Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

Huwezi kusema it could have been avoided wakati huna hata fact moja ya mazingira ya ajali.

Post nzima unauliza maswali, walifunga mikanda hawakufunga? Dereva ana uzoefu au hana? Walikuwa mwendo gani? Hujui fact yeyote ya ajali. How on earth can you say "it could have been avoided"?
 
.....ni huzuni kuu..... ila for future tuangalie na hizi "School Bus" za kawaida kila siku,. sheria inasemaje?,... maana nyingine ni mbovu na zinabeba watoto wengi kwa pamoja,. ndio kuna shule ambazo wanazo gari zao za shule ambazo nyingi ni nzuri,.. vipi kuhusu hizi daladala zinazogeuzwa kuwa school bus mida ya asubuhi na jioni?. mikataba ni kati ya mwenye daladala na mzazi shule hapo inajitoa kwanini?, na wao ndio wamekuagiza kwa huyo mtu kwamba ndio wanamtumia
 
Tu

Tujifunze kutoka hili. Kama nchi zilizoendelea Mfano za Scandnavia Maximum speed ni 70 KM/saa na kila section kuna camera kwanini sisi tusiweze. Maisha ya mtu ni ghali yakipotea hayarudi tena!!. Tunakwenda vizuri kwa mabasi makubwa ya mikoani ila sasa ni awamu ya kwa magari yote!! 70KM/saa. No compromise on ones life.


NAOMBA WAZIRI HUSIKA NA WATAALAMU WA VYOMBO VYA USAFIRI WATUSAIDIE KUCHUNGUZA,NA KUTOA MAJIBU YA MASWALI HAYA, NA KUTUNGA AMA KUSIMAMIA SHERIA ZA USALAMA WA VYOMBO VYA USAFIRI KWA WATOTO WA SHULE ZOTE TANZANIA.

MUNGU WAPE NGUVU WAZAZI WA WATOTO HAWA NA UTUSAMEHE SISI WATANZANIA KWA KURUHUSU VIFO HIVI VITOKEE KWA KUTOKUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI, NA USALAMA WA VYOMBO VYA USAFIRI VYA WATOTO WETU MASHULENI.

AMINA.[/QUOTE]

hasa mabasi ya shule
 
.....ni huzuni kuu..... ila for future tuangalie na hizi "School Bus" za kawaida kila siku,. sheria inasemaje?,... maana nyingine ni mbovu na zinabeba watoto wengi kwa pamoja,. ndio kuna shule ambazo wanazo gari zao za shule ambazo nyingi ni nzuri,.. vipi kuhusu hizi daladala zinazogeuzwa kuwa school bus mida ya asubuhi na jioni?. mikataba ni kati ya mwenye daladala na mzazi shule hapo inajitoa kwanini?, na wao ndio wamekuagiza kwa huyo mtu kwamba ndio wanamtumia

hamna sheria rafiki
 
NAOMBA WAZIRI HUSIKA NA WATAALAMU WA VYOMBO VYA USAFIRI WATUSAIDIE KUCHUNGUZA,NA KUTOA MAJIBU YA MASWALI HAYA, NA KUTUNGA AMA KUSIMAMIA SHERIA ZA USALAMA WA VYOMBO VYA USAFIRI KWA WATOTO WA SHULE ZOTE TANZANIA.

MUNGU WAPE NGUVU WAZAZI WA WATOTO HAWA NA UTUSAMEHE SISI WATANZANIA KWA KURUHUSU VIFO HIVI VITOKEE KWA KUTOKUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI, NA USALAMA WA VYOMBO VYA USAFIRI VYA WATOTO WETU MASHULENI.

AMINA.

hasa mabasi ya shule[/QUOTE]
80 km/h
Driving is a great way to explore Norway outside major cities. There is a limited network of motorways around Oslo (up to 110 km/h). Country roads are mostly dual-lane separated by a yellow line in the middle. General speed limit is 80 km/h (50 km/h in villages and towns) if otherwise not s
 
Kwa muonekano wa ile gar,ni dhahir hawa watoto hawakufunga mkanda,maana haijabondeka saana kwa nyuma..meana walio kaa nyuma wangeweza kusalimika kwa asilimia kubwa
Ni kweli ile gari nyuma yote nzima. Inaonekana kama wangefunga mikanada wengi wangepona. Nahisi walimwagwa pamoja wakati inapinduka. Mungu awalaze pema peponi. Ila siku ya kufa ikifika hakuna kinachokumbukwa.
 
Hizi kauli zinanifanya nisimwamini Mungu wako.. Ati bwana alitoa, Bwana ametwaa, una maana huyo Mungu ndo kaua
Hiyo ni dimension nyingine mkuu!!kuna jamaa mmoja alikuwa asafiri na ndege wakati amekaa yeye na familia yake wakiangalia TV utabiri wa hali ya hewa (baada ya habari kama kawa)ikasemekana hali ya hewa itakuwa mbaya,mama yake jamaa akamsihi mwanae aahirishe safari na kweli akaahihirisha, asubuhi yake "breaking news"ile ndege imeanguka hakuna aliyepona, mama mtu akakimbilia chumbani kwa mwanae huku akiwa na furaha isiyokuwa na kifani wakati anamuamsha kijana wake ili ampe habari za ile ndege jamaa haamki kumbe saa nyingi jamaa katangulia mbele ya haki.
 
Hiyo ni dimension nyingine mkuu!!kuna jamaa mmoja alikuwa asafiri na ndege wakati amekaa yeye na familia yake wakiangalia TV utabiri wa hali ya hewa (baada ya habari kama kawa)ikasemekana hali ya hewa itakuwa mbaya,mama yake jamaa akamsihi mwanae aahirishe safari na kweli akaahihirisha, asubuhi yake "breaking news"ile ndege imeanguka hakuna aliyepona, mama mtu akakimbilia chumbani kwa mwanae huku akiwa na furaha isiyokuwa na kifani wakati anamuamsha kijana wake ili ampe habari za ile ndege jamaa haamki kumbe saa nyingi jamaa katangulia mbele ya haki.
Doh aisee kweli siku yako ikifika hamna kitakacho kuzuia hata ukijifungia ndani
 
Hizi kauli zinanifanya nisimwamini Mungu wako.. Ati bwana alitoa, Bwana ametwaa, una maana huyo Mungu ndo kaua
Ni kauli za kidini ambazo hazina mashiko. Kuna ufahamu zaidi ya hiyo kauli ambao ningependa kuufaamisha uma, lakini nachelea kubadilisha MADA.
 
KUNA UHUSIANO GANI KATI YA VYETI ALIVYONAVYO DEREVA, UJUZI ALIONAO DEREVA, KIPATO HALALI APATACHO DEREVA, NA ONGEZEKO LA HIZI AJALI ZA BARABARANI?

Kwa muda mrefu kama taifa tumekuwa tukijaribu kupunguza ajali za barabarani kwa kutumia mbinu za askari wa usalama barabarani kuwabana madereva. Japo yapo mafanikio, lakini kushindwa kwa sekta/idara zingine kushiriki kupambana Na ajali barabarani husussn zinazohusisha mabasi ya abiria kuna punguza mafanikio hayo.

Katika mchezo wa soka kuna msemo maarufu kuwa "Football is a game of mistakes" Na inadaiwa karibu magoli yote yanayofungwa katika mchezo huo utokana Na kosa/makosa ya wachezaji wa timu iliyofungwa. Hivyo basi kama kila kosa lingeweza kusababisha maafa, majanga,misiba na simanzi kama makosa ya kibinadamu afanyayo dereva. Dunia/nchi vingekuwa na katika wakati mgumu sana.

Hivyo basi dereva ana nafasi ya kipekee katika Jamii. He ni kweli Jamii zetu zinatambua hilo? Chukua mfano wa kosa/makosa ya kibinadamu aliyofanya dereva mwenzetu wa basi la wanafunzi lililopata ajali huko Karatu. Kosa/makosa take yalisababisha simanzi nchi nzima, watu 33 wakapoteza uhai Na madhara mengine mbali mbali.

Ni kwanini jitihada kubwa za kikosi cha askari wa usalama barabarani zinashindwa kupunguza kwa uendelevu tatizo hili (yaani hata zisipokuwepo tochi, pasiwepo ajali za mabasi ya abiria)?

Kwa mtazamo wangu kutokana na uzoefu nilioupata nikiwa kiongozi was madereva wa mabasi. Mchawi ni mfumo wetu wa usimamizi was sekta ya ussafirishaji unamfanya dereva was basi la abiria kuwa mtekelezaji muhimu wa ukuzaji mapato ya kampuni Na yeye binafsi.

Kutokana na upungufu huo dereva w basi kipaumbele chake cha kwanza in mapato ya kampuni ili aweze kuendelea kuwepo katika ajira hiyo kupitia kushindana kuipatia kampuni abiria zaidi. Pili ni kuongeza kipato chake binafsi kwa kuwa ujira wao ni Mdogo sana kulinganisha na majukumu yao na umuhimu wao katika Jamii. Tatu ndio hufuata kutumia ujuzi wao vyema na Nne ndio kuzingatia n kutii sheria za usalama barabarani. Mfano hai ni ajali za hivi karibuni za mabasi ya Ally's Na BM coach.

Mfumo wa uendeshaji wa BRT unamfanya dereva kipaumbele chakeiwe ni kiwe kutii na kuheshimu taa na alama za vivuko vya waenda kwa miguu n.k ili aweze kuendelea na ajira yake. Hii ni kutokana ukweli kuwa dereva was BRT sio sehemu ya utekelezaji wa mipango ya kukuza mapato ya kampuni kupitia ushindani wa kupata abiria zaidii.

Tukiondoa umachinga ktk sekta yetu ya usafiri wa umma kwa kuwepo utitiri wa kampuni za mabasi hususan kati ya mkoa mmoja hadi mwingine. Na badala yake tukawa na professional passengers operators wenye uwezo wa kuwekeza ktk yafuatayo:- a) Mabasi ya kisasa kulingana Na miundombinu yetu (b) Raslimali watu yaani madereva, makondakta, mafundi n.k wenye ujuzi Na weledi was kutosha (c) Kuwekeza ktk stahiki za watumishi ikiwemo mishahara bora, malipo mengine kama vile Masaa ya ziada, matibabu,kiinua mgongo n.k (d) Kuwekeza ktk teknoljia za kufuatilia Na kudhibiti mienendo ya watumishi kama vile Tachometer, Tachograph katika Magari yao n.k
 
Kwa utafiti wangu mdogo Nitaandika kwa ufupi, sekta ya Usafirishaji imeachiwa Watu Binafsi ambao hata wengi wao Elimu na Uelewa ni tatizo.

Wengi wao kumwajiri Dereva mwenye taaluma ya chuo ni wachache wamefanya hivyo, Na hata walioajiri Bado madereva hawana mikataba ya kudumu, Wamiliki au wasafirishaji (Matajiri) Wakiwamo Waarabu, wahindu na hata wabongo wenzetu bado wako kwenye fikra za kale sana katika suala la usafirishaji hawaendi na wakati, ingawa wengi wao wana ukwasi wa kutisha lakini uendeshaji wa sekta hii bado serikali inatakiwa kuweka mkono wake.

Mfano, Ni mara chache sana kusikia madereva wa serikali wamepata ajali mara kwa mara hii inatokana na nini?

Madereva hawa wana kozi maalum za usalama barabarani kila baada ya muda fulani na hata madereva hao wana madaraja yao kulingana na ngazi aliyoifikia,wana ajira za kudumu,wana posho zao wawapo safarini, kwa hilo serikali imejipanga kuhakikisha vyombo vyake vya usafiri viko salama na abiria wake, Lakini kwa sekta Binafsi hamna kabisa.

Hapo juu niliongelea swala la Elimu kwa matajiri au wamiliki wa vyombo vya usafirishaji ukweli wengi wao hutegemea ushirikina katika biashara hii..! Wanaaamini kwamba mambo hayaendi bila matunguli, na kuna ajali nyingi zimehusishwa na imani hizi, bila mabadiliko ya kifikra na kielimu juu ya uendeshaji Huduma kisasa Sekta hii itaendelea kuangamiza Maisha ya watanzania kwa tamaa za watu kupata mali.

Hivi majuzi walitangaza mgomo na kwa mshangao wa ajabu walalamikia serikali kwenye media kwamba sheria zimetungwa kwa kiingereza hawajui na hawawezi kusoma ni aibu kubwa hasa katika kupanua soko la usafirishaji ndani ya Afrika Mashariki tutaweza ushindani kweli? Nilitegemea Wasafirishaji hawa wana wanasheria wao ambao wangehusika kwa mambo ya Kisheria yanapotokea masuala kama hayo.

Kulingana na hayo niliyoeleza ni ushauri wangu kwa serikali ifanye tathimini ili sekta ya usafirishaji isibaki tu kwa watu Binafsi, na yenyewe itafakari kuingia kwenye usafirishaji kuokoa maisha ya Watanzania.

KWANZA: Serikali itaepusha migogoro pindi sekta binafsi wanapotangaza kugoma wananchi wataendelea kupata huduma na hii itaondoa adha kwa wasafiri wanaoathirika sana punde migomo inapotokea.

PILI: Mpango huu ufanyike kupitia Halmashauri zote nchini, zinunue mabasi kwa safari za mbali na mijini pia magari madogo (TOWN BUS), malori kwa ajili ya usafirishaji, Mpango huu utazisaidia halmashauri zenyewe kuongeza mapato na kulipa gawio serikalini na kukuza miradi kwenye halmashauri zao, na kama nilivyosema hapo awali madereva wa serikali wana weledi na taaluma zao hivyo nina imani ajali kupungua sana na huko pia sitegemei matunguli katika Biashara za serikali.

TATU na Mwisho nina imani kabisa na serikali ya JJPM na watendaji wake usimamizi ukiwa mzuri sekta hii itafika mbali ikiwa ya UMMA na Migomo ikitangazwa ya usafirishaji hatutakuwa na wasiwasi .
 
TUNDALI,

Mkuu umeandika mengi lakini bahati mbaya ni kuwa ume bwabwaja zaidi kuliko kuwa na hoja.

Hujaona magari ya serikali au ya mashirika ya umma yakihusika kwenye ajali? Ni magari ya umma yapi yanayofuata alama za barabarani? Yapi yanayojua kuna speed limit barabarani au hata kuwa kuna zebra crossing?

Mkuu kwa kukumbusha tu au kukufahamisha kama ulikuwa hujazaliwa siku za nyuma kulikuwa na mabasi ya serikali yakiwamo Kamata, mabasi ya Railways, Kauma, Kaudo, UDA, CoCabas nk you name them. Yote yalikufa kifo cha mende achilia mbali kuwa yalikuwa hayasumbuliwi na polisi wala mamlaka kama Sumatra kama wanavyofanyiwa hawa ambao wewe una uthubutu wa kuwaona kuwa wana akili zero. Ndugu ni eneo lipi ambalo wewe unalitanabaisha na akili zozote huku makwetu? Kwa nini wachina na makampuni toka nje yanaendelea kuja kutujengea mabarabara? Hatuna wahandisi wetu kufanya haya? Huko midogodini je hatuna ma geologisit?

Sidhani kama kulikuwa na moral authority ya kuwabeza baadhi ya watu katika nchi hii tokea katika hoja nyepesi nyepesi kama zako pasipo na kuangalia boriti kwenye jicho lako kwanza.

Wapo watu katika mamlaka wenye maslahi tofauti ambao wasingependa sekta binafsi ya usafirishaji ku prosper hilo ni wazi. Kama wangekuwa mamlaka zingekuwa na maslahi mapana ya nchi at hand kwa kuanzia wapiga debe wasingekuwapo katika vituo vya mabasi.

Uliwahi kujiuliza nani anawalea wapiga debe kinyume cha matakwa ya abiria wala wenye mabasi?

Nitakuwa sijakutendea haki kama sitakukumbusha kuwa kudai fulani ana ukwasi mkubwa kwa hisia tu bila ya yeye kusema hivyo ni kutojitendea haki wewe mwenyewe. Palikuwa na uzi hapa wa mzee Sumry aliyefikia hatua ya kufunga biashara ya mabasi kurejea shambani tokana na usumbufu na hasara kubwa inayoambatana na biashara hii.

Ni ajabu na kweli mtu unapotokea bila ya facts zozote ku rukia kwenye conclusions kama ulizoweka kwenye bandiko lako na kwa hoja za ki Sizonje kama ulizoweka.
 
Ajali za barabarani haswa zile zenye kusababisha maafa makubwa zimekuwa zikuhusianishwa na mabasi ya abiria na aghalabu makosa huwa ni ya madereva wetu.

Ili kukabiliana na hili ni muhimu tukawa na chuo maalumu cha udereva wa mabasi na course mahususi ya udereva wa mabasi ya abiria.
 
Huwezi kusema it could have been avoided wakati huna hata fact moja ya mazingira ya ajali.

Post nzima unauliza maswali, walifunga mikanda hawakufunga? Dereva ana uzoefu au hana? Walikuwa mwendo gani? Hujui fact yeyote ya ajali. How on earth can you say "it could have been avoided"?
Ndio maana alisema ni mawazo yake. Unaweza kuchangia hoja yako but co kumshambulia. Hekima ni bora zaidi!
 
Ni kauli za kidini ambazo hazina mashiko. Kuna ufahamu zaidi ya hiyo kauli ambao ningependa kuufaamisha uma, lakini nachelea kubadilisha MADA.
Naamini kuna uwezekano wa kutoa hoja au kumrekebisha mtu pasipo kushambulia imani, kabila, elimu n.k yake. Hapo ndio unapoonyesha ukomavu wa kubishana kwa hoja
 
Aise leo nilikuwa kwenye bajaji siti ya nyuma kulia kwangu yupo mmama na kushoto yupo dogo flani, tumefika ile junction ya kuingilia barabara kuu mara mduanzi flani ana chaser katuvamia site yetu ya kushoto kama vile hana akili nzuri, mungu ambariki dereva wa bajaji aliemkwepa yule mduanzi .....Ajali hazikwepeki hii nchi
 
Wanyama wanawekewa Uzio ,,,Watu wanawekewa Bumps

Speed ya 50 ndio imetawala barabara nyingi sasa...sehemu chache sana wameruhusu 80...

Hii inasababisha foleni kubwa sana Dar kuanzia kibaha, mpaka unaingia ubungo

Sasa gari inayotoka Moshi au Arusha...inatakiwa kufika dar saa tisa mpaka kumi badala yake magari yanafika saa moja mpaka saa mbili, haya mabasi yanakuja kufika muda mmoja na yale yanayotoka Iringa, Mbeya...etc

Suluhisho la kupunguza Ajali:

- Elimu itolewe kwa Umma, watu wazima na wanafunzi.. (Kamati ya ulinzi na Usalama) Kila mkoa waitishe mkutano wa hadhara na Traffic watoe elimu kwa raia

- Traffic Wasimamie sheria na Madereva wapewe adhabu kali sana....

- Umakini wa Dreva uongezeke, waache kutumia simu..


- Dreva mchovu au mlevi asiendeshe gari (umakini hapa haupo)

Na Hivyo Lower speed iwe 80 na high way iwe 120 Ruksa

Hii speed limit ya 50 lengo lake ni kukusanya pesa, Kwani serikali haipati kodi?

Hawa Traffic ni wakatili sana na ni Mradi wa Rushwa....Kwa nini hawatoi EFD risiti?

Pia Traffic wanakula elfu kumi kumi nyingi sana


 
Back
Top Bottom