AJALI: Watu sita wapoteza maisha, saba wajeruhiwa wilayani Lushoto

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,669
WATU sita wamepoteza maisha na wengine saba kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wamepanda aina ya Canter lenye namba za usajili T 634 ADF lililokuwa likitokea mnadani Mlalo kwenda Soni.

Gari hilo lilipata ajali baada kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha Mgaro Kata ya Mgaro Tarafa ya Mlalo wilayani Lushoto.

Waliofariki katika ajali hiyo kwa mujibu wa kamanda ni Jamali Hemedi, Khadija Saidi, Zuena Juma, Husna Athumani, Nusura Seif na Hassan Rashid.

Aidha, waliojeruhiwa wametajwa kuwa ni Seif Bakari, Sauda Shemtui, Mwanahamis Ayoub, Abeid Ayoub, Khalifa Juma, Mariam Kassim na Mwanamvua Yusuph.

Kamishna Mwandamizi wa Polisi, Benedict Wakulyamba ambaye ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, na ameeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva kupita kwenye mlima mkali wenye utelezi ulionyeshewa mvua.
16997919_402096476815338_2764274723769516250_n.jpg
16939122_402096626815323_6948505303449180710_n.jpg
16938697_1650231541946429_7542488203629513864_n.jpg
16996397_1650231511946432_7562171153671506996_n.jpg
16939252_1650231498613100_4625792617318932898_n.jpg
 
Pole sana kwa Walio fiwa...ila njia za kama Lushoto na kwingne kwenye milima&kona kali znahitajika uangalizi wa karibu sana.! Saa zngine watu wanapanda magari yaliyobeba makabichi na viazi wanasafiria na pia huwa madereva wa coaster na baadhi ya mabasi wanaendesha kwa spidi wanapokuwa wanapanda na kushuka lushoto utadhani wapo ENSURED kufika salama.!wawe makini tunapoteza NGUVU KAZI ya kujenga taifa kwa mizaha yao
 
Poleni kwa wafiwa poleni kwa majeruhi....

Wana Mng'aro Mlalo na Lushoto kwa Ujumla.

Rai yangu kuhusu madereva wanatumia njia ya Mlalo-Mng'aro kuwa makini saana na hii njia pia vyombo vya usalama kusimamia taratibu za kiusalama
 
Back
Top Bottom