Ajali tena Tabora!

Zyansiku

Member
Jul 27, 2009
49
10
Ikiwa ni ndani ya wiki moja Mkoa wa Tabora kukumbwa na ajali mbaya za vyombo vya usafiri( Bus) Basi lililoua watu zaidi ya 24 mwanzoni mwa wiki hii wilayani Nzega A.M coach dakika chache zilizopita Basi jingine la kampuni hiyo limepata ajali mbaya ambapo watu watatu wamefariki papo hapo! ajali hiyo imetokea nje kidogo ya mji wa Tabora kama km 15 hivi kwenye kijiji cha kazima ambapo pia kuna bwawa kubwa la maji lijulikanalo Bwawa la kazima.
kwa kuwa ajali imetokea muda mfupi uliopita nitawapa habari zaidi baadaye
 
Dah! haya maajali..........
Poleni ndugu wote mliokumbwa katika huu mkasa
 
Same region, same company......what a coincidence!!! poleni sana wafiwa. tatizo mabasi mabovu na madereva wabovu
 
halafu madereva wa yale mabasi ni vijana wadogowadogo wanafanyiana sifa njiani, dereva anaendesha basi huku anatafuna mirungi na kupokea simu mara kwa mara na sisi abiria tunakuwa tunawaangalia...mara nyingine sisi wenyewe tunachangia...poleni sana mliopata ajali
 
Mwendo kasi na ubovu wa magari + madereva, poleni wote mliofikwa na msiba. RIP marehemu wote.
 
halafu madereva wa yale mabasi ni vijana wadogowadogo wanafanyiana sifa njiani, dereva anaendesha basi huku anatafuna mirungi na kupokea simu mara kwa mara na sisi abiria tunakuwa tunawaangalia...mara nyingine sisi wenyewe tunachangia...poleni sana mliopata ajali
Haya tuambie wenzako unaochangia nao kutokea kwa ajali hizo tuwashughulikie sasa hivi!!
 
Ikiwa ni ndani ya wiki moja Mkoa wa Tabora kukumbwa na ajali mbaya za vyombo vya usafiri( Bus) Basi lililoua watu zaidi ya 24 mwanzoni mwa wiki hii wilayani Nzega A.M coach dakika chache zilizopita Basi jingine la kampuni hiyo limepata ajali mbaya ambapo watu watatu wamefariki papo hapo! ajali hiyo imetokea nje kidogo ya mji wa Tabora kama km 15 hivi kwenye kijiji cha kazima ambapo pia kuna bwawa kubwa la maji lijulikanalo Bwawa la kazima.
kwa kuwa ajali imetokea muda mfupi uliopita nitawapa habari zaidi baadaye

Yaani hii inauma sana na serekali kimyaaaaaaa, hivi tutapunguza ajali za barabarani lini? Kila siku ni kukusanya takwimu tu na watu kupata vilema vya maisha. Its not fair to innocent taxpayers. Na kwenye ajali zote utasikia ni mwendo kasi na mabasi mabovu....

These are not accidents they are incidents!
 
wanatabora
embu muulizeni mungu mmearibu wapi jamani
embu tubuni dhambi zenu tumalize hii dhiki ya ma ajali
 
Inasikitisha sna ukichunguza zaidi ni duniani kama hakuna vita au maafa ya mafuriko bas kutakuwa na lingine very sad kifupi tunapungua kuwaachia wengine nafasi!
 
Back
Top Bottom