Ajali Shinyanga: Basi kampuni ya Bright lagongana na gari dogo. Inasemekana watu wawili wamepoteza maisha papo hapo na wengine kujeruhiwa

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,188
4,100
Basi la Bright linalofanya safari zake kati ya Mwanza na Dodoma, limeanguka leo asubuhi nje kidogo ya mji wa Shinyanga, baada ya Dereva wa Basi hilo kujaribu kumkwepa Mwendesha piki piki, na kusababisha gari hilo kugongana na Gari ndogo kisha kupinduka.

Taarifa za awali zinasema Watu wawili wamepoteza maisha papo hapo, na wengine 11 kujeruhiwa huku baadhi yao wakidaiwa kuwa na hali mbaya.

1.jpg
2.jpg

 
Kwa watu tunaojitambua dereva wa basi hakutumia akili, huwezi kukwepa mtu moja halafu uhatarishe maisha ya watu wengi
Yamkini alitegemea atamkwepa na hatimaye kuepusha ajali. Kumbuka ni maamuzi ndani ya sehemu ya sekunde isiyofika hata robo.
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Back
Top Bottom