AJALI: Treni ya abiria kutoka Tabora kwenda Kigoma imeanguka huko Uvinza. Taarifa zilizopo watu watatu wamejeruhiwa

Mafundi wa reli wakisikia njaa tu matukio yanatokezea.

Poleni kwa ajali tunashukuru Mungu kusikia mmenusurika wote.

Uwanja wa ndege wa kimataifa wa chattoh ukimalizika tutarudi kutazama hii reli kwa ukaribu. Kwa sasa mtuache kwanza tushughukie uwanja ule ni muhimu kuliko hii reli ya kizamani . Chattoh mpya yaja
 
Vipi vikosi vya uokozi vimefika eneo la ajali kwa wakati..

Vipi wahanga wamepata matibabu ya awali na huduma nyingine za muhimu kama maji ,chakula ,madawa na mablanketi..ajili ya kujistiri..

Na suala la usalama liko vizuri..
Wasije tokea watu wakutumia huo mwanya kufanya mambo tofauti badala ya kuwasaidia wahanga..
 
Tungeimarisha zaidi reli maana train inapita tu labda kama zimegongana hapo tutalaumu station master.

Lakini tatizo ni RELI miundimbinu mibovu lazima magenge yarudi na wafanyakazi wa railway wale labours walikuwa wanafanya kazi kwa kujituma haswa maana wakati ule unakunywa chai hata hutikisiki kwa sababu reli ilikuwa imeshindiliwa haswa na kokoto.

Wa kumwajibisha sijui lakini shirika lijipange tatizo linajulikana haiwezekani umo kwenye train unarukaruka kama bisi
 
IMG-20180228-WA0015.jpg
IMG-20180228-WA0016.jpg


AJALI YA TRENI KIGOMA: Treni ya abiria ya Shirika la Reli Tanzania iliyokuwa ikitokea mkoani Dodoma kwenda Kigoma imepata ajali katika eneo la Kijiji cha Mpeta wilayani Uvinza.

Ajali hiyo imesababishwa na kichwa cha treni kuacha njia na kusababisha mabehewa mawili kuanguka katika dimbwi dogo la maji.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Othieno hadi sasa hakuna taarifa za kutokea kwa vifo wala idadi ya majeruhi.

Behewa kadhaa bado zimesalia kwenye njia yake baada ya ajali.

Azam 2
 
Hapa habari ya mauaji na maandamano..

Poleni sana wafiwa ila uchunguzi ni muhimu sana hapa( I am curious)
 
Usifike huko ndugu vyama ni itikadi tu, huwezi kuombea wenzio wafe kisa mnatofautiana vyama

Hiyo kauli ilifaa zamani ,kwasasa siasa ni uadui ndo maana jela wamejaa chadema tupu ,wanaokufa ni chadema tupu ,halafu niwapende ccm kwa lipi ?
 
Back
Top Bottom