Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

Mkuu, umeandika points nzuri sana, una hoja za msingi sana, ila kuna haya
1. Limit less speed sio Tanzania pekee, zipo nchi za SADC, nimekuwa South Africa, Zambia na Uganda, ukiacha maeneo yenye vibao vya speed limit unatembea, kama sipo sahihi naomba niambie kwenye hizo nchi nilizotaja bara bara zao limit ni ipi (na bahati nzuri mtaala wa uderva wa nchi za SADC ni mmoja, unaitwa K50)
2. Ni kweli hilo la speed limit za bara bara zetu inabidi liwepo na ni jukumu la TANROADS/TARURA kuset hizo limit kulingana na viwango vya ubora wa bara bara.

3. Ni kweli Polisi na TANROADS wametengeneza mianya ya Rushwa.

Mkuu ninaandika haya kiasi kwa uchungu. Binafsi nimetembea nchi nyingi duniani. Hakuna kitu kama limitless speed na vibao barabarani vina apply kwa magari yote na si vinginevyo. Huko Africa kusini kuna haya:

"The speed limit on a road in South Africa is normally specified by a sign alongside that road.

If no sign is present, then the general speed limits are:

  • 60km/h on every public road in an urban area.
  • 100km/h on every public road situated outside an urban area excluding a freeway.
  • 120km/h on every freeway.
A grace of 10km/h of the posted speed limit may be applied by law enforcement before they would consider issuing a ticket for speeding."

Waweza yaona haya katika site hii pia:

At what speeds you will be fined and arrested for speeding in South Africa

Awapaye watanzania incentive ya kuendesha bila limit anapaswa kuchukuliwa hatua hana nia njema na maisha yetu. Hii si incentives mnatufanya kuingia mabarabarani kwa woga mkubwa.

Dunia nzima Polisi si mtunga sheria hawa wetu wanaotutungia sheria kila leo wanaanzia wapi? Kumbukeni yakiwamo yale ya taa za hazard na zebra crossing. Haya ni Tanzania tu ambako Polisi ni mtunga sheria na msimamizi wakati huo huo. Ajali haziwezi isha kwa mwendelezo huu.
 
Mwaka jana mwezi wa nane nikiwa njiani kutoka mwz kuja dar nimefika maeneo ya singida nilipitwa na v8 ya polisi kwa mwendo wa risasi kufika mbele nikakuta imepata ajari na ndani yake alikuwemo rto wa pwani, sikushangaa sana nilijua kwa mwendo ule na njia za bongo lazima angebutuka tu!

Mkuu ulichoandika hapa ni sahihi kabisa hawa jamaa barabarani ni janga kubwa. Hawajali maana magari haya ni ya umma wala hayawahusu.

Watafute barabara zao kutembea bila limit watuache salama kwenye barabara za umma.

Wanakuja na matamko lukuki yaliyo kinyume cha sheria wakiamini hakuna wa kuhoji.

Waone hapa:

MICHUZI BLOG: NEWZ ALERT:RPC ARUSHA APATA AJALI BAADA YA GARI YAKE KUPOTEZA MUELEKEO

Gari la JWTZ lapata ajali

https://www.jamiiforums.com/threads/ajali-morogoro-mwanajeshi-na-mtoto-wafariki-baada-ya-basi-la-polisi-kugongana-na-noah-iliyokuwa-na-wanajeshi.1435505/page-2


Wanasema kunya anye kuku si bata.
 
Matukio ya ajali za kutisha barabarani zenye kupoteza roho nyingi zisizo na hatia yamekuwa yakija na kwenda. Kila tukio limekuwa likija na reactions tofauti tokea kwa mamlaka ambapo aghalabu ufumbuzi wa kudumu umekuwa hauonekani kuwa mahali popote karibuni.

Zimetokea ajali nyingi mbaya, kumbuka Majinja express, lukuki za city boy express, kigoma karibuni kulikuwa na ya kuonga train, kumbuka wale watoto wa shule arusha nk nk.

Ya Mbeya ya hivi karibuni imepelekea mabadiliko ya waziri wizara ya mambo ya ndani na wakuu kadhaa Polisi Mbeya kushushwa vyeo. Kabla hata hakujatulia, Mbeya huko huko tena, jana watu kadhaa wamefariki kwenye ajali ya lorry na magari madogo.

Ni wazi kuwa kwa mwendelezo wa approach zetu hizi zisizo angalia kwa undani sababu za haya kuendelea kutokea, basi hata sasa itakuwa ni suala la muda tu kusubiria ajali na vifo vingine na vingine, vingine na vingine, nk.

Kwa tafakari ya kawaida tu, haichukui muda kuona kuwa, ni aidha kwa makusudi au kutofahamu kuwa hatua sahihi hazichukuliwi. Kwa bahati mbaya sana kwa kuchukua hatua sahihi pana ulaji mkubwa wa watu fulani utaathirika.

Mzizi mkuu wa vyanzo vya ajali upo katika RUSHWA. Baadhi ya watu waliopo katika nafasi za kuweza kutupishilia mbali na ajali hizi za kila mara zenye kugharimu maisha yetu na kuwa ni suala la muda tu, ati kwa maslahi yao maovu, hawanayo nia wala utashi wa kuliongelea hili.

Jiulize ni nchi gani hapa duniani ati baadhi ya magari katika sehemu ipi ya barabara (you name it) yanaruhusiwa kutembea kwa mwendo kasi wowote pasipokuwa na limit kabisa?! Ati kuwa so long as hakuna restriction ya 50km/h then mwendo kasi ni discretion ya dereva husika?! Ama kweli hili ni katika Tanzania yetu peke yake na tena labda hii ya siku hizi. Jamani, hivi tumerogwa?

Mbaya zaidi magari ya wasimamia Sheria hizi zilizo fyongo namna hii wakiwamo Polisi, wa huko mahakamani, na hawa wenye kupeperusha bendera zao Fulani Fulani hata hizo 50km/h kwa saa haziwahusu. Hii ikiwa ni wao katika capacities zao kama taasisi na hata wao kama watu binafsi. Tafsiri kamili ya shamba la Bibi!

Kwa mtaji huu tutapona kweli humu barabarani? Si kweli kuwa rambirambi kisa ajali ni suala la muda tu? Haipo haja ya kuchoka kutuma rambirambi bali ni vyema nadhani kujiandaa kwa nyingi nyingine and very soon.

Katika hili pana mapato tena very lucrative yatokanayo na RUSHWA yenye mtizamo wa kuona mbali sana. In disguise serikali inafanywa kuona inapata inayodhani kuwa ni mapato halali kwa ajali ya maendeleo, kumbe nyuma ya pazia wanufaika wakuu tena ni binafsi ambao pia hata ndiyo wao wangetegemewa kushauri vilivyo wakiendelea kujineemesha wao na familia zao.

Hivi ni kwa nini askari wa usalama barabarani katika zao ngazi zote maisha yao hayaendani katu na mishahara yao rasmi? Kwa nini kuhamishiwa usalama barabarani huonekana ni promotion na kutolewa huko huwa kama demotion?

Chonde chonde kwa tamaa za hawa jamaa pasipo kuwa na jitihada za kuumong'onyoa huu mzizi wao mkuu wa RUSHWA walipojifichia, tutaendelea kulipa faini zisizo kuwa na tija yoyote, huku tukiendelea kuwaneemesha watu hawa wasiokuwa.na chembe ya huruma tukisubiria zamu zetu za kufa barabarani.

Tumelaaniwa na nani siye, hatuwezi hata kuona tofauti katika Sheria zetu barabarani hata kwa kulinganisha na majirani zetu basi, kama huko walikoendelea ni mbali?


Mkuu umesema vizuri kuhusu swala la ajali za barabarani.

Binafsi nnadhani ajali zinachangiwa na mambo yafuatayo ambayo mmeshayasema wengi wenu;

  1. Miundo mbinu(barabara) mibovu na uhaba wa alama za barabarani
  2. Utoaji holela wa leseni za kuendeshea bila kupitia mafunzo kama inavyopaswa
  3. Kutokuwepo kwa kikomo cha mwendokasi kwa magari binafsi
Kitendo cha kuweka kikomo cha mwendokasi kwa mabasi na kutokuweka kikomo kwenye magari binafsi huku magari yote haya yakitumia barabara hizohizo kinaacha mlango mkubwa sana wa kusababisha ajali.Gari dogo linaloenda kwa kasi linaweza kusababisha ajali kwa bus ambalo linaenda kwa mwendo wa kawaida.
 
Nadhani utaratibu wa South Africa kuhusu limit za barabarani panapo nia njema ulikuwa bora sana pia kwetu katika kuondoa kabisa ajali au kuzipunguza kabisa. Pia utaratibu juu wa South Africa ungekuja na majibu kwenye kero nyingine ifananayo na hii kama nilivyowahi kuandika uzi huu:

Adha katika usafiri wa umma Mikoani kuhusisha Dar

Badala ya kuwekeza peke yake katika sala ili mwenyezi Mungu atunusuru na ajali hizi tungejipanga pia katika kujifunza tokea kwa wenzetu waliotutangulia. Mark my words hayupo wa kujifunza tokea kwetu kwa kuweka limit less speed kwa magari yoyote yasiyokuwa katika misafara rasmi inayoambatana na kusaidia barabara kabisa kupisha magari ya misafara pekee.
 
Tumekua na ajali za mara kwa mara ambazo haziishi lakini sidhani kama mpaka sasa vyanzo hivi muhimu vya ajali vinazungumziwa zaidi ya kuambiwa tatizo ni mwendo kasi, na Uzembe wa dereva.

Fatigue, Umasikini, Ubovu wa barabara, Elimu ndogo ya vyombo vya moto, Elimu ya msingi (std 1 to std 7), pia ni vyanzo vikubwa sana vya ajali hapa Tanzania.
Nitaelezea kwa uchache na wengine wataweka nyama.

FATIGUE (UCHOVU):
Madereva wengi wa malori, mabasi na hata gari ndogo huwa hawapumziki vya kutosha kiasi cha kufanya safari ndefu, Madereva wa mabasi na malori husafiri mamia ya km lakini huwa hawalali vya kutosha kiasi cha kuwa na nguvu ya kuanza safari siku inayofuata. Wengi wa madereva hawa wakifika kwenye vituo vyao vya kupumzika huanza kufanya starehe kwa maana ya pombe na umalaya na matokeo yake asubuhi huamka na hangover ya K**MA na POMBE, hangover ya hivi vitu viwili ni usingizi na uchovu kupitiliza siku ya pili yake. Elimu ya kujitambua na kuirasimisha hiyo ajili ndio muarobaini pekee kwenye hili, vijana wanahitaji elimu ya kutosha ya kujitambua na Serikali iifanye hiyo kama ajira rasmi kwa maana ya watu walipwe mishahara, night allowance's na wawe na mikataba inayotambulika kisheria wakatwe PAYE NA HIFADHI YA JAMII.

UMASIKINI:
Jamii nyingi sana za kitanzania ziko kwenye umasikini mkubwa na huu umasikini ni chanzo cha matatizo mengi sana Tanzania.
Jamii nyingi za kimasikini ndio zimetoa hawa madereva wengi wanaoendesha roho za watu huko barabarani, na jamii hizi za kimasikini zimekuwa tegemezi sana kwa hawa ndugu zao ambao ni madereva wetu, Shida/Umasikini huleta stress na mwisho wa siku hupunguza umakini barabarani. Dereva huyu anapenda kuwapa wanae elimu bora kama wengine maana anaona mateso anayoyapata yeye barabarani, Dereva huyu anahitaji kusomesha ndugu zake wapate elimu bora, Dereva huyu anahitaji kuwa na nyumba bora ya kuishi, Dereva huyu anahitaji kuwapa matibabu ndugu na wanae, Dereva huyu anahitaji kuwa lishe bora watoto wake, Dereva huyu anahitaji kulea wazee wake choka mbaya wanaishi kijijini huko, HAYO YOOTE MWISHO WA SIKU HULETA STRESS KWA HUYU DEREVA NA MATOKEO YAKE NI KUPUNGUZA UMAKINI AU KUTOKUWA MAKINI KABISA.

Serikali au wenye mamlaka lazima watambue umasikini ni tatizo kubwa Tanzania na tukiwatoa watanzania kwenye umasikini tutakuwa tumetatua mengi, Dereva na ndugu zake wakiwa na kipato kizuri ataishi maisha ya furaha na kazi yake ataifanya vizuri na kwa umakini maana ndio inamuweka mjini ( mfano Madereva South Africa, Botswana, Namibia,Zambia pale London, USA nk).

UBOVU WA BARABARA:
Tanroad jaribuni kuwa na road patrol za mara kwa mara kila mkoa, kila wilaya ili mjue matatizo yaliyopo kwenye barabara zebu na muamue haraka, uzibaji wenu wa viraka bado ni wakizamani na huchukua muda mrefu, barabara zinakaa na mashimo na mibonyeo kwa muda mrefu sana (hapa ni vyema kila Tanroad mkoa ikawa na fungu la emergency){naikumbuka ajali ya basi la MAJINJA PALE KATI YA IRINGA NA MBEYA NA LILE KONTENA CHANZO NI LILE SHIMO PALE).

Tanroad ni vyema mpeleke watu wenu nje wajifunze namna bora ya usimamizi na ujenzi wa barabara ili mwisho wa siku tuwe na Standard yetu ya ubora wa barabara zetu ili kila mjenzi akija tunampa specifications zetu, Kona zisizo na msingi ni nyingi kwenye barabara zetu kiasi cha kutengeneza hatari zisizotakiwa, Maeneo korofi yote yakijengwa mjaribu kuyafanya yawe mapana na ikiwezekana muweke TAA eneo husika ili usiku iwe rahisi. TANROAD NA SERIKALI acheni siasa kaeni chini mchunguze kwa wenzetu ili tupata standard yetu ya ubora wa barabara zetu na tuachane na hizi barabara zinazobonyea na kuchimbika kila siku, kona sehemu zisizohitajika (kifupi makona sio muhimu mbona Kenya hapo wanatushinda hawana kona zisizoeleweka, kule Zambia pia mbona hakuna makona kona kila mahali)

ELIMU NDOGO YA VYOMBO VYA MOTO.
Watanzania wengi wanamiliki na kuendesha vyombo vya moto lakini hawajui matumizi sahihi ya vyombo hivi kifupi wengi hawavijui hivi vyombo sio lazima uwe fundi au proffesional driver hapana hapa tunaongelea General knowledge ya kujua magari na tabia zake mfano huwezi ukawa na IST unataka kuovertake FORTUNER na mbele yako linakuja LANDCRUISER V8 na bado unajiamini utaliwahi, huwezi ukawa na gari yako inachelewa kubadili Gia na wewe huna habari, Ufanyaji wa service kwa wakati na kujua wakati sahihi hii sio kazi ya Fundi, Oil sahihi kwa matumizi ya Gari, Upepo sahihi kwa matumizi ya Gari lako, kwa wale wanaondesha manual kujua wakati gani utumie gia gani, Waendeshaji wa Magari sio lazima uwe umeajiriwa kuna umuhimu wa kulijua gari zako hata kwa kusoma broachure mbali mbali za magari, kuangalia vipindi mbalimbali vya magari, kuzungumza na wataalamu wa magari upate abcd za magari ili ubongo ujue matumizi sahihi ya magari na barabara.

ELIMU YA MSINGI (STD 1- STD 7).
Hii elimu ni nzuri na muhimu sana kwa watu kuwa na uelewa na kujitambua, Elimu ya msingi humsaidia mtu kujijua yeye ni nani na anatakiwa afanye nini, Elimu ya msini humsaidia mtu kujua kusoma na kuandika na hili litamsaidia mtu kujua na kuelewa alama mbalimbali za barabarani, Elimu ya msingi itamfanya mtu kuwa muelewa hata pale anapokosea na kuruhusu kueleweshwa na sio kuwa mbishi, Elimu hii humfanya mtu ajielewe na kuwa na utu barabarani kiasi cha kureport jambo lolote baya alionalo barabarani, Elimu hii humsaidia mtu kuwa na ubongo active kiasi cha kuwa na maamuzi sahihi barabarani.

Watanzania tuitilie mkazo sana elimu ya Tanzania ili watu wengi waweze kuipata, Serikali ni vyema ikahakikisha elimu ya msingi inakuwa bora ili watu wamalizapo shule ya msingi wawe na content sahihi kichwani itakayowawezesha kweli kupambana na mazingira yao, Elimu bora ya msingi ijikite zaidi kwa watu kupata uelewa na kujitambua na kuwafundisha watu mambo yasiyo na msingi, vitu kama alama za barabara,namna bora ya matumizi ya barabara inaweza kuwa kipindi maalumu kwa wanafunzi wa darasa la sita, tusifikirie sana watu kufanya mtihani au mitihani migumu katika level hii hapana ziwepo tu test za kupima uelewa na continuous assessment , Elimu bora ya msingi itajenga watu bora wenye msingi imara ambao mwisho wa siku watatupunguzia matatizo mengi..
 
Ajali za Tanzania hazisababishwi na Ubovu wa Miundombinu, ingekuwa hivyo miaka ya nyuma tulikuwa na miundombinu mibovu kuliko hii ya sasa ila dereva walifika salama.

UMAKINI BARABARANI NDIYO TATIZO.
 
Ajali za Tanzania hazisababishwi na Ubovu wa Miundombinu, ingekuwa hivyo miaka ya nyuma tulikuwa na miundombinu mibovu kuliko hii ya sasa ila dereva walifika salama.

UMAKINI BARABARANI NDIYO TATIZO.

Zamani magari yalikuwa LANDLOVER 109, BEDFORD, LEYLAND DAF, SCANIA 111, SCANIA 93, PEOGEOT nk magari haya mengi yalikuwa low speed huwezi kukimbia kifupi gari lenyewe linakulimit.. Gearbox za hayo magari zilikuwa ni low speed high torque. Sasa hivi hayapo tena hayo magari, tuna magari ambayo high speed na dunia pia inakimbia lazima nasisi tukimbie kuharakisha production.
 
Zamani magari yalikuwa LANDLOVER 109, BEDFORD, LEYLAND DAF, SCANIA 111, SCANIA 93, PEOGEOT nk magari haya mengi yalikuwa low speed huwezi kukimbia kifupi gari lenyewe linakulimit.. Gearbox za hayo magari zilikuwa ni low speed high torque. Sasa hivi hayapo tena hayo magari, tuna magari ambayo high speed na dunia pia inakimbia lazima nasisi tukimbie kuharakisha production.
Ajali ni spidi?
 
SOLUTION KUUUUUBWA YA KUZUIA HZO AJALI YA KUGONGANA USO KWA USO NI KUJENGA BARABARA ZOTE ZA KWENDA MIKOANI ZENYE NJIA NNE AMBAZO ZIMETENGANISHWA KATIKATI. OVA
 
Kwa upuuzi huu wa kusitisha uokoaji, maoni yetu watayasikiliza kweli...

Mbunge alionya akakejeliwa kwa majibu ya hovyo ila sasa ndio yanaonekana madhara yake
 
Kwa usafiri wa majini kwa kutumia vivuko, abiria avae boya ndo aingie kivukoni. Sio taharuki inatokea ndo tuanze kutafuta maboya. Hali ikiwa mbaya zaidi mimi nanunua boya langu kuanzia leo natembea nalo kila napo fanya safari zangu majin
 
Hakuna jawabu la kumaliza kabisa ajali.Kwasababu ni ajali.
Ila tunaweza kupunguza baadhi ya mambo yanayochangia ajali.
Moja ninalopendekeza ni kuwalipa madereva kwa saa. Hii ina maana kwamba dereva akiongeza mwendo atapunguza malipo yake mwisho wa safari au mwisho wa mwezi.
Kuweka madereva wawili ina maana dereva mmoja atakaa kiti cha abiria, halafu kisheria yupo kazini hata kama haendeshi basi. Hizi gharama za ziada mwenye chombo hawezi kukubali.
Utaratibu wa malipo kwa saa unafaa hata maofisini. Watu wengi maofisini wanachelewa kufika asubuhi na kwahi kuondoka jioni kwa sababu za usafiri, lakini mwisho wa mwezi analipwa mshahara kama vile alifanya 45-48 hrs kwa week!
Huo ndiyo mchango wangu.
 
Tatizo pia lipo upande wa askari wa usalama barabarani hasa kwenye barabara za vumbi.Mfano njia ya kutoka Kahama kwenda Mwamnange na Kutoka Kahama mpaka Geita kupitia Kakola zimeshageuzwa kuwa miradi ya askari wa barabarani.Ukifika Kakola utashangaa kuona jinsi ambavyo jamaa wanayaangalia magari yakipita na abilia mpaka mlangoni..
 
Naomba kujua hili wakuu,


Maana siku hizi watu wamekuwa waoga kusafiri kwa kuhofia maisha yao na ndoto zao kukatishwa na maajali barabarani na majini.


Siku hizi mtu ukiwa unajiandaa safari unawaza kama utafika salama.
 
Back
Top Bottom