu ndo wakati wakujua.

  Nikajifanya kauzu,nikainama pale chini nikajaribu kuvuta lile wigi halikuchomoka,nikamuuliza do you speak english?Akanambaia kwa kishwahili,ndio ila na mim naongea kiswahili,nikamwambia umejuaje kuwa mim naongea kishwahili akasema nimekusikia ukisema yesuuuu,basi nikamwambia abonyeze pale yule mtu alipobonyeza ili ngazi ziwake labda wigi lake litachomoka.Anyway,kwa kifupi nimefanikiwa kumchomolea wigi lake akalivaa haraka haraka nakuondoka ila nimeshajua viatu vyake vinauzwa wapi na pia nimejua ni mtanzania mwenzangu.

  Haya mim nawarushia huu uzi labda kuna chochote kina dada wenzangu mtakua mmjejifunza,nikisharusha huu uzi naenda kutafuta vile viatu maana yule mdada kasema hilo duka hata humu ndani lipo,baada ya hapo muda si mrefu nitakuwa on board.Sitaweza kucoment lolote kwa sasa ila nikifika niendako na kupumzika nitakuja kuwacheki.

  Nitakieni safari njema.
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Ghafla moja hiyo mmesikia uvundo?!

  Nshushe dada
   
 3. Egyps-women

  Egyps-women JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2012
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 499
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hhahaha nicheke kwa sauti:smile-big:
   
 4. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Very true, mwanzo nilifikiri ni kweli lakini hadithi ilivoendelea mhhhhhhhh........
   
 5. queenkami

  queenkami JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2012
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  hahahaa cheusi hii kali ya mwaka.Kusema kweli wadada wengi wanaficha uchafu ndani ya mawigi,sio wote lakini nimesema baadhi.Safari njema.
   
 6. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Duh . . . .
   
 7. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2012
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Enheee bibi wee Gaijin kwani kiforensic forensic huwa inachukua muda gani kwa harufu ya uvundo kusikika?Maana sie ghafla tulisikia uvundo ukinuka wewe waona ajabu,ilitaka uchukue siku nzima ndo usikike au? maana umechekecha nyuma na mbele kutafuta kitu kisicho cha kawaida as if uko lab. ukisolve murder case.
  Eti "nshushe dada" kwani mim ndo nlo kupandisha au umedandia mwenyewe,utajishusha mwenyewe kama ulivyojipandisha.
  Tutaendelea kuongea nikifika muda wangu wakuboard tayari.
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  May 3, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,406
  Trophy Points: 280
  Kama Mwanahawa Chipolopolo vile!
   
 9. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #9
  May 3, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #10
  May 3, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,431
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  mawigi yana mambo jamani ... acheni tu...
   
 11. Angel Nylon

  Angel Nylon JF-Expert Member

  #11
  May 3, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 4,471
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  Sijui kwa nn w'ke hatupendi kuwa natural jamani.
  Mi sijawahi eka manywele ya ajabu wala sitawahi.
   
 12. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #12
  May 3, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Mhhhhhhhhh........
   
 13. Mchochezi

  Mchochezi JF-Expert Member

  #13
  May 3, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 6,952
  Likes Received: 1,155
  Trophy Points: 280
  mazungumzooooooo baada ya habariiiii
   
 14. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #14
  May 3, 2012
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ushafika? We umepanda fisi ama ungo?
   
 15. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #15
  May 3, 2012
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  cheka tu shosti wangu wala sikulaumu mi nimecheka nilivyofika home Egyps-women
  Asante kwa kuniwish safari njema malkia,ni kali zaidi hasa kama ungekuwepo pale kushuhudia kwa macho yako
  acha tu dogo yaani uanawake kazi ila huyu mwenzetu ni mchafu Smile
  ndo hivyo si unaona kina lulu wanavaa mawigi yenye rangi rangi kama za tausi lkn unaonaje wanavyogombewa na wanaume tena vigogo.Hongera Angel Nylon unatural ndo wenyewe.
  Nishafika Eeka Mangi wewe shukuru ndugu yako nimefika salama haya ya fisi,punda,ungo bajaji au mshikaki wa bodaboda tuyaweke pembeni.Unataka zawadi?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #16
  May 3, 2012
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mashosti ndo nimefika,hapa inabidi nikajaze maji kwenye bath tab nijiloweke kwa muda ili kuondoa uchovu uchovu wa safari.
   
 17. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #17
  May 4, 2012
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Pole na safari Cheusimangala. Naskia eti ndege yako imeanguka Mbeya ulizidisha zawadi nini. Punguza baadhi si utaenda siku ingine bana. Naskia Mbeya wabaya kwa hizi ndege za private!
   
 18. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #18
  May 4, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Naona mko wawili hivyo ndege kuzidiwa uzito wenu na mizigo yenu si ajbu.
   
 19. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #19
  May 4, 2012
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  hehehee asante mkuu,tena kakijana kenyewe kalikonitungua nimekafundisha huu utaalam mim mwenyewe lakini ngoja nipumzike Eeka Mangi nitakaonesha nani ticha nani denti.
  Huyu nilimpa lifti na hadi namshusha hapakutokea tatizo lolote TaiJike labda kama alinifanyizia baada ya kutua ardhini,
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...