Ajali nyingine

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
Ajali ya basi la Kampuni ya Southern Coach katika kijiji cha Miteja, Kilwa, Mkoani Lindi, iliyotokea leo majira ya saa 8 mchana. Kwa mujibu wa mashuhuda, hakuna aliyefariki japo kulikuwa na majeruhi walioumia vibaya na kukimbizwa hospitali. Chanzo cha ajali bado hakijajulikana

download+(3).jpg


Sehemu ya nyuma ya basi lililopata ajali leo
download+(2).jpg



Wanakijiji wakiangalia kama kuna abiria aliyenaswa ndani ya basi. Picha zimeletwa na mdau kwa kutumia simu yake ya iPhone. Picha zote kwa Hisani ya Michuzi Blog​


download.jpg
 
Dah! Hizi ajali tutakuwa tunaogopa kusafiri. Pole kwa majeruhi.
 
Leo pia Bus la Ng'itu liendalo kati ya Dar-Mtwara limepinduka kati ya Nangurukuru na kijiji cha Sinza Wilayani Kilwa...
 
maisha ya tz kama yanakua valued in a monetary scale, yamefikia minus zero sasa! cha kusikitisha tumezoea,utaskia 'bwana alitoa,bwana ametwaa!' my foot!
 
  • Thanks
Reactions: EMT
now days ukisafiri na kurudi salama kwako ni jambo la kumshukuru sana Mungu ati!!!
 
basi la ng'itu hili aisee!!!!! hakuna aliepoteza maisha kwa halli hii Mungu ni mkuu, poleni majeruhi.
 
Barabara nzuri taabu, barabara mbaya tabu tupu sijui hizi ajali chanzo chake hasa ni nini!
 
Tatizo la rushwa, leseni zinauzwa kama njugu. Madereva wasio na udereva wanaendesha gari.
 
Leo pia Bus la Ng'itu liendalo kati ya Dar-Mtwara limepinduka kati ya Nangurukuru na kijiji cha Sinza Wilayani Kilwa...
Ni hiyo hiyo uliyowekwa kwenye picha... hilo ndilo basi la Ng'itu lililopinduka kijiji cha Sinza huko Miteja, wilayani Kilwa karibu na Nangurukulu
 
Waingereza bado hawajabadilisha ushauri kwa wananchi wao wanakuja Tanzania: "Long distance buses are frequently involved in accidents which can often result in fatalities. If you have concerns over the safety of the vehicle or the ability of the driver, use alternative methods of transport."

Tanzania travel advice
 
Back
Top Bottom